Nguvu ya Chakula inavyoweza kukujenga au kukubomoa

Nguvu ya Chakula inavyoweza kukujenga au kukubomoa

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,037
Reaction score
168,688
NGUVU YA CHAKULA
Yakobo alinunua haki ya mzaliwa wa kwanza kwa chakula (dengu) Yonathani alifunguliwa macho kwa kula(asali), Isaka alihitaji chakula kitamu ambariki mwanae( Esau) japo Yakobo aliwahi, Eliya alitoa suluhisho la njaa kwa mama mjane kwa sharti la kula yeye kwanza, Abigaili alimnusuru mumewe Nabali kwa kuleta chakula kwa Daudi, Watu walijaa mkutanoni kwa Yesu kumsikiliza na kusubiri mkate maana aliwahi walisha, Yusufu alipanda cheo kwa kutoa wazo zuri namna ya kutunza chakula.
HII NI BAADHI TU YA MIFANO MIZURI YA CHAKULA KWA WALIOKITUMIA VIZURI KILILETA MATOKEO MAZURI.

Lakini njaa pia ilimfanya Esau auze haki ya mzaliwa wa kwanza, tamaa ya macho kwa tunda ilimfanya Eva amsikilize shetani, Israel ilienda utumwani( Misri)kwa sababu ya njaa. IPO MIFANO MINGI MIBAYA AMBAYO ILILETA MSIBA KWA WALIONASWA NA NGUVU YA CHAKULA.

Nimalizie kwa kusema NJIA YA MKATO KABISA( SHORTCUT) KUPATA KITU UNACHOKITAKA NI CHAKULA, NA NJIA FUPI YA KUINGIA UPOTEVUNI PIA NI CHAKULA.

Ukitaka kuutawala moyo wa mtu kwa haraka, njia rahisi zaidi pitia tumboni kwa kutumia chakula, MATAIFA YANATUMIKIA MENGINE KWA SABABU YA NGUVU YA CHAKULA, Watu wanasalitiana kwa sababu ya chakula, wanaume wanahama nyumba zao kisa chakula, wanawake wanasaliti ndoa na kuvunja uchumba kisa chakula. UKIWEZA KUDHIBITI TUMBO NA NJAA JAPO ITAONEKANA UNACHELEWA KUFANIKIWA, ILA MAFANIKIO YAKO LAZIMA YATAKUWA YA KUDUMU NA YENYE HESHIMA SANA.
 
Hata ndoa nyingi pia zimepoteza ustawi kwasababu ya chakula,.wake wanapikia waume/familia zao makorokocho lol,.badala ya kutulia jikoni mwanamke ukapika chakula ambacho mumeo akienda kazini anakitafakari siku nzima mpaka anaona kuchelewa kurudi nyumbani aje kula vinono,ukipika chakula kitam jamanii hata watoto wako hawawezi kuwa doezi kwa majirani,.lazima amiss chakula cha mama nyumbani na muda wa kula ukifika watoto hawachezi mbali,.lakini ukipika ushuzi hahaha utapata tabu sanaa!!!!
 
Hahaha eti 'ukipika ushuzi'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pia, mama yangu ndie mtu pekee duniani aliyenipikia chakula kizuri na sasa nina nguvu na afya.
 
Back
Top Bottom