Nguvu ya kucha na nywele katika ulimwengu wa kichawi

Nguvu ya kucha na nywele katika ulimwengu wa kichawi

Bana Balume

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2017
Posts
999
Reaction score
2,730
Nawasalimu wanaJF,

Leo nimeona ni vyema niwaletee makala hii fupi kuhusiana na kucha na nywele zinavyo husika katika ulimwengu wa kichawi ulimwengu huu ni mpana sana mimi nimejitahidi kuweka kile kidigo nilicho pata, basi bila kupoteza wakati twende sawa.

Nywele na kucha zinaaminika kuwa na nguvu sana katika ulimwengu wa kichawi hivyo vimekuwa viungo muhimu katika kutengeneza uchawi (magic spells).

Pia Nywele zinahusishwa kubeba nguvu ya mchawi mhusika na pia ni kama kinga, katika historia za miaka ya nyuma, kuwa na nywele nyingi iliaminika kuwa ni moja wapo ya alama ya utajiri na nguvu kwa wafalme wengi, pia Wamisri wa zamani waliamini kuwa dawa iliyotengenezwa kwa nywele, vipande vya kucha na damu ya mwanadamu inampa mtu nguvu nyingi zaidi kuliko wengine.

Kama nilivyoeleza awali, nguvu za kichawi za mchawi zimefungwa kwenye nywele zake hivyo katika kutengeneza uchawi mchawi akitikisa nywele zake nguvu ya huo uchawi inaongezeka mara mbili.

Katika ulimwengu wa nguvu za kichawi kukata nywele kunachukuliwa kama kitendo cha kumdhoofisha mchawi na kupoteza nguvu zake pia ni udhalilishaji au adhabu.

Samsoni japo hakuwa mchawi alipoteza nguvu wakati Delila alikata nywele zake hii inaonesha ni kwa jinsi gani nywele zinaweza kubeba nguvu za mtu husika katika ulimwengu wa kiimani pia Wabils wa India ya Kati walitesa wachawi wanaoshukiwa, kisha wakakata nywele zao na kuzika ili kukata uhusiano kati ya wachawi na nguvu zao za kichawi hii hata Tanzania huwa inatokea sana pale wachawi wanapokamatwa, wachawi walinyolewa kwa imani kwamba iliwafanya wasiwe na nguvu na uwezekano mkubwa wa kukiri; pia, walinyolewa kutafutwa alama katika miili yao ambazo zinaweza kutambuliwa kama alama za Ibilisi.

Kucha ndefu huwa zinahusishwa kwa kiasi kikubwa na mashetani au majini ndio maana katika utamaduni wa Wayahudi na jamii zinginezo ni marufiku mtu kufuga kucha ndefu hivyo huhakikisha kucha zao ni fupi muda wote pia makabila ya huko Madagaska wanaamini kuwa Ibilisi au majini huishi chini ya kucha zisizo katwa yaani kucha ndefu.

Habari hizi za nywele na kucha ndefu katika ulimwengu wa kichawi zinatupeleka nyuma hadi katika Vendidad kitabu cha Zoroastrian kilichoandikwa katikati ya karne ya 5, Kulingana na yaliyoandikwa katika Vendidad, nywele na kucha ni vyombo/viungo muhimu katika ulimwengu wa uovu kwa sababu nywele na kucha hukua katika maisha yote ya mwanadamu hivyo vinaweza kutenganishwa na mwili ili kutumiwa na wachawi kuita mizimu na majini, kuroga na kutengeneza uchawi (spells) katika kipindi hiko mtu ajulikanaye kama Ahura Mazda alitoa mila maalumu iitwajo Zarathustra kwa utupaji salama wa vipande vya nywele na vifurushi vya kucha ambayo ina husisha kuzizika/kuzifukia ili zisiweze kutumika katika shughuli za kichawi.

Mila ya kuzika/kufukia nywele zilizokatwa na kucha iliendelea katika jamii nyingi watu walikuwa wanatupa nywele zao na kucha kwa siri sana kwa maisha yao yote mila hii ilikuwa ikitumiwa katika jamii nyingi sana hasa ndani ya bara la ulaya katika kipindi hiko.

