Ngeleja na Malima wawajibishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja na Malima wawajibishwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Jul 28, 2012.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Sasa iko wazi, Ngeleja kwenda kujiunga na wafanyakszi wa Wizara kumpokea Jairo na kumkumbatia

  Skendo la mafuta ya kuendesha mitambo kuzalisha Umeme

  Mgao feki kwa kipindi chote wamekuwa Mawaziri wa Wizara ya nishati na madini

  Malima kuwa na pesa nyingi za kigeni hadi kuogopa kuweka benki na kulazimika kusafiri nazo hadi vijijini huku akiwa na bunduki mbili kujilinda

  Kukataa kutumia sheria mpya ya madini kufanya maboresho yarabaha. Mawaziri wapya tayari wameshaboresha

  Kukataa kusimamia makampuni ya uchimbaji kulipa jamii inayozunguka migodi service charge. Sasa limesimamiwa kwa kuanzia na Resolute ya Nzega

  Kulea menejimenyi na bodi dhaifu za Tanesco na migongano ya kimaslahi na shirika

  Kuajiri Mkurugenzi wa Tanesco ambaye siyo mwadilifu

  Etc

  Kwanza huyo Kigoma Malima anyanganywe unaibu Waziri mara moja

  Pili Malima na Ngeleja wapelekwe pale Mtaa wa Kongo Kariakoo wakashuhulikiwe na wananchi. Hili siyo jukumu la Takukuru. Kukosa ufwisadi wao tungekuwa sasa na flyover hadi Karagwe, madaktari wasingegoma, shule zingekuwa bora kuliko zile za Marekani
   
 2. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nakuunga mkono kabisa wanhusika asilia 100 haiwezekani uozo wote huu wasiwe wanaujua.
   
 3. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Wana JF,

  Naomba samahani sana kwa hizi threads tunazozianzisha zikigongana kwa hoja ile ile. Ni kwa sababu kuna mapya yanazuka na tungetamani sana wahusika wayaone ili wafahamu kwamba tunafahamu madudu yao. Labda wataona aibu.

  Kuna hawa watu wawili wanaojiita vijana, January na Zitto. Hawa jamaa ktk kamati za Bunge walikuwa pamoja. January akiwa mwenyekiti wa hii kamati iliyotangazwa kuvunjwa na mwenzake ile ya mahesabu ya mashirika ya umma. Kwa ufupi watu hawa walifahamu kwa undani kabisa yanayotokea ndani ya Tanesco. Kama hawakujua basi nitawaitwa wenye uwezo mdogo, au wanaojifanya ili kukwepa ufisadi maana kuna watu bora uwaite 'mbumbumbu' kuliko kuwaita mafisadi.

  Wote kwa pamoja wasingeweza kushindwa kugundua madudu haya yaliyoonyeshwa wazi jana na leo. Uzuri ni kwamba wana ushirikiano wa karibu sana na hata siku chache zilizopita wakati Zitto akichangia hoja ya Wizara ya Sayansi, ambayo January ni naibu waziri, nilichokiona ni kwamba walipeana mamabo ya kuzungumza. Zitto alichangia mambo ambayo walikwisha yajadili na January. Hata January alipotoa majibu kwa Wabunge alionyesha wazi kwamba alimuelewa vizuri Zitto na alirudia aliyoyasema Zitto.

  Kwa uhusiano wao huo na kwa haya yaliyokuwa yakitokea TANESCO, tunaomba tufahamu ni nini alichokifanya January. Yote yaliyofanywa na TANESCO January alikuwa mwenyekiti wa kamati husika ya Bunge.

  Kama alivyo Zitto, January pia ni mtu wa kumiliki mawazo. anajipanga kuzungumza kwa mtindo unaoonyesha kwamba hakuna mwingine. Maneno yake hayana labda kwa hiyo kila wakati hana mashaka kabisa! Kabisa! sasa leo asije akasema eti alikuwa hajui. Hata kama hesabu kwake ni ndoto asingeweza kutoona jambo kama hili la makusudi.

  Naomba orodha ya kuwachunguza TANESCO hawa wote wajitokeze pamoja na Ngereja na Malima.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ni wazo zuri sana kama watu hawa watahusika ktk uchunguzi na ushahidi wa madai ya Tanesco. Lakini ningeomba tu kusema kwamba hakuna sababu ya kuwatuhumu ila kuna umuhimu wao kuwepo ili ukweli upatikane. Wanahitajika sana kutoa maelezo au ushahidi wa yale wanayoyafahamu wao ama waliyaona..
   
