Ngano ni nafaka hatari sana

Angalia headline ya habari yako.Imefanya ulichoandika kikose ukweli.Huwezi kufa kwa kula vinavyotokana na ngano.Ukiwa na gluten intolerance haifanyi ngano iwe "nafaka hatari sana".
 
Kuna mahali pia nilisikia kuwa mahindi nayo ni hatari sana kwa afya..!!! Tushike lipi tuache lipi
 
Angalia headline ya habari yako.Imefanya ulichoandika kikose ukweli.Huwezi kufa kwa kula vinavyotokana na ngano.Ukiwa na gluten intolerance haifanyi ngano iwe "nafaka hatari sana".
katika nafaka, ngano ni nafaka hatari sana. Ikiwemo na wenzake kama shayiri. Si lazima iue
 
Mikate ya mahindi ipoje??, juu ya yote unga wa sembe siku hizi unatiwa virutubisho (fortification chemicals), sina hakika kama hizo fortifications zina usalama gani!!.
Inaokwa kawaida tu kwa kutumia unga wa dona. Lakini hawatumii hamira, wanatumia tu baking powder.
 
Ah ukiwasikuliza Sana wataalamu utaishi maisha ya shida Sana mda huohuo ukiyaita ya kisasa! Sasa tusitumie ngano tule Nini Sasa?
Juzi Kati BBC walileta list ya vyakula vya kutopendelewa eti ndizi, asali nk.
Nb.
Kila chakula wanakiwekea pingamizi ya matumizi yake.
Babangu kazaliwa mwaka 1930. Kwa miaka yote hi ameishi akila wanga na ngano uisemayo. Na Tena anapenda chai maandazi ile mbaya.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Ngano ni nafaka hatari sana na watz wengi hatufahamu. Tofauti na nafaka zingine kama mahindi, ulezi, mtama na mchele, ngano ina aina fulani ya protin inayoitwa Gluten. Protin hii ndiyo hufanya ngano ikikandwa iwe kama banzoka wakati ukikanda unga wa mahindi hauwi namna ile.

Sasa hii protin inaweza kusababisha mzio(allergy/autoimmune reaction) ya hatari sana. Kifupi inaweza sababisha mwili ujishambulie. Maeneo yanayoathirika zaidi ni utumbo mdogo. Hili linaweza sababisha kuharisha bila kukoma, tumbo kujaa gesi, udumavu na afya dhaifu.

Pia inaweza athiri ngozi na mtu kutoka mapele ya kuwasha kama mwenye ugonjwa mkali wa ngozi.

Pia inaweza sababisha matatizo kwenye ubongo na kusababisha mtu atembee kama aliyelewa.

Inasemwa kuwa matatizo haya hutokea hadi kwa asilimia 2 ya watu wote.
Ni vyema tukatumia mikate ya mahindi, ulezi nk. Ngano ni hatari sana.
Kwa hii life ya ki TZ ngano ni pagumu mtu kukuelewa athari maana ndiyo mlo mkuu
 
Back
Top Bottom