Ngono/mapenzi kabla ya Ndoa: Faida na Madhara yake...

Ngono/mapenzi kabla ya Ndoa: Faida na Madhara yake...

Mwanapropaganda

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
4,235
Reaction score
2,512
Mara kwa mara nikuwa nikisikia kuwa ngono hizi zinazofanywa kabla ya ndoa ndio zinachangia kufanya ndoa nyingi zisidumu.

Nimewahi kusikia hivyo kwenye semina za vijana miaka ya nyuma kidogo ambapo vijana walihimizwa kuhakikisha wanatunza miili yao hadi pale watakapounganishwa na ndoa na kuwa mme na mke halali.

Jana tena nikiwa nasoma kitabu fulani cha kiingereza kinachozungumzia masuala ya maisha ya ndoa, nimeona msisitizo kama huo nikajisemea kuwa hapa kuna namna ambayo huenda vijana wa sasa hawaelewi.

Ni kwamba inasemwa kuwa tendo la ndoa linalofanywa na wahusika siku ya kwanza linakuwa na msisimko wa aina yake kuliko tendo lolote litakalofuata, ndio maana inasemwa kuwa si rahisi mwanamke kumsahau mwanaume aliyefanya naye mapenzi siku ya kwanza.

Kama hivyo ndivyo wewe kama mwanaume au mwanamke unategemea mwenzako akuone wa pekee kuliko yule aliyekutana naye kimwili mara ya kwanza? Kama sivyo basi kila mmoja anawajibika kwa usaliti wake kwa mwenzake ambaye pengine kwa sasa bado hujamfamu, je unapolilia kusalitiwa umejiuliza uliwahi kusaliti mara ngapi?

Kama tunaamini kuwa kila mtu aliwekewa mtu wake tangu alipozaliwa basi kwa vyovyote vile ufanyavyo kabla ya kuoa/kuolewa unakuwa ni msaliti kwa huyo mtu ambaye pengine kwa sasa bado hujamfahamu, au ikiwa umeoa/kuolewa lakini uliwahi kujihusisha na ngono na me/ke mwingine na wewe pia ni msaliti hivyo huna haki ya kulalamika pale msaliti mwenzako anapokufanyia usaliti.
 
Watanzania wenzangu.
1. Imani yako ndio itakayo kuponya
2. Apandacho mtu ndicho avunacho.
3. Mungu hadhihakiwi
4. Mungu humpa mtu wa kufanana nae (Hili nalisemaga mara nyingi)
Mtoa mada anaongelea swala muhimu sana ambalo misingi yake ni kutoka katika kitabu cha Mungu ila cha kushangaza ataonekana mshamba na hovyo. Kupenda kuonja kabla ni kuingia maagano na roho usizo zijua zitakazo kusumbua baadae katika maisha yako ya ndoa ...linalopelekea vimizizi vya michepuko kuota na kukomaa. Utapinga lakini ukweli ndio huo na wewe mwenyewe ni shahidi wa maisha yako.
 
Zinaa haiwezi kuepukika kwa kizazi chetu sababu:

>Mtu anabalehe akiwa 13/15 lakini kulingana na maisha kubadilika kijana anatakiwa kutafua maisha(shule)anakuja kuoa/kuolewa akiwa na 30.

>kumbuka urijali mwaname anazaliwa nao sio baada ya kuo,kwa maana hiyo kijana atahitaji tendo la ndoa tangu kubalehe

>Tangu akiwa na miaka 15_30 ukiacha masturbation kijana atatumia sehemu zake kukojoa tu eeeh?

>Mnao kua mnapiga kelele vijana kuacha zinaa bila kuwa shauri funge ndoa mapema inamana mnataka vijana wafanye masturbation sio?

>Maisha ya saivi kijana kuoa/kuolewa akiwa na miaka 18 ni ngumu wanakua bado hawaja simama kiuchumi kitu ambacho ni muhimu sana kwenye ndoa.

Mwisho zinaa itapungua kiasi chake kama watu wata funga ndoa mapema kitu ambacho ni kigumu sana!

Hua siwaelewi hawa watu wanao Pinga zinaa kwa vijana(wasio kua na ndoa) na wanaendelea kutukumbusha Masturbation ni mbaya!
 
Habari za leo members,

Naamini wote ni wazima wa afya. Bila kupote muda niende kwenye maada.

Wakuu nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sana kuhusu hii sheria ya dini ya kutokufanya mapenzi kabla ya ndoa. Hii sheria mimi siamini kama iliwekwa na Mungu. Nina sababu za msingi za kusema hivo.

Kwanza kabisa binadamu tumeumbwa na maumbile tofauti tofauti. Kuna warefu na wafupi, kuna wanene na wembamba. Hizi tofauti zipo katika maumbile yetu yote wanawake kwa waume,kuanzia muonekano wa nje mpaka viungo vya ndani. Na hili inajulikana kwa kila mmoja wetu.

