Ngeleja:Tatizo la umeme ni la Serikali nzima

Ms Judith

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
2,563
918
Tuesday, 19 July 2011

Neville Meena, Dodoma

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amesema kwamba hawezi kujiuzulu kwa tatizo la bajeti yake kukwama bungeni akisema tatizo la umeme si lake peke yake, bali Serikali nzima. Ngeleja alisema jana mara baada ya kuahirishwa kwa Bunge juzi jioni kwamba: "Hilo sidhani kama ni muhimu. Muhimu hapa ni kutekeleza maagizo na ushauri wa wabunge kwa Serikali. Wabunge wamesema wanataka umeme na jinsi Serikali inavyoweza kuja na mpango wa dharura wa kuondokana na giza." Alipoelezwa kuwa miongoni mwa mapendekezo ya wabunge ni kumtaka ajiuzulu ili kupisha watu wengine wenye uwezo wa kuongoza wizara hiyo, alisema hilo kwa sasa siyo kipaumbele na kwamba kujiuzulu kwake hakuwezi kusaidia kuondoa tatizo lililopo.

"Tunakwenda kujipanga upya na baada ya wiki tatu tutarudi na majibu mazuri kwani tatizo ni fedha kidogo ambazo zilitengwa kwa ajili ya wizara yangu, sasa si mmemsikia Waziri Mkuu, (Mizengo Pinda) ameshasema nyie tupeni nafasi tunakwenda kutekeleza hayo," alisema Ngeleja na kuongeza:

"Bajeti ni ya Serikali si ya wizara ya nishati pekee, hivyo mimi si kwamba ndiye niliyetenga fedha hizo zinazosemwa kwamba hazitoshelezi, lakini hayo si muhimu kwa sasa, muhimu ni kwamba tumepewa fursa nyingine tunakwenda kukaa ili kuona jinsi tunavyoweza kutoka hapa." Shinikizo la kumtaka Ngeleja aachie ngazi lilitokana na kikao cha wabunge wa CCM ambao walikutana juzi mchana na kudai kwamba waziri huyo amewatia aibu kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake kiasi cha kuilazimisha Serikali kuondoa bajeti yake bungeni.

Juzi, Pinda aliondoa hoja ya Waziri wa Nishati na Madini Bungeni akisema hatua hiyo inatokana na hoja nzito zilizotolewa na wabunge wakitaka Serikali kuwasilisha bungeni mpango unaotekelezeka wa kuliondoa taifa gizani kutokana na mgawo wa umeme unaondelea.

Mkulo atema cheche Akizungumzia suala hilo la kujipanga upya na kuja na bajeti bora zaidi itakayokuwa na majibu juu ya tatizo la nishati, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema jana kwamba: "Waziri Mkuu hakusema kwamba tutaongeza bajeti kwa ajili ya kupatikana kwa umeme, bali alisema tutatafuta njia za kuondokana na tatizo la umeme nchini. Njia za kutatua mgawo wa umeme uliopo ni nyingi siyo lazima uongeze fedha za uwekezaji mpya."

Mkulo alisema anaishangaa Wizara ya Nishati na Madini kwa kushindwa kuweka katika bajeti yao njia zisizohitaji fedha za umma kuwekeza ambazo zinaruhusu uwekezaji wa sekta binafsi katika sekta hiyo. "Tulipitisha hapa bungeni Sheria ya PPP, yaani Public Private Patnership (Ushirikiano wa Sekta za Umma na Binafsi), hii inaruhusu sekta binafsi kuwekeza katika miradi ya umeme," alisema Mkulo na kuongeza:

"Ngoja nikwambie, mimi nilikuwa China siku chache zilizopita, pale kuna makampuni manne yako tayari kuja Tanzania kuwekeza bila hata Serikali kutoa senti tano halafu wauze umeme wao Tanesco, sasa hapo si lazima Serikali itoe fedha za mtaji". Mkulo alisema uwekezaji wa Serikali katika uzalishaji wa umeme unaongeza mzigo kwa watumiaji wa nishati hiyo na kwamba ingekuwa vyema Wizara ya Nishati ikatumia mfumo wa kuruhusu wawekezaji ambao wanakuja na mitaji yao. "Tukitumia njia hii, suala la umeme tunaweza kuondokana nalo katika muda mfupi tu usiozidi miezi minne,"alisema
Mkulo.