Pia waganga wa jadi katika jamii hizo walikuwa wanatumia nywele za mtu aliyerogwa na wachawi kutengeneza dawa kuponya mtu aliye athiriwa na nguvu za kichawi, nywele za mwathiriwa aliyerogwa zilitupwa ndani ya moto iliaminiwa kuwa kadri zile nywele zinavyo ungua maumivu ya moto hurudi kwa mchawi aliyemroga mtu huyo.

Wakati huo watu walitumia nywele za mtu aliyekufa kama njia ya kuwadhoofisha maadui zao kwa kuchukua nywele za maiti na kuzifukia chini ya kizingiti cha mlango wa adui inasemekana ilisababisha adui kupata ugonjwa wa homa kali na kutetemeka endapo atazivuka zile nywele pia Katika sehemu za Ujerumani, walikuwa wanatumia begi dogo la nywele laini za binadamu kufunga juu ya tumbo la mtu ili kujua mtu huyo amerogwa au laah kama mtu huyo amerogwa basi zile nywele ni lazma zijinyonge nyonge baada ya siku tatu kama nywele hizo zikitoka zimenyooka ilimaanisha mtu huyo hajarogwa.

Nywele, haswa zile za sehemu za siri (mavuzi) inachukuliwa kama kiungo chenye nguvu katika kutengeneza hirizi au dawa za mapenzi, Kulingana na vitabu mbalimbali, John Fian, mchawi wa Scotland wa karne ya 16, alijaribu kumfanya msichana mdogo ampende kwa kutengeneza dawa kwa kutumia nywele tatu za sehemu za siri kutoka kwa msichana huyo kwa bahati mbaya akatokea mtu akazibadilisha zile nywele za yule msichana na kuweka nywele kutoka kwa kiwele cha ng'ombe John Fian yeye bila kujua akatengeneza dawa kwa kutumia zile nywele hatimae ng'ombe alimpenda Fian na kuanza kumfata mji kote hata hivyo bado ni kawaida kwa wapenzi kubeba vifuniko vya nywele za kichwa, na katika karne zilizopita, wasichana wadogo mara nyingi walitengeneza bangili za nywele kuwapa wapenzi wao ili waendelee kuwa waaminifu.

Katika jamii za ulaya watu waliamini kuwa watu wenye nywele nyekundu ni wachawi, kulingana na imani moja ya zamani ushahidi upo kuonyesha kwamba kuna wachawi wa kipagani walipaka nywele zao rangi nyekundu kama mila katika ulimwengu wa kichawi, pia nywele nyekundu zilikuwa ni kawaida kwa Weltel ambao mila zao zilikuwa zimejaa uchawi pia wakati wa uwindaji wa wachawi watu wenye nywele nyekundu mara nyingi walishukiwa na kukamatwa na uchawi.

Kulingana na ushirikina, kukata nywele ni lazima kuendane na wakati kulingana na majira ya mwezi kulingana na jinsi mchawi anavyotaka nywele zikuwe na nguvu ipi kwa haraka.

Ni hayo tuu, nawasilisha.
 
Kwanini huwa hatufunzwi mambo kama haya siyo lazima uwe mchawi au mganga lakini haya mambo yako kwenye jamii zenu ilibidi tuwe na ujuzi nayo kwa uchache namna ya kuepuka vitu fulani fulani jinsi ya kudeal navyo vikitokea.
 
Kwanini huwa hatufunzwi mambo kama haya siyo lazima uwe mchawi au mganga lakini haya mambo yako kwenye jamii zenu ilibidi tuwe na ujuzi nayo kwa uchache namna ya kuepuka vitu fulani fulani jinsi ya kudeal navyo vikitokea
Tatizo ukiwa una disclose sana mambo haya watu hawachelewi kukushuku kuwa jamaa ni mchawi.
 
