Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Klabu ya Simba imedai kuwa mchezaji Mrisho Halfan Ngassa bado ni mchezaji wao halali kwakuwa wana mkataba naye hadi mwisho wa msimu ujao. Hayo aliyasema Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba,Hanspope alipokuwa akihojiwa na Radio One jana. Hanspope alidai kuwa Ngassa alipelekwa Simba kwa mkopo akitokea Azam FC lakini baadaye alisaini mkataba wa hadi msimu wa 2013/2014. Ngassa tayari ameshatambulishwa rasmi kuwa amejiunga na Yanga. Yetu macho...
sio mpenzi wa simba lakini katika watu walio makini pale Hans Pope ni mmojawapo na hana uswahili mwingi kama tulivyo wengi wetu, anaweza akawa na point!
sio mpenzi wa simba lakini katika watu walio makini pale Hans Pope ni mmojawapo na hana uswahili mwingi kama tulivyo wengi wetu, anaweza akawa na point!
Tatizo wachezaji wetu wengi wa bongo hawana elimu ya kutosha hivyo kuna uwezekano mkubwa wa ku sign mikataba wasiyoielewa vizuri.
Alienda kwa mkopo afu akapewa mkataba duu,. Hii inatokea bongo tu
Wao hawana elimu ya kutosha lakini wewe uliyonayo umeshindwa kuitumia.......pathetic!
Kanuni za usajili zinasema kuwa mchezaji anakuwa huru kufanya makubaliano na klabu nyingine (tofauti na iliyomsajili) ndani ya miezi 6 ya mwisho ya mkataba wake. Hans Pope (Huyu jamaa anaitwa Zakaria) anadai Ngassa alisaini mkataba mwingine wa kumbakiza Simba kwa msimu 2013-2014. Swali la kujiuliza hapo, Ngasa angeweza vipi kusaini mkataba huo katika kipindi ambacho yeye (Ngasa) alikuwa mchezaji wa Azam bila ridhaa ya Azam?
Kabla hujawashambulia wachezaji na kuwaita wenye elimu ndogo, napenda nikukumbushe kuwa, wanaoongoza kwa kusaini mikataba wasiojua imeandikwa nini hapa Tanzania ni 'wasomi' na sio wachezaji wa Simba Koko na Yanga Africa.
Tuache kuwasakama wachezaji kwa kuwa tu hawakufanya yale tunayotaka sisi. Kama nchi inamsomesha mtu kiasi anaaminika kuwa mwanasheria mkuu wa serikali, halafu anatusainia mkataba wa madini wa miaka 100 kwa uwiano wa WAO 97%, SISI 3% na hatuna namna ya kuchunguza quantity, tuna haja gani ya kuwashikia bango wachezaji ambao hatukuwapa elimu wala mtaji?
Wakati Rage na huyo huyo 'Hans Pope' wanaingizwa mjini usajili wa Mbuyu Twite na wao walikuwa hawana elimu? Si walikuwa na makelele kama haya haya mpaka tukaambiwa kwamba Mbuyu Twite hatacheza na akachukuliwa RB, sasa kuna lipi jipya hapa la kuanza kumshutumu Ngasa hakusoma? Hawa wasomi si ndio hawa wanaandaa bajeti ya 1bn kwa makaburi huku wengine wanakunywa maji machafu kwa kukosa 8m za kununua pump ya kisima cha kijiji?
Alienda kwa mkopo afu akapewa mkataba duu,. Hii inatokea bongo tu
Unamjua ANDY CARROLL na sula zima la "kucheza kwa mkopo" ?
Andy Carroll - West Ham agree £15million fee with Liverpool to sign striker | Mail Online
Angalia usikurupuke kufananisha scenario mbili tofauti. And Carrol ni mchezaji wa Liverpool anayechezea West Ham kwa mkopo.
Hans Pope ni Mwenyeketi wa kamati ya usajili ya Simba ambayo imefanya usajili wa wachezaji wabovu kamasio mpenzi wa simba lakini katika watu walio makini pale Hans Pope ni mmojawapo na hana uswahili mwingi kama tulivyo wengi wetu, anaweza akawa na point!
Hii habari ya Caroll ni tofauti na Ngasa kumbuka Caroll ameshamaliza mkopo wake West Ham but still WH wanataka wamsajili moja kwa moja ndio maana wako tayari kutoa hilo dau.Mkopo wa Ngasa Simba umeisha mwezi huu 5 so hiki ndio kipindi ambacho Simba walipaswa kusaini mkataba na NgassaUnamjua ANDY CARROLL na sula zima la "kucheza kwa mkopo" ?
Andy Carroll - West Ham agree £15million fee with Liverpool to sign striker | Mail Online