Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Hata hivyo alitaja uzembe wa usimamizi wa sheria kuwa ndiyo uliolifikisha Taifa hapo kwa kuwa sheria zilizopo ni mzuri, lakini hazisimamiwi ipasavyo.
"Kuhusu kuhojiwa au kuwajibika sina neno la kusema lakini nampongeza sana kwa moyo wa dhati Muheshimiwa Rais maana amezungumza kwa hisia na uzalendo kabisa kuhusu tunachostahiki kupata badala ya tunachopata ", alisema Ngeleja ambaye pia ni mbunge wa Sengerema.
Hata hivyo alikiri mikataba mingi iliyopitishwa siyo mizuri kwa kuwa inawanyonya Watanzania ambao wameshindwa kupitia sheria mpya (ya madini ya mwaka 2010)
kuifanyia kazi.
" Kifungu cha 11 pia kinachosema mikataba yote ipelekwe bungeni baada ya miaka ya mitano na kifungu cha 10 kinasema Serikali ishiriki kimkakati kwenye migodi, lakini usimamizi wake ni shida", alisema Ngeleja
Kuhusu mchanga kusafilishwa nje ya nchi, alisema walishaliona jambo hilo mapema lakini wakabainisha kuwa mashine za kufanya kazi hiyo zina gharama kubwa duniani zaidi hivyo kuhitaji ubia katika ujenzi baina ya Serikali na sekta binafsi.
Chanzo: Mwananchi