NGOs zatakiwa kuweka wazi malengo ya pesa wanazopota kutoka kwa wafadhili

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs, Denis Bashanga amesema kuwa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanatakiwa kuweka wazi pesa wanazopata kutoka kwa wafadhili na kubainisha zinakuja kwa lengo gani na zinapotokea.

Akizungumza leo Machi 13, 2023 katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kwa kushirikiana na Taasisi ya Haki za Binadamu Afrika Mashariki (EAHRI) na Taasisi ya Defenders Protection Initiative (DPI), kutoka nchini Uganda, ambayo yamekutanisha NGOs amesema 2018 Serikali ilitoa kanuni Na. 609 inayosimamia masuala ya uwazi na uwajibikaji ili kuhakikisha mashirika hayo hayajiingizi katika vitendo vya utakatishaju fedha na kufadhili ugaidi.

"Kanuni hizi zinalenga kuhakikisha NGO's na asasi za kiraia zinafanya kazi kwa kuzingatia malengo ambayo nchi inayakubali lakini ambayo yatakuwa siyo kinyume Cha sheria. Mashirika yanatakiwa yaweke wazi fedha wanazopata zinakuja kufanya kitu Gani na zinatoka wapi," amesema Wakili Bashanga.

Sanjali na hayo Wakili Bashanga amesema hadi Sasa hakuna NGO's au asasi zilizobainika na makosa ya utakatishaji fedha au kufadhili vitendo vya ugaidi.

Akizungumzia mafunzo hayo, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amesema mafunzo hayo yatasaidia NGO's hizo kutojihusisha na masuala yanayochochea makosa ya aina hiyo ambayo yako kinyume cha Sheria.

"Asasi 40 zimekuja kujifunza madhara yanayozikuta asasi wanapoingia kwenye mtego wa kusafisha fedha chafu. Wakati mwingine imetokea zipo taasisi zinashiriki bila kujua au kwa kujua kutakatisha fedha kama za dawa za kulevya na rushwa," amesema Mratibu THRDC Kitaifa, Wakili Olengurumwa

Ameongeza kuwa "Tuna mkakati kuhakikisha tunapambana na utakatishaji fedha na kufadhili ugaidi, hivyo asasi tunaopata fedha ndani na nje ni vizuri kujua zinatoka wapi sababu Kuna vyanzo vichafu."

Mafunzo hayo imeelezwa kuwa yamelenga kuzifahamisha Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya kiserikali nini maana ya utakatishaji fedha, njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika kutakatisha fedha kupitia Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya kiserikali na fedha ambazo zinapatikana na kutumika kufadhili ugaidi, na jinsi gani utakatishaji fedha unatokea .

Malengo mengine yaliyobainishwa na waandaaji ni jinsi gani Serikali kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya kisirikali zinaweza kutokomeza kabisa utakatishaji fedha nchini Tanzania na ufadhili wa mipango ya kigaidi, Kuzijengea uwezo asasi za kiraia jinsi ya kuepukana na fedha na mali zilizopatikana kwa njia haramu na zenye lengo la kufanyiwa utakatishaji au kufadhili ugaidi.

Sambamba na hayo malengo mengine ambayo yamebainishwa ni kuwajengea uwezo AZAKI/Watetezi wa haki za binadamu juu ya sera, sheria na mikakati inayoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Tanzania ili kupambana na utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi hasa kwa upande wa mashirika yanayofanya kazi bila faida (NPOs/AZAKI). Kuhakikisha mikakati hii mizuri ya kupambana na utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi haitumiki vibaya kwa malengo yasiyo rasmi kudidimiza nafasi za kiraia nchini ( Civic Space).
 
Monitoring and evaluation zinakua ndani ya organization hakuna haja ya serikali kujua
 
Back
Top Bottom