Nguli wa Gitaa Afrika, Diblo Dibala " Machine Gun"

Bakulutu

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
2,556
1,784
diblo.jpg diblo.jpg
Anafahamika kwa jeuri yake na uwezo wake wa kupiga gita ya solo,mwimbaji pia na alikuwa kiongozi wa bendi ya Matchatcha ya kisangani.
Hakika watu kama Kanda Bongoman, Pepe Kale, Franco na Arlus Mabele hawata msahau bila kusahau bendi yangu ileee ya Africa Bella Bella..

Aliweza kuimba na kupiga gitaa kwenye bahadhi ya nyimbo kama Anni Amour,Bana congo,Maria, Elizabeth n.k

Ni bahadhi ya Nguli wa gitaa Afrika na dunia hasa ktk mtindo wa 'sukuous' amboa ulikuwa ndio mtindo unaoshirikisha vioungo vyote vya mwili kucheza, kanzia kiuno (LOKETO) n.k

Amezaliwa mwaka ulionzishwa bendi ya TP OK Jazz..

Reference: African Music Encyclopidia

Unamfahamu vipi Diblo, napenda kujua yuko wapi na anafanya nini..tusaidiane..
 
Hawa jamaa Ufaransa si ndio nyumbani kwao? ila usimsahau Dally Kimoko pia amekimbiza mbaya kwenye solo gitaa.
 
Hawa jamaa Ufaransa si ndio nyumbani kwao? ila usimsahau Dally Kimoko pia amekimbiza mbaya kwenye solo gitaa.

katika zile chat za zamani dally kimoko alikua anabwagwa sana na diblo na mpaka mwenyewe dally kimoko alimkubali diblo.
Huyu jamaa ktk gita ya solo bado hajatokea mpaka leo wa kuvunja rekodi yake
 
katika zile chat za zamani dally kimoko alikua anabwagwa sana na diblo na mpaka mwenyewe dally kimoko alimkubali diblo.
Huyu jamaa ktk gita ya solo bado hajatokea mpaka leo wa kuvunja rekodi yake
Hapana wewe hujui muziki, kila mtu ana radha yake na kama uliwapenda Wenge Musica BCBG basi solo ilikuwa inakung'utwa na Allain Makaba
 
Hapana wewe hujui muziki, kila mtu ana radha yake na kama uliwapenda Wenge Musica BCBG basi solo ilikuwa inakung'utwa na Allain Makaba

Na pia kama uliwapenda Extra basi utamkubali Logaroga...
Nakubaliana na wewe nguli mwenzangu.
Kuna mabalaa aliyafanya Dally Kimoko akiyasikia Diblo basi ni lazima akajipange upya...

Binafsi yangu naweza sema Diblo na Dally wako sawa ila kuna nyimbo moja tu inayoitwa OK Madame ndo inayompa uzaidi kiduuchu Diblo.

Tuendelee...
 
Hiyo naipata sana na nilifanikiwa kununuwa video ya hiyo Albamu enzi za mikanda ya VHS ni balaa tupu hiyo nyimbo Diblo alikomesha ile soloutadhani inapigwa ndani ya maji, na raha zaidi wacheza show aliwachaguwa madada warembo mno, mkuu umenikumbusha wiki nitatafuta DVD yake nijikumbushe.
 
Kuna kipande lile gitaa linawauliza watu kisha watu wanajibu...

Gitaa: tyu tyu tyu tyuuuuu
Watu: yee yee yee
Gitaa: tyu tyu tyu tyu tyuuuu
Watu: yeee yeeeee yeeeeeee
Gita: tyu
Watu: yee
Gita: tyu
Watu: yeee
 
Kuna kipande lile gitaa linawauliza watu kisha watu wanajibu...

Gitaa: tyu tyu tyu tyuuuuu
Watu: yee yee yee
Gitaa: tyu tyu tyu tyu tyuuuu
Watu: yeee yeeeee yeeeeeee
Gita: tyu
Watu: yee
Gita: tyu
Watu: yeee
Gita: Tantinta tintalalaa, tututuntutuntutu tuntuntuntutu.

Wacha kabisa mkuu umenichesha maana nabofya laptop niko kitandani, umenisababisha nicheke mwenyewe mpaka shemeji yako ameaka anaona kama labda nimekolea viroba kumbe umenikumbusha mbali sana.

Watoto wa Mulugo na Kawambwa hawawezi kuchangia thread hapa haelewi A wala B.
 
Aah hicho kizalia cha shukuru kawambwa waambie kubana suruali chini, kulegeza suruali na kubana pua tu...

Mi nakwambia juzi Jumapili pale Sansiro kwa mbele kuna Bar inaitwa Dagaa Dagaa.
Kuna DJ aliporomosha Soukous wallah nilimong'onyoa uno almanusra niangushe mtungi wa shisha...

mdomoni nina taksima, kijasho kinanitiririka kwa raha zangu mwanakwetu dah...
Balaa lilikuja pale alipolipandishia hilo OK Madame...
Kaka acha, kumbe age is just a namba tu, kiuno bado wamo mpaka mwenyewe nilijishangaa...
Maana nilipiga alama ya msalaba kisha nikastua...dah
 
Diblo alikua ni nouma but i dont ignore kwamba dalo kimoko nae ni moto wa kuotea mbali ukisikiliza nyimbo ya madilu inaitwa simon hahahaha utaamin kua dalikimoko nae ni nouma,kwa sasa mkali wa soloni jamaa mmoja anaitea flame kapaya alikua mpiga solo wa werrason anayetaka thobitsha hili go youtube akifatiwa na kimbangu solo
 
haaa..haaaa..kweli mkuu hata mm nimecheka saaaana...kuna hii kitu ya DANDY ya Victoria Eleyson na Samba Mapangala SIKIZA HIYO GITAA ILIO CHARAZWA NA DIBLO..ni balaaaaa....wabongo huu wimbo wanauita KETEKUNE..
 
Kuna wimbo unaitwa Shalai wa Extra Musica, kazi aliyoifanya Loga loga kidogo inifelishe mtihani mwaka 98, maana kila wimbo huo ulipokuwa ukipigwa siwezi kusoma kwa utulivu hadi uishe ndo niconcentrate, haya mabongofleva yametuondelea fleva za kiafrika aisee.
 
sinasssss..basese...gita inalia..nd'uuuuu..n.duuuuuu..

OK MADAEME....

Last edited by a moderator:
pia mkuu kuna PARDON ya Madilu...bonge la Rhumba na Ringtone yangu..

Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom