Nguvu ya Mahakama za Ardhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nguvu ya Mahakama za Ardhi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Dena Amsi, Apr 13, 2011.

 1. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Wakuu tafadhali msaada kwa huyu mkubwa hapa chini ni ndugu yangu kaniomba msaada na mie sio mtalaam wa sheria msome hapa chini:

  "Nimefungiwa ofisi na mwenye nyumba wangu bila taarifa (Notice) kwa ghafla sana na kafungia kila kitu humo kwa sababu ananidai kodi ya miezi mitatu, nimempeleka mahakama ya ardhi na akapewa amri ya kufungua milango wakati kesi ya msingi inaendelea lakini amekataa kutii amri hiyo na mahakama imebariki hatua yake hiyo kwamba kesi ya msingi iendelee.

  Swali langu ni je amri ya mahakama inaweza kusitishwa bila kusikilizwa pingamizi kwanza?

  Je inawezekana amri ya mahakama kutotekelezwa bila mdaiwa kuchukuliwa hatua za kukiuka amri hiyo?

  Ikiwa vielelezo vya kesi ya msingi vimefungiwa na mdaiwa, mdai anawezaje kuzuia kesi isiendelee mpaka amri ya mahakama imetekelezwa?

  Je hii ni kumaanisha kuwa kuna taratibu tofauti za uendeshaji kesi katika mahakama za jinai na madai au ndio mfumo wa hizi zinazoitwa tribunal courts?"


  Wataalamu wa sheria msaada kwa huyu ndugu yangu.

  Regards

  DA
   
 2. Devils Advocate

  Devils Advocate Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Dec 16, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole. Nenda kalalamike kwa mweyekiti wa baraza la ardhi wilaya kuwa amri ya mahakama haitekelezwi (kama ipo) maana i am sure kwenye suala la kutolipa kodi mahakama haiwezi kutoa zuio lililoombwa maana huwezi ukaenda mahakamani kuomba usilipe. Ukishindwa kwa mwenyekiti nenda wizara ya ardhi kwa msajili wa mabaraza. Otherwise seek lawyers advice.
   
 3. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pole sana kwa matatizo ila hiyo hali iliyokukuta imewakuta wengi sana kwa amri za mahakama zetu kutotekelezwa.
  Kiutaratibu uko sawa kufungua kesi maana unachopinga si kutokulipa kodi bali kufungiwa milango. Kisheria mwenyenyumba haruhusiwi kufunga milango kwa wewe kutokulipa kodi utaratibu ni yeye kwenda mahakamani kukulazimu ww ulipe kodi au mahakama itoe tamko kwamba mkataba umeshidwa tekelezeka kwa ww kutokulipa kodi so uondoke aweke mpangaji mwingine. Sasa kwasababu gurudumu letu la sheria lazunguka taratibu sana basi ndo maana watu hujiamulia kuchukua sheria mikononi.
  Cha kufanya sasa ni kuchukua amri ya mahakama inayomtaka mwenye nyumba afungue milango uende nayo kwa hakimu au jaji umweleze imeshindwa tekelezeka maana mwenye nyumba ameikaidi. Au uende kituo cha polisi chochote karibu waje pamoja na mwenyekiti wa mtaa waitekeleze ama kwa kufungua au kuvunja mlango na wewe kuendelea na biashara zako mpaka kesi itakapokwisha.
   
 4. d

  daisy Senior Member

  #4
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mwambie achukue hiyo amri ya kufungua duka aende nayo kituo cha polisi kufungua shitaka la jinai la kukaidi amri halali ya mahakama. Hilo kosa kwa kizungu linaitwa Contempt of Court.
   
 5. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Thats right Daisy nimemwambia afanye hivyo pia kazi kwake kutekeleza.
   
Loading...