Nguo za ndani zinazowalinda wanaume

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,516
2,000


Nguo hizi za
ndani zinasemekana kuwa na uwezo wa kulinda wanaume kutokana na

madini hatari yanayoathiri nguvu za kiume


Kampuni ya Belly Armor, ambayo ilikua ya kwanza kutengeza bidhaa zinazohitajika na wanawake wajawazito, kutokana na kitambaa maalum kinacholinda mwili kutokana na athari za madini ya chuma mwilini, imeanzisha biasharta nyingioenkwa manufaa ya wanaume.


Kampuni hii imeanza kutengeza nguo za ndani za wanaume ambao zinawalinda kutokana na athari ya madini ya chuma yanayoweza kupunguza nguvu za kiume na kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume hali ambayo inaweza kusababisha mwanaume kukosa kuzalisha.
Unaweza kujiuliza je biashara ya kutengeza vitambaa hivyo inanawiri? Jibu? Ndio tena sana.


Mbegu za wanaume zinaweza kuthiriwa na madini yanayotumiwa kutengeza simu za mkononi

Mnamo mwaka 2011, shirika la afya duniani lilitaja madini hayo hatari ikiwemo miale inayotokana na simu za mkononi kama yenye uwezo wa kusababisha saratani ya ubongo mbali na athari nyinginezo hatari kwa mwili kiafya.
Kwa mfano, watumjai wa Iphone, je mlijua kama mnapaswa kuzibeba simu zenu umbali wa milimita 10 kutoka kwa mwili wako kuhakikisha kuwa madini hayo hayaathiri mwili?

Licha ya kwamba utafiti mpya unahitajika kuthibitisha hili....ni wazi kwamba madini fulani yanayotumika kutengeza simu yanaweza kusababisha aina ya saratani za mwilini.
Na ndio maana kampuni ya Belly Armor ikaja na wazo la kuwatengezea wanaume nguo za ndani zinazoweza kuwakinga kutokana na athari hizo.

Pia utafiti ambao umefanywa unaonyesha kua baadhi ya miale inayotokana na vifaa kama vile simu za mkononi, Tabiti au Ipad, inaweza kusababisha mwili wa wanaume kupungukiwa na nguvu za kutengeza mbegu za kime au hata mwili kuishiwa na nguvu za kiume. source.BBC
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,516
2,000
aisee, zitakuwa tofauti na chupi hizi tunazovaa.....?
Zitakuwa ni chupi za aina ya boxer mimi huku nilipo ninazo chupi za Boxer kama mtu atahitaji ninaweza kumletea kwa pesa Mkuu kabanga
Ukihitaji chupi imara kama hizo nitaweza kukuletea lakini bei yake kwa moja ni elfu 10 na idadi yake ni kuanzia chupi 10 na kuendelea ukihitaji nitafute kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano
 

kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
36,999
2,000
Zitakuwa ni chupi za aina ya boxer mimi huku nilipo ninazo chupi za Boxer kama mtu atahitaji ninaweza kumletea kwa pesa Mkuu kabanga
Ukihitaji chupi imara kama hizo nitaweza kukuletea lakini bei yake kwa moja ni elfu 10 na idadi yake ni kuanzia chupi 10 na kuendelea ukihitaji nitafute kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano
ikiwa ni cotton ya ukweli, nitakutafuta....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom