Technician
JF-Expert Member
- Mar 30, 2010
- 841
- 222
Ngeleja aibomoa kambi ya CHADEMA, Wenyeviti, Makatibu watimkia CCM
Mwenye taarifa kamili tafadhali atuhabarishe
Nimeipata hii kwenye Twiter.nadhani kuna ukweli ndani yake au unasemaje wewe.
Ni sawa tu... Hata wakina Shitambala waliondoka.....
Sidhani kama kuna jipya hapo...
Ila na sisi watz tuna njaa mbaya kweli of all the people Mtu kwenda kumuamini na kumuangukia Ngereja ni zaidi ya taahira na mpuuzi
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Mganga Ngeleja ameibomoa ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya viongozi wa chama hicho Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kurudisha kadi na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Miongoni mwa viongozi wa Chadema waliohamia CCM na kutambulishwa jana kwenye mkutano wa hadhara mjini Sengerema mkoani Mwanza ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Sengerema, Ayub Malima, Katibu wa chama hicho wilaya, Kesi Misalaba, Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema Sengerema, Sarah Mathayo na mwenyekiti wa Vijana wilaya Chadema, Stanslaus Pstory.
Viongozi wengine wa Chadema waliohamia CCM ni Katibu wa Vijana wilaya hiyo, Frenk Dotto, Lusia Mussa Mjumbe, pamoja na Sayi Busumabu mjumbe pamoja na mwanachama mmoja wa Chama cha Wananchi (CUF), Peress Essau ambaye mwaka 2005 aligombea ubunge jimbo hilo la Sengerema.
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Mganga Ngeleja (katikati), akimpongeza aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Ayub Malima, baada ya kiongozi huyo na wenzake saba kutangaza rasmi kuhamia CCM, kwenye mkutano wa hadhara mjini Sengerema. Kushoto ni mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Jaji Tasinga Gabanyaga
ENDELEA KUSOMA
Yote yametokea kwa sababu uongozi wa juu wa CDM unatumia ruzuku kumlipa posho ya mwezi Dr. Slaa badala ya kupeleka katika ofisi za mikoani na wilayani