Ngumi za kulipwa - Mpambano wa marudiano wa Panama kati ya Zapir Zap Rasulov vs Ibrahim Class


Kaka

Kaka

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
738
Likes
283
Points
80
Kaka

Kaka

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
738 283 80
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Class Mgendera yuko chini Ujerumani kwa ajili ya kushiriki pambano la ngumi za kulipwa litakalochezwa kwa raundi nane (8), uzito wa kati (Light Weight, 68Kg) kwa kuwakutanisha tena kijana anayekuja kwa kasi kwenye mchezo wa ngumi za kulipwa Tanzania dhidi ya Zapir Zap Rusolov mzaliwa wa nchini Urusi mwenye makazi yake mjini Berlin, Ujerumani. pambano hilo ambalo limebatizwa jina la “Mpambano wa marudiano wa Panama” baada ya kukutana ulingoni katika jini la Panama mnamo tarehe 15 Aprili, 2016 Ibrahim Class alishinda pambano hilo. Baada ya Rasulov kuomba mchzo wa marudiano, kampuni ya Power of Boxing ya Ujerumani chini ya promota maarufu wa ngumi za kulipwa Mario Pokowietz alihakikisha pambano hilo linafanyika na sasa tunahesabu tu masaa kabla ya mabondia hao kukutana tena katika ukumbi wa Huxleys Neue Welt, Hasenheide 107, 1967 Berlin siku ya jumanne, tarehe 29 Novemba, 2016 ambapo bondia Ibrahim Class ameahidi kuedelea kuandika historia ya kumchapa bondia huyo kwa kumaliza pambano hilo kwa TKO.

upload_2016-11-29_1-59-2-jpeg.440857


Bondia Ibrahim Class a.k.a King Class ambaye yuko chini ya usimamizi wa kampuni ya Joe’s Gym ambayo imejikita, pamoja na mambo mengine, katika kusimamia na kuendeleza vipaji kwa wanamichezo mbalimbali, alisafiri siku ya Ijumaa, tarehe 25 Novemba, 2016 kuelekea nchini Ujerumani akiwa ameambatana pamoja na Mkurugenzi wa Joe’s Gym ndugu Joe Anea. Kabla ya safari hiyo, King Class alikuwa akipata mafunzo toka kwa mwalimu mwenye uzoefu wa hali ya juu katika kufundisha mchezo wa ngumi, mzee Habib Kinyogoli.

Tarehe 28, Novemba 2016 Bondia huyo pamoja na mkurugenzi wa Joe’s Gym walipata fursa ya kukutana balozi wa Tanzania nchini Ujerumani mheshimiwa Phillip Marmo ambaye pamoja na mambo mengine alimsihi Bondia huyo kuhakikisha analinda kipaji chake kwa kufanya mazoezi kwa bidii pamoja na kuwa na nidhamu wakati wote. Pia alimtakia ushindi mnono katika pambano hilo ili kuiwakilisha vyema nchi yetu ya Tanzania katika tasnia ya mchezo wa ngumi za kulipwa duniani. vilevile, alimpongeza Mkurugenzi, mzee Kinyogoli pamoja na watendaji wote wa Joe’s Gym kwa kumsimamia bondia huyo pamoja na dhamira yao ya kuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa pamoja na michezo mingine, hasa kwa wanamichezo vijana na zaidi katika kuhakikisha wanamichezo hao wanafaidika kwa hali zote kutokana na vipaji vyao. Balozi pia alitumia fursa hiyo kuwaomba watanzania waishio Ujerumani pamoja na nchi za jirani kujitokeza kwa wingi katika kushangilia na kumpa hamasa bondi huyo wakati wa mpambano wake na pia kuwakaribisha tena mara baada ya pambano hilo.

upload_2016-11-29_1-59-41-jpeg.440858

Kutoka Kushoto; Joe Anea, Mhesimiwa Phillip Marmo (Balozi) na Bondia Ibrahim Class

Imeandikwa na Victoria Joseph - Mkurugenzi wa Masoko, Joe's Gym
 

Forum statistics

Threads 1,273,086
Members 490,268
Posts 30,470,815