Mgogoro wa Kanuni
Kuondolewa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kunaashiria mgogoro wa kikanuni baada ya Kamati ya Uongozi ya Bunge iliyokutana juzi jioni chini ya Uenyekiti wa Spika wa Bunge, Anne Makinda kushindwa kukubaliana jinsi ambavyo hoja hiyo itarejeshwa bungeni baada ya kuondolewa chini ya Kanuni ya 69 (1) na 69(2). Kwa mujibu wa marekebisho ya tatu ya ratiba ya Bunge la Bajeti yaliyofanywa juzi jioni na ratiba mpya kutolewa jana, hoja ya Wizara ya Nishati na Madini iliyoondolewa juzi, sasa itajadiliwa Jumamosi, Agosti 13, 2011.

Habari kutoka katika kikao hicho kilichofanyika mara tu baada ya Bunge kuahirishwa juzi jioni, suala la jinsi ya kuwasilisha upya hoja hiyo liliibuliwa na baadhi ya wajumbe na kwamba Spika alisema hoja hiyo itaanza kwa mawaziri husika kuwasilisha maelezo ya mpango wa dharura wa kukabiliana na uhaba wa umeme. Kwa mujibu wa taarifa hizo, baada ya waziri kuwasilisha mpango huo, ataendelea kujibu baadhi ya hoja za wabunge na baadaye Bunge litakaa kama kamati ili kupitisha bajeti hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya wajumbe waliozungumza kwa masharti ya kutotajwa majina walitofautina na msimamo huo wa Spika. "Spika alisema hivyo ingawa mimi sikubaliani naye, hapa kuna mgogoro wa kikanuni kwani kanuni hazisemi kitu jinsi ya kurejeshwa kwa hoja iliyoondolewa bungeni," alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Uongozi.

Spika Makinda hakupatikana jana kutoa ufafanuzi wa suala hilo kwani alikwenda Kongwa kuhudhuria mazishi ya bibi mlezi wa Naibu Spika, Job Ndugai. Kutokana na utata huo wa kikanuni hueda Spika akafuata utaratibu uliotumiwa na mtangulizi wake, Samuel Sitta, Julai 2009 wakati Serikali ilipolazimika kuondoa bungeni Bajeti ya Wizara ya Miundombinu wakati huo baada ya wabunge kuikataa.

Mgogoro wa 2009 Julai 2, 2009 aliyekuwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Phillip Marmo alilazimika kuondoa bungeni hoja ya Wizara ya Miundombinu baada ya aliyekuwa Mbunge wa Ilemela, Anthony Diallo kuwasilisha mapendekezo ya kufanya marekebisho makubwa. Waziri wa Miundombinu wakati huo, Dk Shukuru Kawambwa alikuwa amewasilisha makadirio ya matumizi ya wizara yake lakini wabunge wakiongozwa na Diallo waliikataa wakidai kwamba rafu ilikuwa imechezwa katika mgawo wa fedha za ujenzi wa barabara nchini.

Kama ilivyokuwa katika Wizara ya Nishati na Madini juzi, wabunge wengi hawakuunga mkono hotuba ya Dk Kawambwa na kushinikiza yafanyike mabadiliko makubwa ambayo yaliifanya Serikali kuondoa hoja yake na kwenda kujipanga upya.

Hoja ya Diallo ilikuwa ikisababisha kuwepo kwa mabadiliko ya matumizi ya kiasi kikubwa cha fedha, hivyo Spika Sitta aliielekeza Serikali kukutana na Kamati ya Miundombinu ambayo wakati huo ilikuwa chini ya Mohamed Missanga ili kufikia mwafaka. Bajeti hiyo ilipitishwa Julai 4, 2009 siku ya Jumamosi na ikipata wakati mgumu kutokana na maoni mengi yaliyoibuliwa na wabunge wakati Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi, chini ya Mwenyekiti Sitta.

Kabla ya Bunge kukaa kama Kamati ya Matumizi, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Missanga, alisoma taarifa ya kamati yake kuhusu hoja ya Diallo ya kufanya mabadiliko katika matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2009/10.

