Nguvu ya hofu katika kuleta matokeo halisi

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,229
3,525
Habari za mda huu wakuu. leo napenda kushare na nyie kisa kimoja kilichowahi kunikuta katika enzi za ukuaji wangu hakika ukiambiwa ujana maji ya moto basi amini ni kweli ujana ni maji ya moto haswaa!

Basi bwana nakumbuka ilikuwa mwaka 2013 nilikuwa kidato cha sita mkoani Mbeya shule kwenye mabano, Siku moja nimekaa zangu chimbo flani maarufu kama chimbo la maficho kuwepa bakora za mwalimu wa zamu, gafla nyuma yangu nikasikia hatua nikasema my GOD hapa NIMEKUTWA NA BWANA PEPSI, wacha banaa kuangalia kumbe kalikuwa katoto ka olevel nako kalikuwa katika harakati za kutafta pakujihifadhi, basi bana waharifu wote tukajibana pale chimbo ila kale katoto mashalaah kila nikikatupia jicho naona nako kananitupia jicho la kiwiziwizi tukitazamana kunakuwa na nguvu ya silent commnication baina yetu wote ikabidi nivunje tu ukimya nikakauliza namna ya kukapata kakasema kama ninasimu nikaandike namba yangu, basi mzee chap nikakaandika namba na baada ya assembly kuisha watu kuingia madarasani tukaagana nikaenda darasani nako kakakimbia darasani kwao, kwa ile shule madarasa ya olevel na advance yalikuwa mbalimbali na tulitenganishwa na kaukuta flani ivi kiasi kwamba olevel tulikuwa hatukutani nao mara kwa mara, ilikuwa nadra sana tena ni kwa wale vihelehele tu ambao walikuwa wanaleta shobo kwa vidume wa advance ila assembly tulikuwa tunashare.

Haya picha linaanza muda wa break ile tumerudi mabwenini kwa ajili ya maandalizi ya chai, kwa waliopita shule wanajua hapa mabaharia lazima break ifikie kwenye kichatio kwanza kabla ya kuchukua kikombe ''Wacha bana nimekutana na sms karbia 50 namba ngeni kuchunguza nikagundua ni kale katoto yaani kamemaliza kila kitu mimi nilitaka nikatongoze ila cha ajabu kamemaliza kila kitu yaani kameniomba kenyewe nikapige "mbupu",,, sasa maswali yangu yakabaki kuwa huyu mtoto mbona yupo darasani ametoa wapi simu na mda wa kutuma sms zote hizi? sikujali sana maana lengo lilikuwa anitafte ko kama kanitafta ndio ilikuwa furaha yangu baharia wa nchi kavu.

Haya bana mawasiliano yakaendelea hadi ikafika siku ya siku nikakanyandua kikatili sana tena nilienda kwao, na ikawa mazoea natoroka shule naenda kupiga mbususu na nilikuwa nakuta kapo kenyewe hapo linaandaliwa diko la maana alafu wahuni tunazama chumbani kukulana, sasa siku moja nipo na dogo flani ivi wa olevel mshikaji wangu tunapiga story mara kakapita kakatupa hi kakasepa dogo kaniuliza unamfahamu huyo dogo nikasema yap sikutaka kumpa mchongo mzima maana madogo wa olevel akili zao hazijatiulia muda mwingine, ila nikamuuliza dogo kwani vipi?

Basi dogo kaanza kunipa mchapo kuwa bana huyo dogo ni jirani yake na muuwaji haswa maana dogo kiafya hayuko sawa na analijua hilo na anapambana sana kutafta wadau wa kwenda nae na kila siku hom kwao anakatazwa tabia za kusambaza ngoma kimaksudi ila hasikii ,,, jamaa kanisimulia kuwa dogo hata nyumbani siku nyingi halalagi, anaenda kujiuza, aseeh nilichoka wakuu afu nikirudisha picha ndio nakumbuka kuwa dogo alinitafunia mwenyewe nikameza aseeh acha tu wakuu hii isikilizie kwa jirani yako

Sasa kilichoongezea nyundo kwenye msumali ambao tayari ulikuwa ushapigwa kwenye kidonda ni baada ya wiki moja after iligongwa kengere ya dharula tukaenda assembly mara anakuja mama mmoja na yule dogo assembly na kutangaza official kuwa ameamua kufanya vile alete yule dogo amtangaze shuleni ili aokoe wanafunzi wa kiume maana imekuwa too much yule dogo kutoka na wavulana wa advance kimaksudi kwa kuwa sio wenyeji na hawajui profile yake kwa mara ya kwanza naona yule mama anakiri kuwa yy na mwanae wote ni waathirika na akatuonyesha hadi vidonge. Asee kuna watu wanajiamini dunia hii and kuna watu wazuri na wema sana.

