Elections 2010 Nguvu ya CDM moto mkali kwa CCM

yutong

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
1,601
338
Hayo yote tunayoendelea kuyashuhudia ni kutokana na moto mkali uliowashwa na CDM. Tunaweza kusema hivi kama sio Chadema je Lowasa angejuzulu? kama sio CDM CCM wangejivua Gamba? katiba kusitishwa kujadiliwa bungeni unadhani ni nguvu ya nani? Je makamba angeng'ooka kwenye nafasi ya ukatibu CCM? je rostam aziz angejiuzulu ubunge? Anayewaona Chadema hawana maana yeye ndo atakuawa na matatizo.

Ni katika hali hiyo nathubutu kusema kwamba kwa moto huu waliouwasha CDM utaendelea kukimaliza taratibu chama cha magamba kama tuvoshuhudia. CCM wameshindwa kabisa kuwaletea maendeleo wananchi wa tanzania.
 
Tangu awali CCMimekuwa ikifanyishwakazi na CDM,mfano
-CDM mwaka 1995 walisema gharama za kujenga makao makuu Dodoma ni kubwa, wao CDM wangeufanya mji ule chuo kikuu kikubwa cha fani zote. CCM wamelidaka hilo.
-CDM wamekuja na katiba mpya kwa moto mkubwa. CCM na serikali yake wamelidaka ila linawunguza kweli kweli.
-Ufisadi mkubwa, CCM wanapelekana mahakamani.
-Posho kwa wabunge, CCM wamelishika ila wameshika makali. linawakata vidole vyao.
Na mengine meeeeengi yajayo!
 
Chademaa wangekuwa makini wangezikonga nyoyo za wengi, tatizo lao wanapapara sana na siasa bado hawana mbinu. Wajifunze. Upinzani wanapochochewa na ccm kuwa kazi yao ni kupinga kila kitu wao huona ni kweli kumbe wanaingizwa mkenge. Yale wanayoyaona yametekelezwa kikweli wangekuwa wana appreciate na kutafuta njia za kuchukuwa credit, na pale wanapoona mapungufu wangekuwa wanafanya kwa vitendo vya kuonesha inawezekana na si kupiga kelele tu. Mwisho wanaonekana kuwa ni watu wa kulalamika tu kwa kila kitu. Wawe makini, wanaingizwa mkenge na wanauvaa kichwa kichwa.
 
Mimi wala sijaona CCM walichotekeleza. Siasa za tanzania sasa zimeingia sura nyingine siku hizi, chama fulani kuendelea kujisifu kwamba wao wako madarakani na wakati hamna wanachowatendea watz sasa hivi hiyo haitakubalika tena. Watz wanataka kuona ni nini unafanafanya ili kuwaletea maendeleo. Kuna mambo mengi ambayo ni ya wazi na kama CCM wangeweza kurekebisha haya basi labda wangeirudishia imani tanzania. Haina haja ya kuyataja hapa kwa vile imekuwa kama wimbo siku hizi.

Tupende tusipende CDM imechangia sana mpaka haya tunayoyaona sasa hivi. Tunataka mfumo wa utawala wa serkali ubadilike kwani uliopo ni mzigo mkubwa kwa watz kwanai unatumia gharama kubwa sana kujiendesha.

Back
Top Bottom