Ngasa alizwa na deni

Ngasa alizwa na deni

Kwameh

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Posts
1,793
Reaction score
2,162
Ngasa alikopa kuilipa Simba!

21/01/2014 Posted by Clezencia Tryphone

ngasa_6.jpg


WANACHAMA wa klabu ya Yanga wameuomba uongozi wao wamchangie kulipa deni mshambuliaji wao, Mrisho Ngasa, baada ya kukopa katika moja ya benki hapa nchini kuwalipa Simba.

Ngasa alikopa sh milioni 45 katika moja ya benki ambayo haikutajwa jina, kwa ajili ya kulipa deni la Simba, baada ya kugundulika kumwaga wino sehemu mbili na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumfungia mechi sita na kutakiwa kulipa fedha hizo.

“Jamani ni fedheha kwa klabu kubwa kama Yanga kuona wachezaji wetu wanaadhirika, maana Ngasa mpaka sasa anadaiwa fedha na benki.....

--------------------------------------------------------------------------------------------------

Soka hailipi. Kama mchezaji nyota kuliko wote Tanzania anashindwa kulipa milioni 40, ambazo wakina Diamond wanazitengeneza kwa show mbili tatu kwa mwezi basi soka bora ifutwe vijana waka focus na vipaji vingine au wakomae na shule tu.
 
sijaona popote Ngassa akisema anadaiwa, hap wanachama taarifa wamezitoa wapi? au Benki ndiyo imetoa hizo taarifa, mbona mwenyewe alipoenda kulipa alisema zimetoka mfukoni mwake (any way inaweza kumaanisha alikopa kwa collateral zake) but the key point ni mdaiwa kujitokeza mwenyewe na kuomba kusaidiwa (if at all)

ama badu hivi kumsaidia mtu ni mpaka uombe mahali? kwani uongozi unahusikaje na hilo deni?
 
huyu mtoto pimbi sana ..si alikuwa anajidai ana mamilioni huyu wakati anawalipa Simba au?mxxxxxxx
 
Unataarifa mpya hadi muhusika hazijui aisee kweli wewe ni noumer , hebu tusaidie kukujua wewe ni nani kwake au shemeg wetu nini?don mind it joh..
 
Unataarifa mpya hadi muhusika hazijui aisee kweli wewe ni noumer , hebu tusaidie kukujua wewe ni nani kwake au shemeg wetu nini?don mind it joh..

Ngoja nimsaidie.Hii iliwekwa wazi siku ya mkutano wa yanga wa tarehe 19 kuwa hilo deni ni lake na anakatwa kila mwezi na bank ya CRDB.
 
Halafu waache ujinga hao.. Hiyo hela Ngassa aliopewa na Simba aliitumia kwa matumizi yake binafsi leo kwanini watoke watu baki wamchangie kulilipa deni wakati yeye ni professional anaelipwa mshahara na Yanga..? Huu sio mpira wa ridhaa so wamuachie mwenyewe alilipe deni lake lol..
 
taarifa rasmi ni kwamba Okwi kazuiwa kuchezea yanga paka amalizane na club yake kwanza, kwa hiyo msimu huu hauhusiwi kucheza kabisa
 
Back
Top Bottom