Nguvu ya kitanda

Focus120

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2014
Posts
1,092
Reaction score
798
Utafiti umeonyesha baadhi ya vitu vilivyosababisha ndoa za babu zetu zidumu ilikuwa babu na bibi kulala pamoja kwenye vitanda, ngozi za wanyama au mikeka yenye ukubwa usiozidi futi 2.5.

Umbali wa futi 2.5 uliwawezesha wanandoa kuwa pamoja na kugusana usiku kucha.-
Hiyo iliwalazimisha waongee hata kama wamegombana mchana, maana bila kusema sogea huko huwezi kupata nafasi ya kulala.

Baridi ilivyokuwa inaongezeka kunapokaribia kucha iliwalazimisha wasameheane hata bila ya kuombana samahani, maana kugusana kule kuliwapa joto lililokuwa linafuta lenyewe makosa yote waliyofanyiana mchana na kuanza upya.

Vitanda vyetu vya 6 x 6 vinakwenda anti-clockwise na kazi iliyokuwa inafanywa na vitanda vya akina babu.

Vitanda vyetu havina ubavu wa kufuta makosa ya wanandoa waliyofanyiana mchana. Kila mtu anakuwa kwenye kona ya 6x6 na kujisikia aibu kuanza kumgusa mwenzie, nani aanze kupandisha mguu kwenye paja la mwenzie wakati kulikuwa na ugomvi?

Ngoma inakuwa droo hadi asubuhi na ugomvi ukiwa palepale na kila mtu akijfanya nunda wa kukataa kujishusha kwa kusema samahani ama kumpapasa mwingine.

Rudisheni vitanda vyenu kwa fundi seremala avipunguze viwe 3 x 6 ili viweze kuwasuluhisha wanandoa mnapokoseana sio kwenda kwa mshenga, shoga, wazazi, majirani kutafuta suluhu.

CHANZO: sky Tanzania. Subject to minor edits.
 

Attachments

  • 1444739150341.jpg
    25.2 KB · Views: 2,060
Babu na bibi zetu Waligombana bwana, ndo maana babu alioa wake watatu na kuendelea....tafakari


Ila ushauri wako una mlengo sawa....nimependa mawazo positive uliyoleta
 
Babu na bibi zetu Waligombana bwana, ndo maana babu alioa wake watatu na kuendelea....tafakari


Ila ushauri wako una mlengo sawa....nimependa mawazo positive uliyoleta

Anza mchakato Wa kuchonga 3 x 6
 
Tena sasa hivi kuna mivitanda king size!!!na mimito ya kila aina tunaijaza kitandani.
😂😂😂😂😂😂 ila mimi siruhusu kulala bila kulalalana na kukumbatiwa!!!
Hakyamungu usingizi hauji...
So most of the time nayamaliza mwenyewe kuepuka kusinzia ofisini
 
Vitanda vya 2.5×6 sasa na zile staili za kukunjana kama samak ztafanyikaje?
 
kuna jamaa alisema kuna staili ya pakachongo sasa sijui kama inafaa kwenye 2.5x6.
embu mzee wa pakachongo njoo ufafanue
 
hahahahahahaha.
umenikumbusha mapenzi ya kwenye deka.
unachosema ni kweli mkuu. nlikuwa naishi hostel mwanzo, badae nikapanga nkaeka bed ya 5 by 6, ikawa ukimwaga ugali namwaga mboga.
 
Kitanda changu kikiwa kikubwa sana hakizidi 4 kwa 6.
Na hata iweje siruhusi tuingie kulala tukiwa tumekasirikiana, yaani i wont sleep, na kwakuwa usingizi ni starehe niipendayo na siko tayari kuikosa, nitahakikisha tunayasawazisha kabla ya kulala
 
mi namiliki 4 kwa 6 vipi bado kikubwa au
 
Mkuu umewaza mbali sana.
Ama kweli old is gold...
 
Hiyo hiyo sita kwa sita najisogeza karibu hata kama kanuna au nimenuna
 
Ila zamani sijui walikuwa wanafanyeje romance... maanake.. miswaki hakuna. Marashi hakuna. Sabauni hakuna.
 
Uko vizur n tht makes me hav wishful thinking...
 
Ila zamani sijui walikuwa wanafanyeje romance... maanake.. miswaki hakuna. Marashi hakuna. Sabauni hakuna.

Walitumia miti kupiga mswaki..

Walitumia sabuni za mipapai
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…