Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,735
- 167,782
NIAMBIE RAFIKI ZAKO NITAKWAMBIA TABIA ZAKO. NIAMBIE RAFIKI ZAKO, NITAKWAMBIA KIPATO CHAKO. NIAMBIE RAFIKI ZAKO, NITAKWAMBIA UTAISHIA WAPI MAISHANI. NGUVU YA MARAFIKI NA UWEZO WA KUISHI MAISHA YA NDOTO ZETU.
kuna watu ambao hawajui nguvu ya watu walionao karibu nao wanaathiri kwa asilimia nyingi uwezo wa watu hawa kuishi maisha ya ndoto zao. mawazo, maneno, matendo na hisia unazokuwa nazo unapokuwa na marafiki zako. Haya yote ndiyo yanajenga maisha halisi ya mtu husika.
1. Mtu mwenye marafiki ambao wanawaza jinsi ya kufanya biashara kubwa kama za kwenda Dubai, Ulaya, China n.k, Taratibu mtu huyu huanza kuona naye mwanga na kujihisi anao naye uwezo wa kufanikiwa na kuwa mfanyabiashara kubwa za kimataifa…. Hata kama awali mtu huyu hakuwa na wazo la kufafanya biashara kubwa kama hizo!
2. Mtu ambaye marafiki zake ni watu wanaolalamika kila mara na kudai kuwa maisha yao yameendelea kuwa madogo kwa sababu ya siasa na wanasiasa, taratibu nawe utajikuta silaha za kupambana kupata maisha bora utazitundika, na kuanza kuona kuwa huna uwezo wa kufanikiwa kwa sababu wanasiasa wamechukua kila kitu/ UPOFU WA MAWAZO.
3. Mtu mwenye marafiki ambao muda mwingi wanaongelea vipaji vya watu wengine, taratibu mtu huyu ataanza kuona katika mawazo yake kuwa, kamwe yeye hawezi fanikiwa maana waliofanikiwa ni wale tu wenye vipaji wachache anao washabikia, na kushindwa kujua halisi kuwa naye anacho kipaji. Mtu huyu hupooza kimawazo na kujiandikisha rasmi kwa daftari la kudumu la maskini bora wa duniani! MAISHA YA MTU HAYEWEZI KUKUA ZAIDI SANA YA MARAFIKI WA KARIBU WA MTU HUYU…..MAANA MAISHA YA MTU NI TASWIRA YA UELEWA WA MTU NA UELEWA WA MTU NI TASWIRA YA UELEWA WA MARAFIKI WA MTU. KUMBUKA: Mawazo ni mbegu ya maneno. Maneno ni mbegu ya matendo.
Matendo ni mbegu ya tabia na Tabia ni mbegu ya maisha halisi ya mtu. SWALI LA MSINGI KUJIULIZA NI JE, MARAFIKI ZAKO NI WAPI? Marafiki utujenga na wengine kutubomoa, marafiki hutupa bidii au utukatisha tamaa na kwa nguvu hii ya watu walio karibu nasi, ndugu zetu wengi wamefukiwa makaburini bila kuvitumia vipaji vyao. Mwandishi mmoja akaandika, sehemu moja ambayo ukifika machozi yanakulengalenga ni makaburini:
1. Mwanamuziki mkubwa ambaye amekufa hajawahi kuimba muziki ambao ungelibadilisha tasnia ya muziki aliwaamini sana marafiki zake, kumbe nao walikuwa waoga, walikuwa tayari wamekata tamaa na maisha yao wenyewe….alipoomba ushauri kwa hawa waoga/maskini wa mawazo….wakamkatisha tamaa……sasa mtu huyu siku zake za mwisho zimekuwa za majuto, familia anaiacha ikiwa inaelekea kuishi maisha ya ombaomba.
2.Mfanya biashara ambaye angelifanya biashara ya kubadilisha maisha ya watu wengi, ameenda kaburini hajawai kufanya hivyo, aliogopa kuthubutu, aliomba ushauri kwa waoga, marafiki wake wa karibu…….nao kwa hila au kwa kutokujua kipawa chake, wakamkatisha tamaa!!! SWALI LA KUJIULIZA NI KWA NINI WATU WENGI WANAPENDA KUFANYA URAFIKI NA WATU WENGI WASIO WAJENGA/MASKINI WA MAWAZO/WAOGA? JIBU LA MSINGI NI MAZOEA, WATU WENGI WANAISHI KWA MAZOEA…..AU AIDHA HAWA WATU NDIO WALIO WENGI KUWAPATA!!!.....MAANA MITAA IMEJAA WATU WA NAMNA HII, WAOGA, MASIKINI WA MAWAZO, WENYE HOFU YA KUTHUBUTU,LKN KWA HILA ZAO WALIOJIPACHIKA VYEO VYA WASHAURI MABINGWA WA MAISHA.
Ndg zangu, kipaji alichonacho mtu anakijua mtu mwenyewe na Mungu wake hata wazazi wetu hawajui vipaji vyetum tatizo kubwa ni watu wengi kuamini kuwa kuna mtaalamu bingwa wa kukwambia na kukushauri juu ya kipaji chako, mara nyingi kuwatumia walioshindwa wawe ni washauri wetu!!!!! RAFIKI YAKO WA KARIBU MARA NYINGI ANAWEZA KUWA MWALIMU WA MAISHA YAKO/ COACH. 1. Usikubali kuwa na mwalimu asiyejua njia unayotaka kuendea, atakufundisha nadharia zisizo na mshiko, tafuta kwa bidii uwapate marafiki ambao wameisha pita njia unayotaka kuipita, hawa watakuwa walimu bora, kumbuka vibaya vyajiuza, hivyo zuia kupokea ushauri wa haraka wa vijiweni, ni ushauri wa darasni na si wa maisha halisi. 2. Usipojua marafiki sahihi, kila siku utashi ndoto zao marafiki wengi ndoto zao ni wewe uendelee kuwa chini kimaisha!