Sasa picha linaanza yule maza kabla hajamaliza kutoa speech nikaona mhuni anaangua kilio na kutoka mbio kwenda kusipojulikana ikabidi tena watu waanze kukimbizana nae hadi kumkamata mwamba ni kulia tu mda huo mimi pale hata miguu haina nguvu tena , yaani nilikuwa nafikiria picha za misiba tu kichwani kama movie ya kikorea.

Hapa sasa ndio baada ya wiki kadhaa nilianza kukonda kwa kasi ya 5G kichwa hakikatiki kuharisha mara kwa mara, na kila dalili zote ambazo ulishawai kuziskia mkuu zilitokea kwangu nakumbuka nilipima nikakutwa nina Uzito wa kg 37 nikiwa form six huu ni uzito wa mtoto wa darasa la tatu au nne. sasa take image 37kg form six. nilikuwa najitahid kudanganya akili ili nipate walau furaha ila nafsi inasaliti mwili na akili inauambia mwili wewe enjoy tu ila mimi utanikuta nimekaa pale pembeni nakusubilia uje twendelee na masikitiko,
Kuna mda nilipomaliza shule nikajiunga na chuo nikajisahaurisha kidogo nami nikajiamulia kuwa sitakufa peke yangu nikafungulia paipu kila anaekatiza mbele yangu namkula na nilisahau kabisa habari za kinga nilikuwa nafanya maksudi ili nipate wengi wa kwenda nao maana kwa utoto niliokuwa nao nilikuwa najua UKIMWI ndio mwisho wa maisha.

Mwenyezimungu aliniondoa katika utumwa huo baada ya kumpa mimba mwanamke mmoja na akaahidi kuilea na alipoenda cliniki kwa mara ya kwanza nilimblock kila sehem nikijua majibu kuwa yatakuwa yaleyale ninayoyajua ila chakushangaza ametoka clinic ananipigia yupo blacklisted akaja geto ile nasubiria aniambie alichokutana nacho cha ajabu ananiambia amepima ni mzima, SEEH nilimuuliza mara mbilimbili hadi akashtuka na kutambua shauku yangu ila nikavunga tu, hapo nami ndio nikawaza inabidi nami nikapime pengine naweza kuwa sawa na baada ya kupima cha ajabu et mwamba nikawa niko ok. Na hadi sasa nina watoto wawili na the same woman ndio mke wangu am enjoying my life japokuwa kuna changamoto za tozo na kodi ila tunaishi na nina amani... Ila huwa ninajiuliza pasipo wife kubeba ujauzito hatma ingekuwa kitu gani?

USHAURI WANGU KWA WADOGO ZANGU MLIOKO MASHULENI NINAJUA KABISA KWA VIZAZI VYENU SMARTPHONE MNAZO NA HAPA JF MNAPITA KUCHUNGULIA MAMBO YA WAKUBWA. KUWENI MAKINI SANA MAISHA YA UANAFUNZI NDIO HUPOTEZA WENGI NA NDIO NKIPINDI WENGI HUHARIBIKIWA NA KUHARIBU HATMA ZAO. PIA KUWENI NA MAZOEA YA KUPIMA AFYA YAKO UNAPOHISI KUNA TATZO HOFU INAUA KULIKO TATIZO JENYEWE.

Sent from my SM-G988N using JamiiForums mobile app
 
Aisee hongera kwa kukutwa mzima, je ulikua unahofia sababu hukua ukitumia kinga na yule mwanafunzi wa o level?.
Huu ugonjwa muda mwingine unaconfuse jinsi unavoambukiza, Tuendelee tu kujilinda
 
mkuu watoto wa level hizo hakuna anaetumia kinga wanapigana kupekupe tu ila mungu anawalinda kwa kweli mimi nilikuwa napiga peku tena shoo shoo kweli yani hata kwa siku mara 2 kwa nyakati tofauti ndio maana nilijua pale sijachomoa

Sent from my SM-G988N using JamiiForums mobile app
 
Mada za kujisifia uhuni, uasherati na uzinzi, bahati walimu wa nidhamu hawakuona, suspension ingehusika
 
Mada za kujisifia uhuni, uasherati na uzinzi, bahati walimu wa nidhamu hawakuona, suspension ingehusika
mkuu punguza stress hiki kipindi ni cha mpito tu kodi ya jengo utalipia tu hata kama hauna hela ya kodi ya chumba aliekuambia ninajisifia ni nani mimi nmeshare kisa kama funzo na ujana unamambo mengi sasa ulipokurupuka kutoka chooni kwanini hujatawaza
 
Aisee hongera kwa kukutwa mzima, je ulikua unahofia sababu hukua ukitumia kinga na yule mwanafunzi wa o level?.
Huu ugonjwa muda mwingine unaconfuse jinsi unavoambukiza, Tuendelee tu kujilinda
Deception alinifungua macho sana kwenye janjajanja ya ugonjwa huu.
 
Back
Top Bottom