Katika mchakato huo, Diallo alipewa nafasi ya kutosha mbele ya Kamati na baadaye Waziri Kawambwa kutoa maelezo ambayo yaliwezesha Bunge na Serikali kukubaliana jinsi ya kutatua mgogoro uliokuwepo wakati huo. Kutokana na uzoefu huo, upo uwezekano mkubwa kwa Spika Makinda kuamua kuipa nafasi Kamati ya Bunge ili itoe maoni kuhusu mpango mpya wa Serikali katika kukabiliana na tatizo la umeme kabla ya Bunge kukaa kama kamati na kupitia bajeti hiyo kwa vifungu.

Kadhalika, upungufu wa kanuni unaojiokeza sasa unaashiria kuwapo kwa umuhimu wa kanuni hizo kupitiwa upya, ili kukidhi matakwa ya kimatukio yanayojitokeza sasa hivyo kumpa nafasi kubwa Spika kuamua jambo "kadri anavyoona inafaa".

SOURCE: Ngeleja:Tatizo la umeme ni la Serikali nzima
 
amekuwa wizarani kwa miaka zaidi ya 4, mnaomtetea leteni mikakati chanya aliyoifanya na serikali ikagoma kumsikiliza. na kama serikali haikumsikiliza alichukua uamuzi gani kama mkuu wa Wizara hii nyeti?

Lawama hizi hatazikwepa na sisi tunajua jamaa ni ka-mzigo hakabebeki, awaachie wengine wapige kazi.

hapo kwenye bold, ni kina nani hao?
 
Mpuuzi Ngereja go out, Mjinga wewe unadhani hiyo ofisi ni shamba la bibi yako, Hatukutaki unasubiri nini? Pinda fukuza huyo kibaraka wa Rostum
 
Mwingine huyu hapa: nafikiri nimekupa ushahidi wangu haya changanya na za kwako.

By Nyani Ngabu Watu tuna kumbukumbu fupi sana na ukweli huu umejidhihirisha hivi sasa kwenye haya matatizo ya umeme. Waziri Ngeleja anaoneka ndiye kama vile amesababisha matatizo yote haya wakati ukweli wa mambo umeme wa uhakika umekuwa tatizo sugu Tanzania.

Sasa iweje Ngeleja leo abebeshwe msalaba wa lawama na shutuma wakati mawaziri wa nishati na serikali zilizopita zimemrithisha tatizo? Hiyo si haki hata kidogo. Jaribuni tu kurudi nyuma miaka 20 iliyopita muone ni kina nani waliweza kupata fursa ya kuongoza wizara hiyo na walifanya nini kuhakikisha tatizo linakuwa historia.
 
Mpuuzi Ngereja go out, Mjinga wewe unadhani hiyo ofisi ni shamba la bibi yako, Hatukutaki unasubiri nini? Pinda fukuza huyo kibaraka wa Rostum

Pinda hana uwezo wa kumfukuza yeye wala Jairo, anachoweza kufanya ni kumshauri Rais tu. Cha msingi bunge liamue kupiga kura za kutokuwa na imani na Ngeleja, if YES then huo ndiyo itakuwa mwisho wake. 'cause hata JK nawezi kumfukuza ni mawahiba hawa.
 
Ngeleja yuko sahihi kabisa tena kwa asilimia 800!

Mkitaka yeye ajiuzulu basi hamna budi kumtaka raisi naye ajiuzulu maana yeye pia aliwahi kuwa naibu waziri na waziri wa wizara hiyo hiyo na hakuja na mikakati yoyote ile ya kuhakikisha matatizo ya umeme yanakuwa 'a thing of the past'. Halafu bado mkampa uraisi mtu huyo huyo ambaye wizara ilimshinda kuwa raisi wenu. Huo kama si upumbavu ni nini?
 
Hakuna kitu kama hicho, "Two Wrongs dont make a Right".... kama huyo mwenzake kipindi chake aliweza kupona fagio la Chuma does not mean na huyu mwingine nae apone...