 5. D

  DR. RICHARD Senior Member

  #5
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwendo ni mmoja tunachotaka sisi raia ni usawa kwa wote katika nchi hii aijalishi cha Zitto wala January, hata kama ni mambo ya chama chetu M4c hatuwezi kumsamehe bora yeye akae pembeni sisi tusinge na chama chetu hasa hasa na nchi yetu, hata hivyo alishalalamikiwa mara kibao kwa hiyo dalili zimeonesha muda mrefu, lazima ajadiliwe na chama na chama nadhani hakiwezi kukubali kuchafuka kwa ajili yake, tutasikkitika tu kwamba tulianzanaye pamoja tutamaliza kivyetu!
   
 6. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,478
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono, lakini hayo tunaonge sisi lakini wao ukiwauliza watakuambia hawahusiki na hata serikali itasema hivyo kwa sababu wameishawajibishwa.
   
 7. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Madudu nchi hii ni mengi na wengi wamefanya madudu. Kwa namna moja ama nyingine uliowataja wanahusika kulea matatatizo kwenye shirika la umeme. Lakini kiini cha tatizo ni mfumo duni wa undeshaji wa taasisi za kiserikali na bunge kama mhimili wa utawala wa nchi hii. Ukitaka kuangamiza malaria nenda kwenye "source" inayozalisha mbu na sio kutoa "quin" ama kutumia chandarua.
  Swali la msingi, je nchi yetu ina sera ya umeme? ama kwenye "big picture" sera ya nishati ipo? na kama ipo inasemaje? Ukianzia kutengeneza huko kwenye chanzo cha matatizo utagundua kuwa Shirika la Ugavi wa umeme halitakiwi kuwapo kama lilivyo sasa hivi. Viongozi wa serikali kuu na baadhi ya wabunge hawataki kuelewa hivyo kwasababu wanamaslahi makubwa sana kupitia taasisi zilizopo chini ya kivuli cha Nishati na Madini. Hio ndio inapelekea mvutano kwani kuna kundi la waliokosa na waliopata na yataendelea kukinzana kama mfumo hautafumuliwa na kujengwa upya. Hii sinema ilichezwa kwenye Richmond saga....ikajirudia kwa Jairo na sasa imerudi haraka sana kwenye kamati za kibunge na katibu mkuu wa wizara. Ni kama vita ya kuviziana...........wala sio suluhu ya tatizo la msingi.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,588
  Likes Received: 82,143
  Trophy Points: 280
  Uchunguzi huu pia uanike hadharani majina ya Wabunge wote waliochukua rushwa toka Nishati na Madini katika kikao cha mwaka jana cha bajeti ili kuipitisha bajeti ya wizara hiyo kinyemela.
   
 9. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Mimi nakuunga mkono 100% kutokana na ukweli kwamba mara tu baada ya kishindo cha CDM katika uchaguzi mkuu wa 2010 Serikali ilikuwa kama vile imeingiwa na hofu hivyo January Makamba akiwa Mwenye kiti wa Kamati ya Nishati na Madini na ZittO akiwa mwenyekti wa kamati ya Mashiriki ya Umma walianzisha utaratibu wa kuiendesha Seriakli kwa maana ya Wizara zilizo chini yao hususan Tanesco kwa remote. Nyakati zingine walidiriki kuingilia maamuzi ya Wizara na manejimenti ya Tanesco. Ni kwa mantiki hiyo Mhe Zitto alikurupuka kumtetea Eng Mhando hata katika jambao ambalo lilikuwa halihusu Kamati yake kwani upitishwaji wa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini unaihusu Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. Mara tu baada ya Mhando kusimamishwa Zitto alikumbwa na kimbelembele gani?
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,588
  Likes Received: 82,143
  Trophy Points: 280
  [h=2]Dar`s power blues: How Tanesco loses billions[/h]


  By Florian Kaijage  28th July 2012


  When politicians, notably Members of Parliament, wanted electricity at any cost – and threatened to block the budget estimates of the ministry of energy and minerals last year -- little did they know they were also courting financial dire straits for the state-owned power utility firm.

  Though they won the battle, the war still holds because the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) is now spending half its revenue on exorbitant capacity charges to independent power producers.

  These costs do not include the price tag for buying power from the same independent power producers – while the so-called capacity charges still have to be paid whether Tanesco consumes electricity or not.

  Capacity charge is money paid to the owner of the power generating plant regardless of the operation of that plant, which means the money accumulates every month and has to be paid even if the plants were to switch off.

  As things now stand, Tanesco's monthly collections between July and December, this year, stand at an average Sh94 billion per month, but the firm will have to spend half of that money on capacity charges, with the biggest chunk of it goes to Symbion Power -- the company that inherited the controversial operations of Dowans Tanzania.

  The revelations come amid claims that the cash-strapped power utility is making a huge profit from its monthly revenue collections, but the firm cannot sustain its operational cost.

  According to Tanesco's financial analysis and forecast for the period under question (July-December), capacity charges alone would cost the state power utility a whopping Sh256 billion. At the same time, Tanesco will spend another Sh331 billion during the same period an average of Sh55 billion per month to buy electricity from private producers, The Guardian has established.

  This means monthly that, when all the sums are done, Tanesco will be left with a monthly deficit anounting to Sh3 billion shillings.
  The Minister for Energy and Minerals, Professor Sospeter Muhongo was quoted this week as saying that Tanesco's income stood at Sh94 billion a month and put the firm's monthly recurrent expenditure at a mere Sh11 billion – rubbishing Tanesco's apparent financial crisis – and argued that Tanesco doesn't need any fiscal assistance from the central government. He also queried the expenditure of the remaining money after deductions of recurrent expenditures, such as salaries.

  According to the financial analysis and forecast, the biggest winners in Tanesco's spending spree are Songas, Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Symbion and Aggreko.

  Symbion alone will pocket a staggering Sh85.755 billion in the next six months in capacity charges from its plant located in Dodoma, but would still sell power to Tanesco worth Sh19.602 billion -- which surpasses its ability to sell by more than 400 percent. According to technical documents made available to The Guardian, the same company (Symbion) would receive a monthly Sh74.327 billion over the next six months (Sh12 billion) in capacity charges, but would still sell power worth Sh20 billion at its heavy fuel powered plant in Arusha.

  Songas is meanwhile projected to make Sh28.248 billion in capacity charges over the same period, but would sell power worth Sh56.103 billion (Sh9 billion) every month. IPTL is the only independent producer making lowest returns on capacity charges, projected at Sh4.964 billion during a period it expects to produce energy worth Sh168.9 billion.

  Symbion Dar es Salaam will also comparatively lower expenses on capacity charges against money spent on power purchases, now currently estimated at monthly incomes of Sh22 billion in capacity charges and Sh35.3 for sale of energy from its Jet A1 fuel-powered plant, while Aggereko would receive is Sh12 billion in capacity charges compared to Sh24.691 for energy produced.

  This paper has also established that Tanesco has projected to spend Sh69.83 billion in the next six months on fuel and lubricants to run the independent power plants and some owned by Tanesco – all amounting Sh11.6 billion.
  In its last edition of July 22, our sister paper, The Guardian on Sunday carried a story on an apparent dark cloud of power shedding should the government back down on its own pledges to bail out its money-starved Tanesco.

  That came in the wake of apparent government attempts at shifting goal posts, analysts said, citing suspension of Tanesco's top management as a case in point.

  The Permanent Secretary of the Ministry of Energy and Minerals, Eliakim Maswi, had earlier accused the state-owned utility firm's top managers of ‘intentionally' planning and initiating power rationing to damage the credibility of the government in the Parliament.

  Analysts said there was a close link between the financial crisis facing the cash-strapped power firm and its failure to secure a Sh408 billion loan from the consortium of local banks, as well the government's delayed guarantee required by the lenders. They are instead processing for $65 million (Sh103) billion as a bridge financing to Tanesco, according to Finance Minister, Dr William Mgimwa.

  Fears of a repeat period of black-outs stem from the fact that while the government has not honoured its financial commitments to Tanesco – made public inside Parliament last August -- the level of waters in the main hydropower generation dams is dropping drastically, with the likelihood that it could worsen by the end the year.
  However, the ministry of Energy and Minerals through it minister, Professor Muhongo and Permanent Secreatry, Elikim have dismissed any possibility of power crisis noting that there were enough initiatives to avoid power rationing and ensure reliable power generation and supply.
  The duo concurred in their statement early this week that there was enough money to purchase fuel for independent power generating plants and that the situation was manageable.  SOURCE: THE GUARDIAN
   
 11. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Nimekwisha jipima kama mimi ndo ningekuwa mpangaji wa magogoni hali ingekuwaje! Hapa ni kwa nadhalia kwamba yoote yalikuwa yakifanyika bila fahamu zangu. Na kwamba mimi sina skendo yoyote ile, tangu ya kubeba wanyama hai mpaka ile ya kumiliki vituo vya mafuta nchi nzima.

  Sijui kama hawa wananchi watatu wangekuwa tena huko beadroom kwao. Hakika kwa hasara ya kitaifa iliyotokea kwa mgao wa umeme, ningekwisha amua kutumia ile nguvu ya kizuizini.

  Mbona Iceland Rais wao mstaafu kashitakiwa kwa kusababisha matatizo ya kiuchumi mwaka jana?
   
 12. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Naomba Rais Kikwete alisisitize hili katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi ili kurejea utawala bora kama alivyoagiza wakati anafungua Bunge. Apigilie msumali wa nchi sita kuunga mkono maagizo ya Spika na kuongeza maagizo ya Mwanasheria mkuu wahusika wote wafikishwe mbele ya sheria haraka sana.

  Halafu mambo kama haya ndipo hata usalama wa Taifa unaweza kurejesha hadhi yao kwa kutusaidia kuingia deep na kuleta walichokiona hapo TANESCO na wamiliji wa hiyo mitambo na kesi zisizoisha kama ya IPTL anayoisimamisha Mkono. Uchunguzi wao utachukuliwa moja kwa moja kwa uzitio wake na kujadiliwa katika kamati ya maadili ya Bunge.

  Tuendelee kuwataja wezi maana wanajulikana ili tuliokoe Taifa letu. Nilisema polepole yote yatajulikana , nashukuru Mola imekuwa hivyo.
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  naomba kwanza mtutajie hiyo kamati iliyovunjwa yoote

  ya sasa ikoje ikoje?

  majina please
   
 14. d

  dagjrtz Member

  #14
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  jamani hii nchi shamba la bibi natamani na mimi ningekuwa mwekezaji wa kigeni (najua lugha tofauti na inayoeleweka na wapenda ufisadi). ????
   
 15. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #15
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,102
  Likes Received: 1,492
  Trophy Points: 280
  Wote kwa pamoja wasingeweza kushindwa kugundua madudu haya yaliyoonyeshwa wazi jana na leo. Uzuri ni kwamba wana ushirikiano wa karibu sana na hata siku chache zilizopita wakati Zitto akichangia hoja ya Wizara ya Sayansi, ambayo January ni naibu waziri, nilichokiona ni kwamba walipeana mamabo ya kuzungumza. Zitto alichangia mambo ambayo walikwisha yajadili na January. Hata January alipotoa majibu kwa Wabunge alionyesha wazi kwamba alimuelewa vizuri Zitto na alirudia aliyoyasema Zitto.
  Huyu January Makamba bado hajaacha mchezo wake wa kupata maswali kabla na kuwa tayari na majibu anapoulizwa kwani hii tabia ndio ilisababisha akafutiwa matokeo yake ya form four
   
 16. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Sidhani kuwa kuna mwamanchi yeyote wa Tanzania ya leo atakayeamini kutokea jambo kama hilo. Kutegemea Mkuu wa nchi hii alizungumzie swala la TANESCo kwa ukweli wote si kitu rahisi hata kidogo na wala usitegemee. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo.
  Kwanza yeye mwnenyewe ndiye anayeteua Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa shirika
  Plili ndiye anayeteua Meneja Mkuu wa Shirika
  Tatu Februari Minyororo ni mtu wake wa karibu sana, na haiwezekani hata kidogo asiwe anahusika, aidha alifahamu fika kilichokua kinaendelea TANESCO.
  Nne yeye mwenyewe ndiye aliyeteua viongozi wa TAKUKURU, na hii ni moja wapo ya kazi walizostahili kuzifanya na kuhakikisha shirika nyeti kama hili halitafunwi kipuuzi namna hiyo na kuua uchumi wa nchi kiasi hiki.

  Sasa kama kweli kutakuwepo nia thabiti ya kulizungumzia hili swala la TANESCO kwa uwazi inabidi pia aweze kuwataarifu wananchi, haswa baada ya Waziri kuwataja bungeni wanaoliibia shirika, basi awe pia na ujasiri wa kuwatajia wananchi kuwa serikali yake inadaiwa kiasi gani na TANESCo, pamoja na taasisi zote including Ikulu zote. Na atoe ahadi kwa wananchi kuna mkakati gani na ni lini watarekebisha mapungufu hayo.
   
Loading...