Ngeleja na utetezi wa uongo nje ya Bunge

Wakuu wangu JF, i beg to differ na namna kauli ya Ngeleja ilivyochukuliwa out of context. Kauli yake ni nzito na inahitaji tafakari siyo kuibeza pengine kwa kuangalia upande mmoja tu. Ninaamini anachotaka kusema ni kwamba kwa kutambua ukubwa wa tatizo la umeme wao kama wizara waliomba bajeti kubwa ambayo inatoa majibu ya muda mfupi kwa tatizo la umeme lakini hawakupewa allocation waliyoiomba hivyo anashukuru kwa wabunge kuliona hilo na hivyo pengine kile ambacho wizara walikiomba kinaweza kupatikana na hivyo kupata majibu yanayotarajiwa na wananchi kwa kipindi cha muda mfupi. Kama wakati wa mtikisiko wa uchumi tulikuja na stimulus package ya kisanii na kutenga zaidi trillion 1 kwaajili ya wafanyabiashara hewa wa pamba! Tunashindwa kuja na emergency plan/rescue plan kwaajili ya tatizo la umeme? Kipi ni muhimu zaidi kwa taifa kati ya stimulus package aliyoipeleka Jk bungeni kwa mbwembwe na emergency plan ya umeme ambayo ni muhimu kwa kila sekta ya uchumi nchini? Tutafakari! Tuache kumuona Ngeleja wakati wote ni tatizo! Tusifanye mambo kishabiki tu! Majibu tunayoyahitaji kwa Ngeleja kwasasa ni shabaha ya barua ya Jairo kwa taasisi zilizoko chini ya wizara yake na nini yalikuwa malengo ya matumizi ya fedha hizo. La mgao wa umeme linahitaji utashi wa kisiasa na maamuzi magumu ya Mkuu wa Kaya ambaye tunahitaji maelezo ya kina kuhusu safari zake za nje na mafanikio yake kama tumeendelea kuwa na mdororo kwenye sekta ya umeme kwa miaka yote sita aliyokuwa madarakani. Mhh Urais siyo kuzunguka tu na ndege ya Rais!!
 
Sawa kinyamana!
Ila inabidi ajiuzulu kutokana na corruption ambayo ilitakiwa kutembezwa ili bajeti ya wizara yake ipitishwe.....
Ingawa tunajua uliyoyasema ni CRAP,tunakupa the benefit of doubt kwa mengineyo yote.Ila hili la rushwa ni lazima ajiuzulu.
 
Wakuu wangu JF, i beg to differ na namna kauli ya Ngeleja ilivyochukuliwa out of context. Kauli yake ni nzito na inahitaji tafakari siyo kuibeza pengine kwa kuangalia upande mmoja tu. Ninaamini anachotaka kusema ni kwamba kwa kutambua ukubwa wa tatizo la umeme wao kama wizara waliomba bajeti kubwa ambayo inatoa majibu ya muda mfupi kwa tatizo la umeme lakini hawakupewa allocation waliyoiomba hivyo anashukuru kwa wabunge kuliona hilo na hivyo pengine kile ambacho wizara walikiomba kinaweza kupatikana na hivyo kupata majibu yanayotarajiwa na wananchi kwa kipindi cha muda mfupi. Kama wakati wa mtikisiko wa uchumi tulikuja na stimulus package ya kisanii na kutenga zaidi trillion 1 kwaajili ya wafanyabiashara hewa wa pamba! Tunashindwa kuja na emergency plan/rescue plan kwaajili ya tatizo la umeme? Kipi ni muhimu zaidi kwa taifa kati ya stimulus package aliyoipeleka Jk bungeni kwa mbwembwe na emergency plan ya umeme ambayo ni muhimu kwa kila sekta ya uchumi nchini? Tutafakari! Tuache kumuona Ngeleja wakati wote ni tatizo! Tusifanye mambo kishabiki tu! Majibu tunayoyahitaji kwa Ngeleja kwasasa ni shabaha ya barua ya Jairo kwa taasisi zilizoko chini ya wizara yake na nini yalikuwa malengo ya matumizi ya fedha hizo. La mgao wa umeme linahitaji utashi wa kisiasa na maamuzi magumu ya Mkuu wa Kaya ambaye tunahitaji maelezo ya kina kuhusu safari zake za nje na mafanikio yake kama tumeendelea kuwa na mdororo kwenye sekta ya umeme kwa miaka yote sita aliyokuwa madarakani. Mhh Urais siyo kuzunguka tu na ndege ya Rais!!

Kama alitaka kueleza hayo unayoeleza alikuwa na sababu gani ya kuzunguka mbuyu na kufanya aeleweke tofauti na msimamo wa wabunge bungeni si angekuwa straight? . Hapa hakuna ushabiki kwa sababu tunaandika tulichosikia kutoka kwake alipotoka nje ya ukumbi wa bunge mkuu. Hatufanyi kazi ya kumpepea, kumrushia maua na kuimba anameremeta hapa bali kuhoji ufahamu wake wa tatizo liliofanya bajeti ikawa shelved.
 
Back
Top Bottom