Kwanini huwa hatufunzwi mambo kama haya siyo lazima uwe mchawi au mganga lakini haya mambo yako kwenye jamii zenu ilibidi tuwe na ujuzi nayo kwa uchache namna ya kuepuka vitu fulani fulani jinsi ya kudeal navyo vikitokea.
...Tatizo kubwa no kuwa Tumeloea mno kwenye kuamini kuwa kila kitu cheti no cha Kishenzi wakati waliosema hivyo kumbe wenyewe wanayo kama yetu wanayoita ya Kishenzi...!![emoji53][emoji53]
 
...Tatizo kubwa no kuwa Tumeloea mno kwenye kuamini kuwa kila kitu cheti no cha Kishenzi wakati waliosema hivyo kumbe wenyewe wanayo kama yetu wanayoita ya Kishenzi...!![emoji53][emoji53]
Yeah ukisoma hiyo makala utaona jamii za ulaya ndio zimekubuhu katika hizo ishu
 
Elimu nzuri sana hii, ila jinsi tumetawaliwa ukolon mambo leo kuna watu watakwambia unafunza jamii uchawi. Hata ukisema chumvi ni dawa ya uchawi utaambiwa wew ndio MCHAWI ila yale mafuta na maji ya baraka ambayo yanawekwa CHUMVi kwakuw yanatoka ulaya au ni elimu ya watu weupe vinathaman sana. Wakat chumvi n ile ile na maji ni yaleyale ila ngumu kuwaambia watu ile ni miradi ya upigaji, ushawahi sikia bei ya yale maji na mafuta???????
 
Umeongea uongo ndugu nywele na kucha hazihusiani na uchawi kama hivyo
katika uchawi tunatumia nywele au kucha sababu ndio sehemu ya mwili wa mwanadamu ambayo tunaweza kuipata kirahisi pasipo kumuumiza na tunapata dna yake moja kwa moja,
ndio maana wakikosa nywele au kucha wanaweza kuiba nguo yako ambayo inakuwa tayari ina chembe chembe za dna zako,
na uchawi huo unatumika katika mambo makubwa mawili
unapotaka kumroga mtu asiyekuwa ndugu yako ama unahitaji kumuunganisha ama kumfungamanisha na viapo fulani fulani,

kuna raha sana yakuelewa uchawi kiuhalisia kutoka kwa wahusika wenyewe kuliko kuchukua kutoka katika masimulizi.
na samsoni kwakweli Nywele ilikuwa ni sehemu ya Agano la Mungu ilikuwa ni alama tu wala nguvu hazikukaa katika nywele na SAmson pale alipozihitaji nguvu aliomba yaani akimaliza kuomba tu nguvu zimemjaa,
ndio maana mwisho anapokufa japo alikuw ahana nywele aliweza kuomba toba yakuvunja agano lake na Mungu kisha akaomba tena nguvu zikamjia

Pia katika uchawi kuna nguvu sana katika kunyoa nywele sio kufuga mwogope sana mchawi ambaye anakuwa anakipara mda mwingi zaidi kuliko mwenye nywele,
kuna matambiko yenye nguvu na ibada za kunyoa nywele katika ulimwengu wa kichawi

pia unapokuwa unasoma habari za uchawi mara nyingi kwa africa inakuwa ni tofauti kdigo na wazungu kimaelezo sababu za kijiographia
pia ukiingia ndani ya africa uchawi wa mara hauwezi kuwa sana na uchawi wa singida au mbeya na iringa.
ila kuna baadhi ya mambo yapo kwa usawa karibia jamii zote duniani ni mambo yapo yanahusiana na misngi ya dunia moja kwa moja kama nywele na kucha nk
 
Sasa unajitekenya halafu una cheka mwenyewe, umesema nywele na kucha havihusiani na uchawi tena umesema katika uchawi unatumia nywele au kucha, yaani ni full contradiction.

Unataka kuniambia hujawahi kuona wachawi wakikamatwa wananyolewa nywele?
 
Acha uongo uchawi ni sayansi, Sayansi ni kipande kidogo tu cha Magic. Nywele na kucha vinachukuliwa na wachawi kwakua vinabeba DNA mtu husika. No more than that
Unakosea sana kujaribu kulinganisha science issues na maswala ya spiritual practices

Katika ulimwengu wa kisayansi utasema kuna connection ya DNA lakini katika ulimwengu wa kichawi wanakwambia kuna connection kiroho, sasa unaweza kuprove roho iko wapi ktk mwili wa mwanadamu sababu science is all about proofs
 
Back
Top Bottom