Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2021: Viongozi wa upinzani Kizza Besigye na Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) waunda muungano

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1592219180374.png

Viongozi wa upinzani Uganda Kizza Besigye na Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine wameunda muungano wa upinzani.

Robert Kyagulanyi wa vugu vugu la People Power kwa pamoja na Dkt. Kizza Besigye ambaye chama chake FDC kinaongozwa na Amulati, Meya wa Kampala Erias Lukwago wa chama cha DP, Rais wa chama cha CP Keny Lukyamuzi, rais wa chama cha JEEMA Asumani Bsalirwa na wengine wengi wamezindua rasmi muungano mpya wa upinzani kuwa na mshika bendera mmoja katika uchaguzi ujao mwaka 2021 dhidi ya Rais Museveni.

Akizindua rasmi muungana huo katika wilaya ya Wakiso, Robert Kyagulanyi ameutaja muungano huo kwa jina la 'United forces of change' na kusema kuwa kufikiwa walipo, wamepiga hatua kubwa.

''Nataka kushukuru viongozi wetu walioona njia, wakafuata njia hiyo na kutuonyesha njia,'' Kyagulanyi amesema hayo.

Aidha ameweka wazi kwamba hakuna njia nyengine zaidi ya kuungana.

''Ni lazima tushirikiane kwa manufaa ya nchi yetu.'' Kyagulanyi ameongeza hayo huku akisisitiza kuwa njia walioshika ndio sahihi.

Mwanamuziki huyo ambaye pia ni mbunge ameweka wazi kwamba wao (walioungana) sio maadui na kadiri wanavyoendelea kupigana vita wenyewe kwa wenyewe ndivyo wanavyoendelea kuchelewesha mabadiliko ambayo raia wamekuwa wakisubiri kwa hamu.

Robert Kyagulanyi ameeleza kwamba kufikia wanacholenga kunaweza kufanikiwa tu kwa ushirikiano wa watu.

''Natoa wito kwa raia wote wa Uganda musilale badala yake mupaze sauti zetu,'' Kyagulanyi amesema na kusisita kwamba kampeni yao ni ya amani.

Katika hotuba yake, amemnukuu Malcolm X ambaye alikuwa mwanaharakati wa haki za kiraia za Waafrika-Waamerika '' Mikakati inaweza kutofautiana, hatua za kuchukua na mbinu zinaweza kutofautiana lakini lengo likawa moja.''

Chanzo: BBC Swahili
 
beth,

Ni hatua nzuri wamechukua maana kwenye chaguzi ndogo huko manusura wapoteze majimbo yote kisa kugawana kura na chama tawala.

Ila hapo mgombea anapaswa kuwa Besigye, na kyagulanyi aive kidogo sioni kma ni right candidate for 2021 maana hana experience ya uongozi kabisa kuna hatari akawa dikteta zaidi ya aliepo sasa.

All in all it's the right move and wish them best of luck
 
Back
Top Bottom