Alafu hebu nikumbushe hali ya mgao wa giza wa kipindi kile na kipindi hiki kama ni sawa, na kama katibu wake pia alikumbwa na kashfa ya kuwaonga wabunge????

Ule msemo wa Mshikwa na Ngozi ndio Mwizi hapa ndio mahala pake
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Na mawaziri wote wale ambao walimtangulia Ngeleja, kama baadhi wapo serikalini basi nao lazima wajiuzulu nyadhifa zao maana hata wao hawawezi kazi. Hatuwezi tukawa tuna recycle watu wasio na uwezo wa kuongoza halafu tutegemee mabadiliko.
 
Nahisi wizara nyiiing huwahonga WABUNGE,KAMA KUSIMGEKUWA NA MGAO,WANGEHONGWA NA TUSINGEJUA
 
Hakuna kitu kama hicho, "Two Wrongs dont make a Right".... kama huyo mwenzake kipindi chake aliweza kupona fagio la Chuma does not mean na huyu mwingine nae apone..

Sawa, alipona...lakini huoni kama mfupa alionao sasa ni mkubwa kuliko ule wa wizara? Au wewe unaridhika na utendaji wake kama raisi wa jamhuri? Mtu anayeishindwa wizara nchi ataiwezaje? Tumia akili yako ya kuzaliwa.

Alafu hebu nikumbushe hali ya mgao wa giza wa kipindi kile na kipindi hiki kama ni sawa, na kama katibu wake pia alikumbwa na kashfa ya kuwaonga wabunge????

Mgao kwangu ni mgao tu. Kama wewe uliridhika na mgao wa kipindi kile huyo ni wewe. Mimi siridhiki na mgao wa aina yoyote ile. Halafu Ngeleja hata akijiuzulu huu mgao hautaisha endapo tutaendelea kutegemea mvua kujaza hayo mabwawa ya kuzalishia umeme. Lakini nyinyi mmeng'ang'ania Ngeleja Ngeleja....

Stop seeing the forest for the trees. Ngeleja can be gone today but the problem will persist. You can quote me on that.
 
Na mawaziri wote wale ambao walimtangulia Ngeleja, kama baadhi wapo serikalini basi nao lazima wajiuzulu nyadhifa zao maana hata wao hawawezi kazi. Hatuwezi tukawa tuna recycle watu wasio na uwezo wa kuongoza halafu tutegemee mabadiliko.
We have to start from somewhere.., and Ngeleja is as good a start as anyone..
Nobody is saying the previous people did a wonderful Job.., and because the cracks are now showing now more than ever, we need to set an example that these jobs must be result oriented..., and not politicization of the issue...

Hivi huyu jamaa alitwambie ni lini mgao utakuwa Historia????. , Kwa mimi kufata kauli yake kama waziri nikatumie funds zangu kwemye shughuli nyingine badala ya kununua Generator!!!, This man has cost me and is costing me a lot.... (and am afraid am not the only one)
 
Sawa, alipona...lakini huoni kama mfupa alionao sasa ni mkubwa kuliko ule wa wizara? Au wewe unaridhika na utendaji wake kama raisi wa jamhuri? Mtu anayeishindwa wizara nchi ataiwezaje? Tumia akili yako ya kuzaliwa.

Mgao kwangu ni mgao tu. Kama wewe uliridhika na mgao wa kipindi kile huyo ni wewe. Mimi siridhiki na mgao wa aina yoyote ile. Halafu Ngeleja hata akijiuzulu huu mgao hautaisha endapo tutaendelea kutegemea mvua kujaza hayo mabwawa ya kuzalishia umeme. Lakini nyinyi mmeng'ang'ania Ngeleja Ngeleja....

Stop seeing the forest for the trees. Ngeleja can be gone today but the problem will persist. You can quote me on that.

