Ngumu kuishinda vita inayoendelea mkoani Pwani, Uchunguzi wa chanzo unahitajika

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,846
5,057
Wandugu habari zenu,

Naomba nitoe maoni yangu tena kwa sentesi chache kuwa, Ni ngumu kwa upande wowote kushinda na hatimaye kuimaliza vita au mauaji yanayoendelea mkoani Pwani, Uchunguzi zaidi kubaini chanzo unahitajika na baada ya kubaini chanzo tunaweza kuona ni njia zipi zitumike kulimaliza tatizo hilo.

Bahati mbaya kwa sasa kinachotumika siyo ueledi Wa majeshi yetu Bali tunatumia vitisho, nguvu na maneno kupambana vita hii. Tumeshindwa kujuwa kama wauaji ni majambazi? Vibaka? au magaidi? na kwa nini wanaua? Nini sababu au chanzo? Nani wako nyuma ya hili kwa maana ya wafadhili?

Tumeishia kujidanganya kuwa tukimteua mtu Fulani ni kamanda mkali hivyo tatizo litakwisha. Hapana, Tatizo hili halimalizwi na mtu mmoja ambaye naye anahitaji ulinzi mkali ili kuzuru eneo LA tukio.

Tukumbuke kuwa vita hii amabyo Mimi naiita ugaidi ni tofauti na vita inayopiganwa USO kwa USO ile unaweza kushinda au kushindwa kirahisi maana uwanja Wa mapambano unaujua na unafahamu kuwa Leo tunaenda kupigania ngome Fulani. No tofauti na hii ya kuvizia hii manaweza kuhangaika Nayo miaka na miaka na msiimalize.

Kumbukeni kuwa nchi za magharibi pamoja na technolojia zao lakini bado mauaji ya kuvizia yamezidi kutikisa Sikh hadi Siku, iweje sisi tujinasibu kuwa tukimuweka kiongozi Fulani atayakomesha? si kweli!

Nahitimisha kwa kusema kuwa kijaza askari lukuki Huko pwani hakutasaidia maana tumeshindwa kujua hata chanzo ni nini, wahusika ni akina nani? na kwa nini wanafanya hivo?

Nawasilisha
 
kuna kipindi nawaza hii ni vita ya kisiasa ambayo siku ikibainika ni nani mfadhili wa haya yote basi nchi hii itakua katika hali mbaya sana .ufanyike utafiti wa kina kujua ni nani au kundi lipi la siasa lipo ndani ya haya yote.
 
Haswa hayo ndo yanayotakiwa kufanyika ili tubaini nani wanahusika kufadhili
 
Udhaifu wa polisi na idara nzima ya upelelezi umeonekana.
Badala ya kutafuta chanzo cha mauaji na kupata chain nzima ya wauaji,wameenda kupiga,kutesa na kuua wananchi wasiokua na hatia.
Polisi rudini darasa mkajifunze upya,mmefeli mpaka sasa.
 
Polisi wengi ni 4m4 B failed..... Unadhani wana weredi wa kutosha apo,,, na wenye weredi wakiuonyesha watasema mara ooh polis kawa kinyume na Bi kirembwe....
Uwanja wa mapambano sio sawa na maabara. Hakuna sayansi pale kupima na upate majibu sahihi. Kwenye mapambano hayo ni kujarubu kwa vyovyote kuiona kesho. Kuwa failure au kuwa na IQ kubwa sio kigezo. Na kama hujajua unaepigana nae ana "pigania" mrengo/itikadi/maslahi gani.

Nadhani approach ya kutumia nguvu inaelekea kukatisha tamaa. Wangekaa mezani tu. Hao jamaa wa ikwiriri wasipoangaliwa watatufikisha mbali kama nchi.

Wakitangaza agenda yao wanaweza kupata uungwaji mkono kutoka sehemu tofauti. Wakae mezani, kama kuna ya kurekebisha au kuboresha suluhu ipatikane maisha yaendelee. Huku kuwindana kubaya manake wanatuona...ila sisi hatuwaoni.
 
Polisi wengi ni 4m4 B failed..... Unadhani wana weredi wa kutosha apo,,, na wenye weredi wakiuonyesha watasema mara ooh polis kawa kinyume na Bi kirembwe....
Ukipelekwa kule wewe wa PHD unaweza saidia???
 
Algorithm to Solve The issue in Kibiti

Short term Strategy
1) Involve the Community, Talk to the influential people, The Sheikhs, Madrassa teachers, Imaams, Parents, Bishops, Reverends etc

2) Apologise for any injustices that ever happened there, and promise it wont happen again

3) Infilitrate the area with informers and Intelligence

4) Use Force when necessary but a limited force not an indiscrimate force!

Long term Strategy
1) Provide good Social services to the areas, to attract people from other parts of the country to migrate, and mingle with the locals

2) Provide an Economic Incentive to the areas, Let the Youth work, make money and have a good decent lives, rembember Iddle minds are susceptible to evil deeds.

3) A thorough Study on all Communities to identify Strategies how to deal with different communities as a form of a comprehensive internal security Strategy should be devised, forexample the way The Police has to deal with Wahehe is different from how it should deal with Warangi when the standoff occur, because One Community has a history of warriors and fighters while the other is not to such extent OR take an example when the Security deteriorates the way The Police Force has to deal with the population with majority Muslims Standoff is Different from how it Can deal with the one which appear to have non Muslims Majority, This is because forexample, The Organisational nature of Christians is in Hierarchies, They can easily listen to their head figure such as Arch-Bishop, so for this matter if you deal with these Key Figures it is easy to calm their followers down, But Muslims are different, they have their organisations structure decentralized, you can't talk to only few Muslim leaders to calm their people down, You may forexample find the Local Sheikh in Mkuranga more listened and trusted than The Regional Sheikhs!. So my advice here is that, POLICE should embark on a study of the Tanzania Community make up, Identify the weak communal links, Device a Strategy to deal with each of that, This Strategy will be a Cook book, a guide and a reference how to engage in different operations to restore peace and order!, In this Book all Successful operations ever conducted should be documented for future references within the POLICE FORCE itself!
 
Uwanja wa mapambano sio sawa na maabara. Hakuna sayansi pale kupima na upate majibu sahihi. Kwenye mapambano hayo ni kujarubu kwa vyovyote kuiona kesho. Kuwa failure au kuwa na IQ kubwa sio kigezo. Na kama hujajua unaepigana nae ana "pigania" mrengo/itikadi/maslahi gani.

Nadhani approach ya kutumia nguvu inaelekea kukatisha tamaa. Wangekaa mezani tu. Hao jamaa wa ikwiriri wasipoangaliwa watatufikisha mbali kama nchi.

Wakitangaza agenda yao wanaweza kupata uungwaji mkono kutoka sehemu tofauti. Wakae mezani, kama kuna ya kurekebisha au kuboresha suluhu ipatikane maisha yaendelee. Huku kuwindana kubaya manake wanatuona...ila sisi hatuwaoni.
Watakaaje mezani wakati wauaji hawafahamiki.

Na kama ni kisasi mara nyingi hakizuiwi na mambo ya kukaa mezani. Kwani wauaji inaonekana wanalist kabisa.

Nafahamu Serikali inajua cha kufanya. Polisi waendelee na kazi yao wakitenda haki. Serikali imejipanga vyema ninauhakika.
 
Back
Top Bottom