Ngeleja atajwa katika ‘dili’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja atajwa katika ‘dili’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 22, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  [​IMG]
  Na Mwandishi wetu - Imechapwa 20 June 2012

  [​IMG][​IMG]
  WAZIRI wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngeleja ametajwa katika "mpango" wa kampuni binafsi inayodaiwa kutaka kuchota fedha katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), MwanaHALISI limeelezwa.

  Ngeleja anadaiwa kutambulisha wamiliki wa kampuni ya Asia Business Channel (ABC) kwa ofisa mmoja wa TMAA; kampuni ambayo sasa inadaiwa kukaba koo mamlaka kwa kuidai pauni za Uingereza (GBS) 35,500 (sawa na Sh. 100 milioni).


  Taarifa zinasema ABC walikwenda TMAA kuomba kutengeneza programu ya televisheni kwa ajili ya kutangaza shughuli za uwekezaji katika sekta ya madini.


  Mtoa taarifa wa gazeti hili amesema, kwanza walikataliwa, lakini baadaye ofisa wa TMAA alikubaliana nao kwamba iwapo watapata fedha, watawaita ili watengeneze programu hiyo.


  Hatua hiyo ilifuatiwa maandishi kuwa ofisa wa TMAA awafahamishe, ifikapo Julai mwaka huu iwapo mpango huo umekubaliwa na fedha zimepatikana.


  Februari mwaka huu, miezi mitano kabla ya muda wa ahadi, ofisa aliwaandikia barua pepe akiwaeleza kuwa fedha kwa ajili hiyo hazitapatikana. Ndipo ABC wakaanza kudai kuwa TMAA wamevunja mkataba wa kulipwa GBS 35,500.


  Lakini Ngeleja alipohojiwa na gazeti hili juzi Jumatatu usiku, alisema "Hakuna kitu kama hicho. Kwa ufafanuzi zaidi, naomba uwasiliane na CEO wa TMAA ambaye atakupa ukweli zaidi."


  ABC imetishia kushitaki TMAA kupitia wakili mashuhuri nchini, Nimrod Mkono ambaye imeelezwa tayari amewapelekea hati ya madai.


  Mtoa taarifa anasema, "…ni juzi tu mtendaji mkuu (CEO) wa TMAA alipokea barua kutoka kwa kampuni ya mawakili ya Mkono ikimtaka kulipa Pauni 35,500 ndani ya siku kumi, vinginevyo watafungua kesi mahakamani."


  Mwandishi alimfuata Paul Masanja, mtendaji mkuu wa TMAA kutaka kujua iwapo kulikuwa na kitu kama hicho.


  Masanja amekiri kuwepo kwa madai hayo lakini amekataa kuongea kwa urefu, akisema gazeti liongee na mwanasheria wa mamlaka.


  Mwanasheria Bruno Mteta ameliambia gazeti hili kuwa suala hilo "…si uongo, ila hakuna kinachoweza kuitwa mkataba kati ya TMAA na ABC."


  "Hawa watu wenye kampuni kutoka Uingereza, walikuja TMAA na kutaka kushirikiana na wakala kutangaza vivutio. Walijibiwa kwamba wakala hahusiki na kazi hiyo kwani wao wanashughulika tu na kazi ya ukaguzi," amesema Mteta.


  Amefafanua kuwa inaonekana ABC walitaka Tanzania ijitangaze; lakini walijibiwa kuwa "Kazi ya TMAA ni ukaguzi tu siyo kutangaza vivutio."


  "Tuliona wale jamaa labda wamepotoshwa tu," ameongeza.


  Hata hivyo, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi amekana kufahamu suala hilo ambalo CEO wa TMAA na mwanasheria wao wanajua na wamelitolea maelezo.


  Alimwelekeza mwandishi aende ofisini kwake Jumanne ili aangalie iwapo "kuna kitu kama hicho."


  "Tangu ulipoanza kunitafuta nimekuwa vijijini mkoani Dodoma kikazi. Kwa sasa, na hivi tunavyoongea, nipo njiani kurudi Dar es Salaam. Ukinitafuta kesho (jana), labda naweza kukueleza zaidi…" amesema Maswi.


  Ofisa mmoja Hazina ameliambia gazeti hili, "Hata pale kwetu tuliishakumbana na kampuni kama hizi, zikilazimisha ushirikiano na ubia hata pasipowezekana."

  Jitihada za kupata anwani na simu za ABC zimeshindikana, lakini ofisa mmoja wa TMAA ameahidi kulipa gazeti baruapepe ya kampuni hiyo.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wakati wa JKT najua Lau Masha asinge fanya Kazi Serikalini; Ngeleja sijui lakini ni kwanini Wamekuwa Walafi hivyo?

  Ina Maana Wazee wetu walio Madarakani pia wao ni Walafi kiasi hicho? Kama Vile Mzee Malecela, Mzee Msekwa najua

  Watoto wao wote wanafanya kazi Nje na Wametulia Wazee Wanawafadhili; Walikuwa Wanaimba Siasa Ya Ujamaa na

  Kujitegemea kiunafiki? Ni bora kuuwawa na Mwizi kuliko kusengenywa na Mnafiki...
   
 3. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa nini magamba mpaka leo hawajamfikisha korokoloni ngeleja? Ndo maana chama kinafulia kwa kuwakumbatia watu kama hawa
   
 4. m

  mahoza JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Dhaifu.
   