Mkuu you are missing my point The Government is full of useless people.., na tunamuongelea one at a time..., Kafungue Thread ya kuwawajibisha Mawaziri wote na Boss wao uone kama sitamwaga nondo ninazomwaga hapa...., A lot of people need to go... Including this Man (Ngeleja). Sometimes sababu hakuna mtu anaechukua responsibility thats why hawa watu wanafanya hizi kazi kama miradi ya familia
 
Tuesday, 19 July 2011

Neville Meena, Dodoma

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amesema kwamba hawezi kujiuzulu kwa tatizo la bajeti yake kukwama bungeni akisema tatizo la umeme si lake peke yake, bali Serikali nzima. Ngeleja alisema jana mara baada ya kuahirishwa kwa Bunge juzi jioni kwamba: "Hilo sidhani kama ni muhimu. Muhimu hapa ni kutekeleza maagizo na ushauri wa wabunge kwa Serikali. Wabunge wamesema wanataka umeme na jinsi Serikali inavyoweza kuja na mpango wa dharura wa kuondokana na giza." Alipoelezwa kuwa miongoni mwa mapendekezo ya wabunge ni kumtaka ajiuzulu ili kupisha watu wengine wenye uwezo wa kuongoza wizara hiyo, alisema hilo kwa sasa siyo kipaumbele na kwamba kujiuzulu kwake hakuwezi kusaidia kuondoa tatizo lililopo.

"Tunakwenda kujipanga upya na baada ya wiki tatu tutarudi na majibu mazuri kwani tatizo ni fedha kidogo ambazo zilitengwa kwa ajili ya wizara yangu, sasa si mmemsikia Waziri Mkuu, (Mizengo Pinda) ameshasema nyie tupeni nafasi tunakwenda kutekeleza hayo," alisema Ngeleja na kuongeza:

"Bajeti ni ya Serikali si ya wizara ya nishati pekee, hivyo mimi si kwamba ndiye niliyetenga fedha hizo zinazosemwa kwamba hazitoshelezi, lakini hayo si muhimu kwa sasa, muhimu ni kwamba tumepewa fursa nyingine tunakwenda kukaa ili kuona jinsi tunavyoweza kutoka hapa." Shinikizo la kumtaka Ngeleja aachie ngazi lilitokana na kikao cha wabunge wa CCM ambao walikutana juzi mchana na kudai kwamba waziri huyo amewatia aibu kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake kiasi cha kuilazimisha Serikali kuondoa bajeti yake bungeni.

Juzi, Pinda aliondoa hoja ya Waziri wa Nishati na Madini Bungeni akisema hatua hiyo inatokana na hoja nzito zilizotolewa na wabunge wakitaka Serikali kuwasilisha bungeni mpango unaotekelezeka wa kuliondoa taifa gizani kutokana na mgawo wa umeme unaondelea.

Mkulo atema cheche Akizungumzia suala hilo la kujipanga upya na kuja na bajeti bora zaidi itakayokuwa na majibu juu ya tatizo la nishati, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema jana kwamba: "Waziri Mkuu hakusema kwamba tutaongeza bajeti kwa ajili ya kupatikana kwa umeme, bali alisema tutatafuta njia za kuondokana na tatizo la umeme nchini. Njia za kutatua mgawo wa umeme uliopo ni nyingi siyo lazima uongeze fedha za uwekezaji mpya."

Mkulo alisema anaishangaa Wizara ya Nishati na Madini kwa kushindwa kuweka katika bajeti yao njia zisizohitaji fedha za umma kuwekeza ambazo zinaruhusu uwekezaji wa sekta binafsi katika sekta hiyo. "Tulipitisha hapa bungeni Sheria ya PPP, yaani Public Private Patnership (Ushirikiano wa Sekta za Umma na Binafsi), hii inaruhusu sekta binafsi kuwekeza katika miradi ya umeme," alisema Mkulo na kuongeza:

"Ngoja nikwambie, mimi nilikuwa China siku chache zilizopita, pale kuna makampuni manne yako tayari kuja Tanzania kuwekeza bila hata Serikali kutoa senti tano halafu wauze umeme wao Tanesco, sasa hapo si lazima Serikali itoe fedha za mtaji". Mkulo alisema uwekezaji wa Serikali katika uzalishaji wa umeme unaongeza mzigo kwa watumiaji wa nishati hiyo na kwamba ingekuwa vyema Wizara ya Nishati ikatumia mfumo wa kuruhusu wawekezaji ambao wanakuja na mitaji yao. "Tukitumia njia hii, suala la umeme tunaweza kuondokana nalo katika muda mfupi tu usiozidi miezi minne,"alisema
Mkulo.

