Isaac JK
JF-Expert Member
- Feb 15, 2012
- 563
- 92
VIONGOZI
ngumu kumeza
Kwanza nianze kusema ndani ya chama kuna viongozi hasa baadhi ya viongozi wa juu wa chama wanaokiharibu chama wakiamini kabisa wanakijenga chama. Kiukweli dhamira yao si kukiharibu chama ila maamuzi yao katika shughuli za kichama ndiyo yanachokitia doa chama. Narudia kusema imani yao ya kweli toka moyoni ni kukijenga chama lakini outcome yake ni doa ndani ya chama
mfano 1: Kuna viongozi wapo radhi wavunje sheria za chama ili kukisaidia chama ila mwisho wa siku tunajua sheria tumeziweka ili tuzifate na siyo kuzivunja hata kama ni kwa maslai ya chama la sivyo tutakuwa tunabaka democrasia tunayoiasisi kama chama.Kama sheria ni mbovu haina budi kuibadilisha kwa utaratibu maalum na siyo kuivunja
mfano 2:Kuidhinisha malipo kwa mtu asiyestahili kulipwa hata kama anakisaidia chama ni uvunjaji wa sheria. Kama sheria ilionekana mbovu ni heri ilekebishwe na siyo kuvunjwa na huu ndio utawala wa sheria na ndiyo democrasia makini tunayoiasisi wana chadema
mfano 3:Maamuzi ya kupitisha kauli, malipo au bajeti za chama yafanywe kwa misingi na taratibu za chama na isiwe shinikizo la mtu mmoja. Tusifanya maamuzi ya kumfurahisha mtu mmoja au watu wachache kwa kuhofia uwepo wao ndani ya chama ( chadema ni nguvu ya umma ikibeba dhima ya kusikiliza sauti za wengi ) Tutumie kikao vya chama kupitisha maadhimio kwa misingi ya sheria tulizoziasisi ndani ya chama
WANACHAMA NA WAPENZI WA CHAMA
Wanachama na wapenzi wa chama wajibu wetu namba moja ni kukitetea na kukipigania chama kwa hali na mali huku tukiongeza wigo na kukipanua chama kwa idadi ya wanachama kwani mtaji wa chama ni wanachama. Na hii ndiyo itakayokufanya utimize wajibu ulioainishwa kwenye kadi yako ya chama
ngumu kumeza
kuna wanachama na wapenzi wa chama wapo radhi kukitetea chama kwa hali na mali bila hata kuhoji baadhi ya hoja wanazoulizwa. Kuna baadhi ya mambo ya ukweli kabisa chama kinaonekana kimekosea badala ya kukili tatizo na kujiuliza ni vipi tutalitatua wenyewe ni kutetea tu bila hata ya kukili udhaifu. Ndugu wanachama kukili udhaifu siyo kukubali kushindwa bali ni kujiuliza wapi tumekosea. Tunapokitetea chama tuwe na hoja za msingi na siyo tu kukitetea chama wakati tatizo linaendelea kuwa palepale
mfano1; Huwezi kusema kero zilizotolewa zinafanyiwa kazi wakati wakati miaka inaenda tu hayo siyo majibu ya kutulizisha wanachama tunahitaji utekelezaji uonekane kwa macho juu ya kero zilizotolewa na si maneno
HITIMISHO
Tusiongozwe na fikra za kukitetea tu chama bila kukiambia ukweli tutakuwa tunakiua bila kujua. Umma umetambua kuwa chadema ndiyo chama mkombozi na hivyo basi chadema inatakiwa irudishe fadhira kwa imani iliyopewa na umma. Na mwisho wito wangu kwa wanasiasa wa chadema hasa wabunge wajue kuwa siasa siyo maneno tu bali na vitendo (yaani waegemee kwenye kusema na kutenda )
Kila la heri chadema kwenye ukombozi wa pili na wa kweli wa taifa hili teule lenye utajiri wa rasilimari