Nguvu ya Marekani inatokana na nini?

ankai

JF-Expert Member
Nov 25, 2017
3,280
4,236
Najiuliza ili swali kwanini nchi kama Urusi, China, Uingereza, Germany, France na nchi nyingine nyingi tu ambazo ziko juu kiuchumi zenyewe hazina uwezo wa kuzifungia ama kuziwekea vikwazo nchi nyinginezo ambazo zinatofautiana nazo kimaslahi na vikwazo ivyo vikatekelezwa na dunia nzima kama afanyavyo Marekani

Namaanisha kwanini Marekani yeye anaamka tu asubuhi anasema Tanzania nimekufungia kununua ama kuuza hiki na kile duniani kote baada ya tamko ilo la Marekani nchi zote duniani zinafata ilo agizo na zinalitekeleza vyema sana bila ata kupepesa macho yaani nchi zote duniani zinafata kauli ya Marwkani na Tz akiamua kushusha bei ili auze kiurahis akuna nchi inayokubali kufanya naye biashara

Kwani Marekani yeye ana kitu gani cha ziada ama cha zaidi ya inchi nyingine zote duniani nataka kujua kitu gani ambacho exptional tofauti na nchi nyingine yoyote yeye anacho na sisi wengine ama nchi nyingine hatuna
 
Hadi Leo ulikuwa hujajua kuwa USA ni nchi inayoongoja kiuchumi na kijeshi duniani? Kwamba akikohoa hakuna wa kumpinga? Na kwamba akiamua kumpiga yoyote anaweza na hakuna wa kumuuliza?
Sisi tanzania hatuwezi kufanya ivyo
 
Iyo mifumo ni ipi ambayo nchi nyingine haziqezi kuimiliki mkuu
Mkuu kimsingi ili uwe superpower lazima uwe vizuri Kiuchumi na Kijeshi,na kikubwa lazima umwangushe aliyekuwa superpower hapo awali-hizo nguvu za kijeshi na kiuchumi ni kama ingredients katika kufanikisha.

Kumbuka kabla USA hajawa superpower alikuwa U.S.S.R.ambayo iliangushwa na USA kwa vita baridi ya kutumia tu Sera za kiuchumi.Ukisoma mgogoro wa kiuchumi aliyoikumba Dunia has a Nchi za kijamaa miaka ya 1970's ni mgogoro wa kutengeza lengo likiwa ni kuiangusha Russia federation na Nchi za kijamaa na hakika ulifanikiwa na ndio ukawa mwisho wa dola LA urusi.

Tukirudi kwenye hoja yako ya msingi,mfumo mkubwa unao ibeba USA ni mfumo wa kifedha yani matumzi ya fedha ya USA-dolla kutumika kama kiungo kikuu cha ubadilishaji fedha kwenye solo LA dunia.Ndio maana Nchi za BRICS zikaja na mpango wa kuwa na Bank ya pamoja na badaye kuwe na Currency ambayo itatumiwa na washirika kuuziana bidhaa na huduma lengo likiwa ni kuondoa mfumo dollar na Ku gain power.
 
Hadi Leo ulikuwa hujajua kuwa USA ni nchi inayoongoja kiuchumi na kijeshi duniani? Kwamba akikohoa hakuna wa kumpinga? Na kwamba akiamua kumpiga yoyote anaweza na hakuna wa kumuuliza?
Acha uongo! Aliufyata kwa mkorea na hapa majuzi mchina kamwambie ajikite kwa mambo yanayomhusu la sivyo ikibidi nguvu itatumika bado mrusi anaishia kubweka tu akiwa ndani ya geti
 
Najiuliza ili swali kwanini nchi kama Urusi, China, Uingereza, Germany, France na nchi nyingine nyingi tu ambazo ziko juu kiuchumi zenyewe hazina uwezo wa kuzifungia ama kuziwekea vikwazo nchi nyinginezo ambazo zinatofautiana nazo kimaslahi na vikwazo ivyo vikatekelezwa na dunia nzima kama afanyavyo Marekani

Namaanisha kwanini marekani yeye anaamka tu asubuhi anasema Tanzania nimekufungia kununua ama kuuza hiki na kile duniani kote baada ya tamko ilo la Marekani nchi zote duniani zinafata ilo agizo na zinalitekeleza vyema sana bila ata kupepesa macho yaani nchi zote duniani zinafata kauli ya Marwkani na Tz akiamua kushusha bei ili auze kiurahis akuna nchi inayokubali kufanya naye biashara

Kwani marekani yeye ana kitu gani cha ziada ama cha zaidi ya inchi nyingine zote duniani nataka kujua kitu gani ambacho exptional tofauti na nchi nyingine yoyote yeye anacho na sisi wengine ama nchi nyingine hatuna
Teknolojia + Uchumi + Jeshi
 
Back
Top Bottom