Swali linakuja, nitamjuaje saizi yangu ikiwa nakatazwa kufanya mapenzi kabla ya ndoa? Maana naweza kuoa mwanamke ambae kimaumbile hatuendani matokeo yake ndoa haitadumu.

Kwa ndugu zetu wakiristo kuna sheria ya kuzuia kuoa mwanamke zaidi ya mmoja. Swali. Nitamjuaje saizi yangu ili nioe mmoja nakuridhika.

Swali lingine hivi kwanini Mungu aliumba kubwa na ndogo?
Mtazamo wangu; Mungu aliumba kubwa na ndogo ili kila mtu ajaribu mpaka apate saizi yake

Angekuwa anataka tusijaribu angeweka namba ili kila mtu achague saizi yake

Wakuu mnaruhusiwa kutoa mawazo yenu endeleeni kutiririka hapo chini
 
Shake well b4 use ndo zinaponza wanawake.Ukitaka ndoa,mwambie huuoni mwili wangu hadi uje home kujitambulisha&kutoa mahari.si umemnyima,na anakupenda lazima atakuja.Vua kabla,jamaa anapiga akimaliza anasema maharage ya mbeya hayo ndo kwa heri,anatafuta mwingine!
 
Mungu mwenyewe ndio amesema tusubiri mpaka ndoa,wadhani kwa kupinga neno lake ndio tutakuwa na furaha katika ndoa?! If you want positive life,start being positive and without faith we will just be filling gaps in this life but not living exactly!
 
Mungu mwenyewe ndio amesema tusubiri mpaka ndoa,wadhani kwa kupinga neno lake ndio tutakuwa na furaha katika ndoa?[/color[! If you want positive life,start being positive and without faith we will just be filling gaps in this life but not living exactly!


Hapo kwenye bluu ndipo watu wanapopuuza na ndio maana kila siku wanatafuta mchawi anayeharibu furaha ya ndoa zao ila hawaoni, kumbe ni kwa sababu wameasi kanuni.
 
Siyo kwa zama hizi mkuu
Watu wanataka MABADILIKO

Kama niabadiliko maana yake ni kwamba, hata wewe(mwanaume) ukiolewa ni mabadiliko hata kama utakuwa unaasi kanuni za awali. Je uko tayari kwa hayo mabadiliko? Au unataka kusema kuwa wale wote waliokuwa wanatunza miili yao walikuwa wajinga na washamba?
 
Umesema ukweli kabisa!!

*Kuna father alichukua karatasi ya rimu akadondoshea wino mweus kidogo then akawauliza, mnaona nini hapa kwenye karatasi hii? Watu wote wakajibu "doa jeusi" na ile karatasi na ukubwa wote hawakutambua ama kuiona kwa haraka badala ya kujibu kuwa ni "karatasi nyeupe" ndio ionekanayo na matokeo yake wameona kitu ambacho kidogo na kimejificha sana! i mean binadamu tumevaa macho ya kuona vitu negative na vya postive havionekani wala kukubaliwa ndivo ivoivo na mleta mada hapa ataonekana ovyo sana lakin uchungu na ukweli mnao ndani ya maisha yenu, ushahidi nyuz nying humu ni za kulalamika sa sijui mpingacho ni nini?.
 
Ili ndoa iwe imara, lazima nyote muwe mmeridhika na kila mmoja kwa kila sector. Sasa mkisubiri, halafu mkakuta faragha hamuendani kabisa na mmeshaingia kwenye ndoa, si ndio migogoro inapoanzia?

Ukifuata taratibu, Mungu atakupa anayekustahili. Wengi wetu tunakurupuka bila kumtegemea Mungu ndio maana tunashndwa mbeleni.
Mtegemee Mungu. Uzinzi ni dhambi wapendwa.
 
Mungu mwenyewe ndio amesema tusubiri mpaka ndoa,wadhani kwa kupinga neno lake ndio tutakuwa na furaha katika ndoa?! If you want positive life,start being positive and without faith we will just be filling gaps in this life but not living exactly!

God bless you
 
Ili ndoa iwe imara, lazima nyote muwe mmeridhika na kila mmoja kwa kila sector. Sasa mkisubiri, halafu mkakuta faragha hamuendani kabisa na mmeshaingia kwenye ndoa, si ndio migogoro inapoanzia?

Mkiendana mwanzoni halafu baada ya kuzaa msiendane itakuwaje?
Je wenye maumbile madogo au makubwa hawapaswi kuoa/kuolewa? Utaonja wangapi hadi ufikie size yako?
Mpango wa Mungu siku zote ni sahihi, mengine yote ni kujitafutia tu vijisababu vya uzinzi.
 
Back
Top Bottom