Mgogoro wa Kanuni
Kuondolewa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kunaashiria mgogoro wa kikanuni baada ya Kamati ya Uongozi ya Bunge iliyokutana juzi jioni chini ya Uenyekiti wa Spika wa Bunge, Anne Makinda kushindwa kukubaliana jinsi ambavyo hoja hiyo itarejeshwa bungeni baada ya kuondolewa chini ya Kanuni ya 69 (1) na 69(2). Kwa mujibu wa marekebisho ya tatu ya ratiba ya Bunge la Bajeti yaliyofanywa juzi jioni na ratiba mpya kutolewa jana, hoja ya Wizara ya Nishati na Madini iliyoondolewa juzi, sasa itajadiliwa Jumamosi, Agosti 13, 2011.

Habari kutoka katika kikao hicho kilichofanyika mara tu baada ya Bunge kuahirishwa juzi jioni, suala la jinsi ya kuwasilisha upya hoja hiyo liliibuliwa na baadhi ya wajumbe na kwamba Spika alisema hoja hiyo itaanza kwa mawaziri husika kuwasilisha maelezo ya mpango wa dharura wa kukabiliana na uhaba wa umeme. Kwa mujibu wa taarifa hizo, baada ya waziri kuwasilisha mpango huo, ataendelea kujibu baadhi ya hoja za wabunge na baadaye Bunge litakaa kama kamati ili kupitisha bajeti hiyo.

Hata hivyo, baadhi ya wajumbe waliozungumza kwa masharti ya kutotajwa majina walitofautina na msimamo huo wa Spika. "Spika alisema hivyo ingawa mimi sikubaliani naye, hapa kuna mgogoro wa kikanuni kwani kanuni hazisemi kitu jinsi ya kurejeshwa kwa hoja iliyoondolewa bungeni," alisema mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Uongozi.

Spika Makinda hakupatikana jana kutoa ufafanuzi wa suala hilo kwani alikwenda Kongwa kuhudhuria mazishi ya bibi mlezi wa Naibu Spika, Job Ndugai. Kutokana na utata huo wa kikanuni hueda Spika akafuata utaratibu uliotumiwa na mtangulizi wake, Samuel Sitta, Julai 2009 wakati Serikali ilipolazimika kuondoa bungeni Bajeti ya Wizara ya Miundombinu wakati huo baada ya wabunge kuikataa.

Mgogoro wa 2009 Julai 2, 2009 aliyekuwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Phillip Marmo alilazimika kuondoa bungeni hoja ya Wizara ya Miundombinu baada ya aliyekuwa Mbunge wa Ilemela, Anthony Diallo kuwasilisha mapendekezo ya kufanya marekebisho makubwa. Waziri wa Miundombinu wakati huo, Dk Shukuru Kawambwa alikuwa amewasilisha makadirio ya matumizi ya wizara yake lakini wabunge wakiongozwa na Diallo waliikataa wakidai kwamba rafu ilikuwa imechezwa katika mgawo wa fedha za ujenzi wa barabara nchini.

Kama ilivyokuwa katika Wizara ya Nishati na Madini juzi, wabunge wengi hawakuunga mkono hotuba ya Dk Kawambwa na kushinikiza yafanyike mabadiliko makubwa ambayo yaliifanya Serikali kuondoa hoja yake na kwenda kujipanga upya.

Hoja ya Diallo ilikuwa ikisababisha kuwepo kwa mabadiliko ya matumizi ya kiasi kikubwa cha fedha, hivyo Spika Sitta aliielekeza Serikali kukutana na Kamati ya Miundombinu ambayo wakati huo ilikuwa chini ya Mohamed Missanga ili kufikia mwafaka. Bajeti hiyo ilipitishwa Julai 4, 2009 siku ya Jumamosi na ikipata wakati mgumu kutokana na maoni mengi yaliyoibuliwa na wabunge wakati Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi, chini ya Mwenyekiti Sitta.

Kabla ya Bunge kukaa kama Kamati ya Matumizi, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Missanga, alisoma taarifa ya kamati yake kuhusu hoja ya Diallo ya kufanya mabadiliko katika matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2009/10.

