Nguvu ya lugha ya usoni na macho katika mawasiliano

BioPsychologist

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
724
1,014
Hello! Jf members

*TUMIA VIZURI USO NA MACHO YAKO UNAPOKUWA UNAONGEA NA MTU*

```Mawasiliano ni moja kati ya vitu mhimu sana katika maisha ya kila siku, ni vigumu kuishi bila kuwasiliana, iwe ana kwa ana, kwa simu, kopyuta, barua, n.k lakini hapa nachotaka kukwambia ni kuhusu mawasiliano hasa ya ana kwa ana yanayohusisha lugha ya maneno,usoni na machoni.(facial expression and eye contact)

Mawasiliano ni jinsi unavyoonekana(usoni) na vipi unasikika (maneno) inaweza kuwa mhimu sana zaidi ya maneno unayoyasema inapokuja swala la kueleweka kwa mtu unaezungumza nae ana kwa ana, mwonekano wa sura ya mzungumzaji unabeba ujumbe mkuu ulioko ndani na huvaa ukweli halisi.

Ikiwa nguvu ya lugha ya usoni na matumizi ya macho katika mawasiliano ni mhimu sana, inaweza kusaidia kupata ujumbe na matokeo ya msemaji na kile anacho maanisha, mfano,; lugha ya usoni na macho vinaweza kuonyesha mihemko saba (8) ya kihisia ifuatayo:

✍ 1. Furaha. 2. Huzuni. 3. Hasira. 4. Hofu/Woga 5. Kupendelea/Uhitaji/Maslahi. 6. Mshangao. 7. Kinyaa. 8. Aibu

Hii mihemko ya kihisia huanza kuonekana katika uso na macho ya mtu pale anapohisi kuwa na kisababishi (mtu) au hata anapohisi na kupata taarifa kuhusu kisababishi mhemko ( MTU au hali yeyote) ndipo uso hubadilika na macho hubadilika na kupoteza uhalisia wake, mfano, umbo la macho huonekana kubwa au dogo, kuwa mekundu, kutoka machozi, kukodoa,kufumba na kufumbua macho kwa haraka haraka n.k

Katika USO kwa ujumla huonesha dalili mbali mbali, mfano; uso kukunjamana, mdomo kuwa mzito katika kuongea, kucheza kwa nyusi za macho, kuinamisha kichwa, kukaza macho, kuangalia pembeni hasa upande wa kushoto, kung'ata mdomo wa chini (buttom lip) n.k

Matokeo yake ni kwamba mwonekano wa USO huweza kuonesha unachomaanisha kabla ya kusema, ndo maana watu hupenda kuangalia sana usoni mwa msemaji anaekuwa yuko mbele ya kundi la watu, unapokuwa unaongea au kusema asilimia kubwa ya viungo vyako vya mwili vinavyokupa na kutoa ushirikiano ni usoni zaidi kuliko pengine hivyo tumia vizuri uso wako unapokuwa unaongea na watu.

Unapokuwa unaongea na mtu au watu jitahidi kuongea uhalisia wako, epuka sana kuingiza vitu katika mazungumzo ambayo hujapanga kusema, maana ake ni kwamba uso na mwonekano wako utakuumbua pale ambapo utaanza kusema kitu ambacho hukukusudia bali umepaparika na kujikuta unasema, hii ni hatari sana maana hupunguza uaminifu.

Epuka sana kuongea ongea bila mpangilio (kuwa makini sana) hasa ukiwa unajisikia una furaha kubwa sana au huzuni nyingi sana, maana moja kwa moja ukishindwa jizuia huweza kukufanya hata usitamke maneno sahihi uliyoyakusudia badala yake utaongelea wengine au wewe mwenyewe na kujikuta unaenda nje na mada.

Mwonekano wa usoni (kabla ya kuongea chochote) ndiyo huweza kutafsri maana ya ndani ya kile unachofikilia, mfano,. Huzuni, hasira, furaha, kinyaa, kupenda, hofu, mshangao .n.k, hivyo kabla ya kusema jambo mbele ya mtu au kikundi cha watu hakikisha unakaa kwanza na kuweka hisia zako ziwe sawa.

Katika watu wengi wanaofanya na kufanyiwa interview, wengi wao huwa kiwango chao cha kujiamini kinatokana na mwonekano wa usoni na machoni, sina maana kwamba wote wnaokuwa sawa katika facial expression huwa wanashinda , lakini ni kwa kiwango furani huonekana kama wajasiri wanaojiamini na kupewa kipaumbele zaidi.

Usidhani nina maana kwamba ukaze sana uso ndipo uonekane mjasiri hapana ,bali hakikisha kwanza kabla ya kuongea na mtu umejiandaa na kuandaa cha kusema (madam) kama unaona kuna taarifa umesahau ni bora ukaahirisha kusema au ukapanga mda mwingine baada ya maandalizi mazuri, ikiwa utasema huku una utata moyoni mwako ni rahisi kugundulika kama anaekusikiliza yuko makini na mwonekano wa uso wako.

Kama unasema na mtu huku ume relax then unachokisema kitatoka kime relax pia na ujumbe wako utakuwa natural maana utatoa mawazo hasa uliyoyakusudia, lakini ukiwa una mashaka sana na kileunachokisema zaidi ni kwamba utababaika sana katika maneno na hasa usoni na machoni utaonekana unasema kisicho halisi.

Vile vile mtazamo wa macho yako dhidi ya yule unaesema nae ni bora sana katika mawasiliano, kama unakwepesha macho, moja kwa moja inaonyesaha hisia na tabia yako iliyoko ndani kwa wakati huo kama nilivozitaja hapo juu.maana macho yana wasiliana sana kuliko part yeyote ya mwili wa MTU pale anapokuwa anazungumza ana kwa ana.```

✍ *Making and maintaining eye contact can have positive outcomes in the groups and during individual communication. Eye contact can be used to indicate to a person that you are receptive to what they have to say. Additionally, eye contact may indicate that you want to communicate with a person. Finally, eye contact can be used to express respect for a person by maintaining longer eye contact.*

```Ukweli ni kwamba watu ambao macho yao yanakuwa relaxed wakati wa kuzungumza, wanakuwa wanazungumza asilimia kubwa ya uhalisia na ukweli kuliko ambao macho yao hayatulii, na mara nyingi mtu asiyeongea uhalisia au ukweli hawezi kutanisha macho yake na mtu anaemsikiliza kwa mda mrefu, bali huwa ana pepesa sana maana hujijengea hofu kabla ya kusema.```

*Kumbuka*

```Kuna watu nyuso zao na macho yao zinaweza kuwa na tabia ambazo hujazoea,hivyo itakuchukuwa mda kumwelewa mhusika kama facial expressions and eye contact yake ni halisi au sio halisi, hivyo basi ni bora kuwa mdadisi wa mapema haswa kabla ya kuhitimisha au ku judge tabia ya MTU na hisia zake kupitia usoni na machoni kwa ujumla.

Ahsanteni sana!!
 
Hizi kitu huwa ni 50 50, hakuna uhakika kamili. Kuna watu wanakudanganya vizuri tu huku macho wanakukodolea adi wewe mdanganywa ndio unaona aibu.

Hii kitu ni Arts hivyo wapo Artist wakuitumia vile watakavyo.
 
Somo Murua kabisa hapa, kuna kitu nimejifunza hapa, mbinu kadhaa zitanisaidia kuwa na kujiamini zaidi na kuondoa uoga hapa na pale..
Poa mkuu
 
Back
Top Bottom