Ngeleja kalipotosha bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja kalipotosha bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchambuzi, Aug 18, 2011.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Nimebaki kujiuliza je wabunge makini walikuwa wapi wakati waziri wa Nishati William Ngeleja anatoa matamshi yasio na ukweli kwamba “ongezeko la bei ya umeme litakalotangazwa na serikali halitagusa wananchi wa kipato cha chini, na badala yake ongezeko litagusa mashirika, migodi na taasisi nyingine kubwa zinazotumia zaidi ya uniti 50 kwa mwezi”??

  Neno ‘kugusa’ hapa lina maana gani kwani suala la msingi hapa ni nani atabeba mzigo, period. Hivi Mawaziri huwa wanashauriana na wachumi kabla ya kuja na kauli za ovyo ovyo kama hizi? Kwani kupanda kwa gharama za umeme na hata mafuta wakati wote anaebeba mzigo si ni mtumiaji/mwananchi wa kawaida?

  Kwa vyovyote vile, ongezeko la bei ya umeme kwa wazalishaji wakubwa na hata wadogo kutachochea wenye viwanda au wazalishaji kupandisha bei ya bidhaa wanazozalisha iwe cement, sukari, unga wa sembe n.k - ni mwananchi wa kawaida ndie atakayefidia moja kwa moja gharama za wazalishaji zitakazo tokana na ongezeko la bei ya nishati, na mtu kutambua hili halihitaji kuwa a rocket scientist.

  Wawakilishi wetu bungeni, lazima mkubali kwamba hamkuwa makini katika hili na mmewangusha wapiga kura wenu.
   
Loading...