Ng'ombe wa masikini hazai, AU tujaribu fikra Ngumu?

Mchuja Nafaka G

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
763
253
Rafiki yangu tumekutana wilaya moja nchini takribani miaka 10 iliyopita tupo pamoja, miaka ya mwanzoni ya urafiki wetu alikuwa kisu kwa wanawake, sasa ni takribani miaka miwili amekuwa mpole na aliweka lengo lake wazi kutaka kuoa baada ya ushauri mwingi sana kutoka kwa marafiki mbalimbali ikizingatiwa wengi tuliokutana naye tukiwa single tayari tuna familia. Hivyo anakuwa mpweke mana mitoko ya usiku, na vile tulikuwa tunalianzisha muda wowote uhuru huo wengine tumepokwa na familia.

Sasa mwanamke aliyemwangukia kwa lengo jema ameajiriwa ofisi moja hapa wilayani miaka miwili na miezi kadhaa iliyopita sasa, tangu awe na huyo dada mshkaj ametulia hadi wengi hawaamini isipokuwa kumuheshimu shemeji yetu na kumpa heshima yake tunakutana kirafiki yani freshi.
Shida huyu amefika huku tayari akiwa ktk mahusiano na mwanaume mwingine alikotoka. Pamoja na hayo wapo pamoja kwenye mahusiano zaidi ya mwaka au labda imefika miwili kutembeleana kila mmoja anaishi kwake.

Wakiwa miezi kadhaa ya mahusiano demu alirudi kwao likizo kwa ajili ya zoezi la utambulisho na kulipiwa mahari na huyo kidume wa kwao, hakuna siri sisi tumejua na rafiki yetu akijua tena kabla yetu. Mbaya zaidi pamoja anajua yote hayo lakini amekufa kwa kigori huyo na kawa mtulivu isivyo kawaida yake, kwa hilo la kutulia tunashukuru.

Hofu yetu kama atashindwa kubadili matokeo mchezo unaisha demu anaolewa na jamaa anayefahamika kwao hatimaye kuondoka wilayani kwetu kumfuata kidume wake jamaa yetu atarudi kwa awali?
Tumedata na kuishiwa nguvu sababu hatua ya kumsaidia aache kuwabadili imetiki tatizo hapo alipoangukia. Ng'ombe wa masikini hazai au tujaribu fikra ngumu?
 
Malipo ni hapahapa.... Usikute ni machozi ya aliowaacha bila sababu....

Ila wanawake ni wengi sana atapata tu asikurupuke kisa ninyi mmeoa so anakua bored atulie atampata tu
 
Back
Top Bottom