MVUMBUZI
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 5,182
- 2,304
Kuna uwezekano mkubwa Mh. Ngeleja akawa aidha hajui anachokifanya au anajidai yeye ana akili sana kuliko wa TZ wote. Kila mtanzania aliyekuwa anaangalia Bunge live jana saa 11:00 -11:15 wakati Waziri Mkuu anatoa comments za kusitisha kupitishwa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini alisikia SABABU KUU za kutopitishwa kwa bajeti ni Wizara kutoainisha mkakati wa haraka wa kumaliza tatizo linaloendelea la mgao wa umeme nchi nzima. Hii ndiyo sababu Waziri Mkuu akaliomba Bunge wiki 3 ili waandae huo mkakati wa kuondoa tatizo la umeme na wa ulete mbele ya bunge.
Cha kushangaza Ngeleja alipotoka nje ya ukumbi na kuhojiwa na waandishi alisema kinafiki" kwanza nawashukuru wabunge kwa kuliona hili kwamba eti bajeti imehairishwa kwa sababu wizara haikupangiwa hela za kutosha na hizi wiki tatu ni za kutafuta hizo hela then warudishe bajeti bungeni" . Hapa alitofautiana kwa kiasi kikubwa si tu na waziri mkuu bali na wabunge na kujaribu kueleza uongo wa papo hapo kuhusu sababu za bajeti yake kukataliwa.
Hii inadhihirisha bado Ngeleja hajalielewa tatizo la mgao wa umeme na hataki kulielewa na hii ni hatari kama atahusishwa kwenye hiyo task force ya Waziri Mkuu kwa sababu mawazo yake bado yana chembe chembe nyingi za ubabaishaji na atakwamisha hiyo task force. Pia kwa utetezi wake wa uongo jana pale nje ya ukumbi wa bunge inadhihirisha jinsi Ngeleja alivyo incompetent na kazi anayoifanya na pia jinsi ambavyo serikali inatakiwa impunguzie mzigo haraka iwezekanavyo kumpangia kazi anayoweza kuifanya kwa uaminifu, ufanisi na umakini zaidi.
Kwa ufupi uwaziri imemshinda Ngeleja na ni wazi inaonekana ni kikwazo kikubwa cha kutatua tatizo kubwa linaloikabili nchi kwa sasa.