Katika mchakato huo, Diallo alipewa nafasi ya kutosha mbele ya Kamati na baadaye Waziri Kawambwa kutoa maelezo ambayo yaliwezesha Bunge na Serikali kukubaliana jinsi ya kutatua mgogoro uliokuwepo wakati huo. Kutokana na uzoefu huo, upo uwezekano mkubwa kwa Spika Makinda kuamua kuipa nafasi Kamati ya Bunge ili itoe maoni kuhusu mpango mpya wa Serikali katika kukabiliana na tatizo la umeme kabla ya Bunge kukaa kama kamati na kupitia bajeti hiyo kwa vifungu.

Kadhalika, upungufu wa kanuni unaojiokeza sasa unaashiria kuwapo kwa umuhimu wa kanuni hizo kupitiwa upya, ili kukidhi matakwa ya kimatukio yanayojitokeza sasa hivyo kumpa nafasi kubwa Spika kuamua jambo "kadri anavyoona inafaa".

SOURCE: Ngeleja:Tatizo la umeme ni la Serikali nzima

ngeleja ajiuzulu kwanza ndo aongee maneno hayo, yeye anaongea kama nani? mbona hawa watu ni ving'ang'anizi hivyo?
 
i affirm with mwanakijiji's stand, tatizo la umeme ni la serikali kwa ujumla yake, wizara kama msimamizi mkuu wa shughuli za nishati hii Tanzania pia inawajibika kwa kutofuata ushauri wa kitaalamu ulioletwa na TANESCO kupitia mpango mkakati wa muda mrefu na mfupi, kuendelea kulitumia shirika kisiasa, kuchagua watendaji wakuu wasio na uwezo na kushindwa kuwawajibisha wote waliotuingiza kwenye mikataba mibovu

kwa sasa hivi wameguarantee tu TANESCO kukopa hela ili kubadilisha hali ya umeme, wameshindwa kujua TANESCO tayari inalipia bills mbalimbali out of mikataba mibovu kama IPTL, Songas, na sasa hivi wanalipa Symbion, wana loadshed wana 300bn syndication loan.. bado Aggreko itakayozalisha only 100MW itachukua theluthi moja ya mapato ya TANESCO kwa mwezi, sasa tujiulize serikali ina ufahamu kuwa kila mwaka mahitaji ya umeme yanaongezeka kwa asilimia 10 hawa ni Large power users na hivyo kusababisha kuwe na ongezeko la 100MW kwa mwaka,

kwa sasa total grid demand ni kama 880 ila total installed capacity ni 1100MW ( almost ) hivyo kama mitambo yote ingekuwa @ full capacity at any given day hakukutakiwa kuwe na mgao, hivyo basi ni lazima juhudi za makusudi zifanywe kunusuru hali ya uchumi nchini, huwezi kuvutia uwekezaji na shughuli za kukusanya mapato ukiwa kwenye mgao wa umeme

kauli yangu ni hii, both TANESCO, WIZARA na Serikali ni wakulaumiwa, siwezi kufanya uchambuzi kama wa mwanakijiji ila TANESCO wanalaumiwa kwa kukosa umakini na kushindwa kusimamia proffesion yao,
 
We have to start from somewhere.., and Ngeleja is as good a start as anyone..
Nobody is saying the previous people did a wonderful Job.., and because the cracks are now showing now more than ever, we need to set an example that these jobs must be result oriented..., and not politicization of the issue...

Here is your problem...you are personalizing the crisis and that is where you go wrong. Yes, we have to start from somewhere but it has to be with concrete and viable plans. Getting rid of Ngeleja will not all of a sudden end the crisis if there are no viable and alternative plans in place.

Hivi huyu jamaa alitwambie ni lini mgao utakuwa Historia????. , Kwa mimi kufata kauli yake kama waziri nikatumie funds zangu kwemye shughuli nyingine badala ya kununua Generator!!!, This man has cost me and is costing me a lot.... (and am afraid am not the only one)

Hata Kikwete aliwaambia atawaletea maisha bora kwenu nyote. Yako wapi sasa hayo maisha bora? Why aren't you calling for his resignation also? He's been at the helm for how long now? Hellooooooo
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Back
Top Bottom