 5. R

  Ramso5 Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huyu jamaa kwa madili ni stadi.Hapa mwanza anaendesha mchezo mchafu wa kutaka kupora kwa nguvu nyumba ya watoto yatima kwa kumtumia wakili mmoja mzee asiye mwadilifu aitwaye Rugaimukamu, mpango ambao uko mbioni kukamilika ambao unaratibiwa na hakimu ajulikanaye kwa jina Masesa.Nilishangaa ngeleja alipata wapi ujasiri wa kupiga kelele bungeni kushambulia wengine wakati yeye si mwadilifu yaani anadiriki kutaka kudhulumu mali ya yatima.joseph kando mkama anakupeleka pabaya
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,831
  Trophy Points: 280
  Ngeleja ni fisadi sana.
   
 7. MAWAZO UJENZI

  MAWAZO UJENZI JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 1,730
  Likes Received: 622
  Trophy Points: 280
  Hivi wasukuma siku hizi wamekuaje? Chenge,Ngeleja na Ndugu yangu Maige jamani
   
 8. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  WAZIRI wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngeleja ametajwa katika “mpango” wa kampuni binafsi inayodaiwa kutaka kuchota fedha katika Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA), MwanaHALISI limeelezwa.Ngeleja anadaiwa kutambulisha wamiliki wa kampuni ya Asia Business Channel (ABC) kwa ofisa mmoja wa TMAA; kampuni ambayo sasa inadaiwa kukaba koo mamlaka kwa kuidai pauni za Uingereza (GBS) 35,500 (sawa na Sh. 100 milioni).Taarifa zinasema ABC walikwenda TMAA kuomba kutengeneza programu ya televisheni kwa ajili ya kutangaza shughuli za uwekezaji katika sekta ya madini.Mtoa taarifa wa gazeti hili amesema, kwanza walikataliwa, lakini baadaye ofisa wa TMAA alikubaliana nao kwamba iwapo watapata fedha, watawaita ili watengeneze programu hiyo.Hatua hiyo ilifuatiwa maandishi kuwa ofisa wa TMAA awafahamishe, ifikapo Julai mwaka huu iwapo mpango huo umekubaliwa na fedha zimepatikana.Februari mwaka huu, miezi mitano kabla ya muda wa ahadi, ofisa aliwaandikia barua pepe akiwaeleza kuwa fedha kwa ajili hiyo hazitapatikana. Ndipo ABC wakaanza kudai kuwa TMAA wamevunja mkataba wa kulipwa GBS 35,500.Lakini Ngeleja alipohojiwa na gazeti hili juzi Jumatatu usiku, alisema “Hakuna kitu kama hicho. Kwa ufafanuzi zaidi, naomba uwasiliane na CEO wa TMAA ambaye atakupa ukweli zaidi.”ABC imetishia kushitaki TMAA kupitia wakili mashuhuri nchini, Nimrod Mkono ambaye imeelezwa tayari amewapelekea hati ya madai.Mtoa taarifa anasema, “…ni juzi tu mtendaji mkuu (CEO) wa TMAA alipokea barua kutoka kwa kampuni ya mawakili ya Mkono ikimtaka kulipa Pauni 35,500 ndani ya siku kumi, vinginevyo watafungua kesi mahakamani.”Mwandishi alimfuata Paul Masanja, mtendaji mkuu wa TMAA kutaka kujua iwapo kulikuwa na kitu kama hicho.Masanja amekiri kuwepo kwa madai hayo lakini amekataa kuongea kwa urefu, akisema gazeti liongee na mwanasheria wa mamlaka.Mwanasheria Bruno Mteta ameliambia gazeti hili kuwa suala hilo “…si uongo, ila hakuna kinachoweza kuitwa mkataba kati ya TMAA na ABC.”“Hawa watu wenye kampuni kutoka Uingereza, walikuja TMAA na kutaka kushirikiana na wakala kutangaza vivutio. Walijibiwa kwamba wakala hahusiki na kazi hiyo kwani wao wanashughulika tu na kazi ya ukaguzi,” amesema Mteta.Amefafanua kuwa inaonekana ABC walitaka Tanzania ijitangaze; lakini walijibiwa kuwa “Kazi ya TMAA ni ukaguzi tu siyo kutangaza vivutio.”“Tuliona wale jamaa labda wamepotoshwa tu,” ameongeza.Hata hivyo, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi amekana kufahamu suala hilo ambalo CEO wa TMAA na mwanasheria wao wanajua na wamelitolea maelezo.Alimwelekeza mwandishi aende ofisini kwake Jumanne ili aangalie iwapo “kuna kitu kama hicho.”“Tangu ulipoanza kunitafuta nimekuwa vijijini mkoani Dodoma kikazi. Kwa sasa, na hivi tunavyoongea, nipo njiani kurudi Dar es Salaam. Ukinitafuta kesho (jana), labda naweza kukueleza zaidi…” amesema Maswi.Ofisa mmoja Hazina ameliambia gazeti hili, “Hata pale kwetu tuliishakumbana na kampuni kama hizi, zikilazimisha ushirikiano na ubia hata pasipowezekana.”Jitihada za kupata anwani na simu za ABC zimeshindikana, lakini ofisa mmoja wa TMAA ameahidi kulipa gazeti baruapepe ya kampuni hiyo.
  CHANZO:MWANAHALISI;Na Mwandishi wetu - Imechapwa 20 June 2012
   
 9. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Mkulu ni Dhaifu
   
 10. c

  commissioner Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duduwasha, hiyo avatar yako ni ya unyanyasaji wa watoto
   
 11. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Bora avatar yangu kuliko ya CCM wametuwekea Avatar Dhaifu... ambayo haiwezi kutimiza ahadi zake hadi leo....
   
Loading...