Ngeleja aibomoa kambi ya CHADEMA, Wenyeviti, Makatibu watimkia CCM

Technician

JF-Expert Member
Mar 30, 2010
841
222
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Mganga Ngeleja ameibomoa ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya viongozi wa chama hicho Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kurudisha kadi na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Miongoni mwa viongozi wa Chadema waliohamia CCM na kutambulishwa jana kwenye mkutano wa hadhara mjini Sengerema mkoani Mwanza ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Sengerema, Ayub Malima, Katibu wa chama hicho wilaya, Kesi Misalaba, Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema Sengerema, Sarah Mathayo na mwenyekiti wa Vijana wilaya Chadema, Stanslaus Pstory.

ngeleja-chadema-cuf.jpg

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Mganga Ngeleja (katikati), akimpongeza aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Ayub Malima, baada ya kiongozi huyo na wenzake saba kutangaza rasmi kuhamia CCM, kwenye mkutano wa hadhara mjini Sengerema. Kushoto ni mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Jaji Tasinga Gabanyaga

Viongozi wengine wa Chadema waliohamia CCM ni Katibu wa Vijana wilaya hiyo, Frenk Dotto, Lusia Mussa Mjumbe, pamoja na Sayi Busumabu mjumbe pamoja na mwanachama mmoja wa Chama cha Wananchi (CUF), Peress Essau ambaye mwaka 2005 aligombea ubunge jimbo hilo la Sengerema.

ENDELEA KUSOMA
 
Sidhani kama Chadema ni saizi yake saizi yake ni mgawo wa million tano za Jairo
 
Jamani hizi ajali hazitaisha kama Waziri ndo anasababisha ajali itakuwaje? Je amebomoa ukuta au paa, bila shaka hiyo kambi itakuwa imeanguka, waliokuwemo humo ndani wamenusurika? yeye mwenyewe mbomoaji kanusurika kuangukiwa na matofali au paa.

Poleni wahanga................nasikia hapo hapo Ngeleja kafanywa mtaji wa kujenga kambi mpya na nasikia hii sasa itachukua watu wengi zaidi maana watu wamekasirishwa na yeye kuivunja hii ya sasa.
 
Kwa viwango vya habari hii sio habari kabisa...................nashangaa hata gazeti ambalo litaandika upuuzi kama huu. Ngeleja anatakiwa ajibu kwanini sehemu kibao hapa Dar hakuna umeme wakati mabwawa yote ''yametapika'' maji.

Habari kama hiyo inakuwa news pale mtu anapotoka CCM kwenda upinzani, and not the other way round, kwasababu hiyo imekuwa kawaida toka 1992, sio habari tena..........................
 
Ni sawa tu... Hata wakina Shitambala waliondoka.....

Sidhani kama kuna jipya hapo...

Ila na sisi watz tuna njaa mbaya kweli of all the people Mtu kwenda kumuamini na kumuangukia Ngereja ni zaidi ya taahira na mpuuzi
 
CDM poleni kwa kuanza mwaka vibaya! Hongera Ngereja kwa kuibomoa CDM wilayani kwako
 
Aah hainihusu mimi hii ngoja niende zangu niwaachie upupu wenu,kama zile za Ja hiro zimetumika vile!!
 
Ni sawa tu... Hata wakina Shitambala waliondoka.....
Sidhani kama kuna jipya hapo...
Ila na sisi watz tuna njaa mbaya kweli of all the people Mtu kwenda kumuamini na kumuangukia Ngereja ni zaidi ya taahira na mpuuzi

Nyani aoni kundule! Mtu akitoka vyama vya upinzani kwenda CCM mapesa yametumika; akitoka CCM kama Shibuda kwenda CDM chereko.
 
Kwani mlifikiri Shibuda ni specie ya peke yake hana ndugu? Otherwise ni pepo mchafu tu amewakumba. Hivi Ngeleja ana lipi la kumu-impress mtu mpk abadili msimamo?
 
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Mganga Ngeleja ameibomoa ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya viongozi wa chama hicho Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kurudisha kadi na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Miongoni mwa viongozi wa Chadema waliohamia CCM na kutambulishwa jana kwenye mkutano wa hadhara mjini Sengerema mkoani Mwanza ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Sengerema, Ayub Malima, Katibu wa chama hicho wilaya, Kesi Misalaba, Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema Sengerema, Sarah Mathayo na mwenyekiti wa Vijana wilaya Chadema, Stanslaus Pstory.

ngeleja-chadema-cuf.jpg

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Mganga Ngeleja (katikati), akimpongeza aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Ayub Malima, baada ya kiongozi huyo na wenzake saba kutangaza rasmi kuhamia CCM, kwenye mkutano wa hadhara mjini Sengerema. Kushoto ni mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Jaji Tasinga Gabanyaga

Viongozi wengine wa Chadema waliohamia CCM ni Katibu wa Vijana wilaya hiyo, Frenk Dotto, Lusia Mussa Mjumbe, pamoja na Sayi Busumabu mjumbe pamoja na mwanachama mmoja wa Chama cha Wananchi (CUF), Peress Essau ambaye mwaka 2005 aligombea ubunge jimbo hilo la Sengerema.

ENDELEA KUSOMA

Kuna kila sababu, Dr.Slaa aende Sengerema akafungue ofisi, kwani uongozi wote umesombwa na mafuriko ya Ngereja 2012
 
Ndio maana halisi ya demokrasia,mtu una ruhusa kujiunga na chama chochote cha siasa ili mradi hauvunji sheria,nawapa hongera hao waliohama na nawaambia tu kuwa uzuri wa walichokiona leo sio watakachokiona kesho
 
Nguo za CCM nzuri ila Ngeleja havai coz zina Laana na Hata Mwl Nyerere Hakuwa anavaa...Kuhusu kuhama ni kweli siamini kama ni utashi wao bali Msukumo wa Nguvu ya fedha
 
Wa ajabu kweli hawa vijana,yani wenzio wanaamka wao wanavuta shuka,wacha waende wakajifie huko
 
Hakuna shida watakuja wengine, lakini sidhani kama watu hawa wa sengerewa wanamfahamu ngeleja.
 
Chama ni itikadi, wananachama, viongozi na vikao. CHADEMA kama chama cha siasa kupoteza wanachama na viongozi wake ni pigo kubwa sana.!! Nawapa pole kwa kupoteza mvuto miongoni mwa viongozi na wanachama wake hadi kuamua kurudisha kadi na kukihama chama chao. Nawapongeza wanachama hao kwa uamuzi wao wa busara kuhamia Chama Cha Mapinduzi. KARIBUNI CCM TUIJENGE TANZANIA YETU.!!
 
Yote yametokea kwa sababu uongozi wa juu wa CDM unatumia ruzuku kumlipa posho ya mwezi Dr. Slaa badala ya kupeleka katika ofisi za mikoani na wilayani
 
Yote yametokea kwa sababu uongozi wa juu wa CDM unatumia ruzuku kumlipa posho ya mwezi Dr. Slaa badala ya kupeleka katika ofisi za mikoani na wilayani

Dhibitisha la sivyo hii post yako ni crap.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom