Maambukizo ya VVU na ugonjwa wa UKIMWI

Kwekitui

JF-Expert Member
Oct 29, 2017
1,070
1,078
VVU huathiri sehemu nyingi za mwili wa mtu. Vinaweza kufanya hivyo kwa
njia mbili. Njia ya kwanza ni kwa kushambulia moja kwa moja viungo mbali

mbali, njia nyingine ni kwa kudhoofisha mfumo wa kinga na kuruhusu viini
au vimelea vinavyosababisha magonjwa mengine kuingia mwilini. Katika sura

hii, tutaelezea uharibifu wa aina ya kwanza ambao VVU husababisha, katika
nyongeza tutajadili aina ya pili ya uharibifu unaofanywa na VVU.

VVU hushambulia seli za ubongo wa mtu. Hii inaathiri uwezo wa mtu
kufikiri (kwa sababu ya uharibifu uliopo kwenye ubongo). Husababisha maumivu
na ganzi katika mikono na miguu (kwa sababu ya uharibifu wa mishipa

ya fahamu (neva). Husababisha kuharisha (uharibifu ulio tumboni) husababisha
upungufu wa damu na kuvuja kwa damu (husababishwa na uharibifu

unaotokea kwenye damu). Ingawaje VVU, vinasababisha mtu augue, tunafahamu
sio kila mtu, mwenye VVU ni mgonjwa. Ndiyo sababu kuna hatua, za

mtu alieambukizwa anapitia, kuanzia mtu anapoambukizwa na VVU, kipindi
ambacho aliyeambukizwa haonyeshi dalili zozote, hufikia hatua ya alieambukizwa
huanza kuonyesha dalili za mwanzo, na hatimaye UKIMWI.

N i n i d a l i l i z a a l i y e a m b u k i z w a n a V V U ?

Hatua nne za maambukizo ya VVU

1. Wiki chache baada ya kuambukizwa, watu huwa na dalili kama homa ya mafua.

2. Kipindi cha utulivu, wakati kuna dalili chache za UKIMWI.

3. Dalili za awali za UKIMWI.

4. UKIMWI, mwathirika huwa mahututi sana.
Huchukua muda toka kipindi kimoja hadi kingine.

Wiki za mwanzo baada ya maambukizo

Baada ya kuambukizwa VVU, kwa kawaida watu hawawezi kutambua
kwamba wameshaambukizwa VVU; hawawezi kujua kwamba wana VVU
mpaka baadae wanapokwenda kupima au wanapokuwa wagonjwa. Hata

hivyo watu wachache, huanza kuona dalili kuanzia wiki 1-4 baada ya maambukizo
ya virusi. Dalili zinazofanana
na mafua, maumivu ya
koo, homa, maumivu ya kichwa,

maumivu ya tumbo, kuharisha
na kujisikia kuchoka. Baada ya
wiki, vipele vinaweza kutokea

kwenye kifua, uso na shingo. Watu
wanaweza wakatokwa na jasho
usiku, maumivu ya misuli na

viungo, uvimbe wa tezi, kichefu
chefu na kutapika. Dalili hizi
kwa kawaida hudumu kwa muda
mfupi, sio zaidi ya wiki mbili.

Ni nadra kwa hatua ya kwanza
baada ya maambukizo ya VVU
kuwa mbaya sana na kuharibu
mfumo wa neva wa mtu. Mtu

aliyeambukizwa anaweza akawa
na uvimbe kwenye ubongo na
ngozi inayoufunika. Hii inaweza

kusababisha maumivu ya kichwa,
kugangamaa kwa shingo, homa,
kuchanganyikiwa, matatizo ya
mfumo wa neva na kupoteza

fahamu. Mtu anaweza kuwa na
matatizo ya neva kwenye mikono
na miguu na matatizo ya neva za

usoni. Hii inaweza kusababisha
maumivu ya ngozi na shida ya
kutembea, tezi wakati mwingine
huvimba na hubakia zimevimba
kwa miezi au miaka.

Kwa vile dalili hizi huonekana pia kwenye maradhi mengine mbali na
VVU, hatuwezi kusema kuwa kila mwenye dalili zinazofanana na hizi nchini
kwamba ana VVU. Ili mtu afahamu ana maambukizo ya VVU anahitaji

Mitoki
Mitoki mara nyingi huitwa “tezi”,
ni kiini cha mfumo wa kinga ya
mtuo. Huwa zina vimba na kuuma
zinapo kabiliana kuondoa viini vya

maradhi. Mfano, mitoki ya shingoni
huvimba mtu anapopata maambukizo
katika koo. VVU husababisha
kuvimba kwa tezi, wakati mwingine
mwili mzima, wakati mwingine kwa
muda wa miaka.

kupima damu. Hata hivyo, kipimo cha kuchunguza VVU, wiki chache baada
ya maambukizo hakiwezi kutoa matokeo ya uhakika. Sababu ni kwamba
kipimo, huangalia kama mtu ana askari dhidi ya VVU (antibodi). Kama ndio

mwanzo tu wa maambukizo ya VVU na mwili wako bado haujatengeneza
askari dhidi ya VVU, kipimo hakiwezi kuonyesha kama mtu ameambukizwa
au la. Watu wengi miili yao huanza kuonyesha kama ina askari dhidi ya

VVU wiki nne baada ya maambukizo. Mtu yo yote anayedhani kwamba
inawezekana ameshaambukizwa na VVU anaweza kupima kwanza na kurudia
baadaye (soma zaidi juu ya kipimo cha VVU sura ya 7 na 8).
Kipindi cha ukimya baada ya maambukizo ya VVU

Siku chache baada ya dalili za
mwanzo zinazoambatana na
maambukizo ya VVU hutoweka na

mgonjwa hujisikia nafuu. Kwa miaka
kadhaa baadaye hujisikia vizuri,
huonekana mwenye afya na kuendela

na maisha ya kila siku. Mfumo wa
kinga unauwezo wa kukabiliana na

virusi kipindi hicho chote na huitwa
kipindi cha ukimya. Ni kipindi
kuanzia maambukizo hadi dalili

za mwanzo za ugonjwa wa UKIMWI. Kwa watu wazima, kipindi hiki huwa
miaka 10 kwa wastani. Kwa sasa watu wengi wenye VVU wako katika kipindi
hiki (cha ukimya). Hawasikii dalili yeyote na wengi hawajui kama wameshaambukizwa
na virusi na wanaweza kuambukiza.

Ugonjwa wa UKIMWI unavyoanza

Baada ya kipindi cha maambukizo, watu wenye VVU huanza kuugua, VVU

hudhoofisha mifumo yao ya kinga, kiasi ambacho uwezo wao ambao kwa
kawaida mfumo wa kinga unaokabiliana na viini hutoweka na kuruhusu
magonjwa mengine, magonjwa hayo huitwa "magonjwa nyemelezi"- na baadhi

ya kansa, ni dalili ya moja kwa moja ya UKIMWI. Tutajadili tiba zake
katika nyongeza. Wakati mfumo wa kinga unadhoofika, watu wenye VVU

Kundi la lishe bora

Protini – Husaidia mwili kukua na kuponya. Vyakula vyenye protini vingi, , ni
samaki na aina nyingine ya vyakula toka baharini, Nyama, mfano, ya ngombe, ya
kondoo na mbuzi. Nyama za kuku, bata, bata mzinga, mayai, maziwa, jibini, jamii
ya kunde, mchele, mbaazi, mchicha mweusi, nafaka, jamii ya karanga, tofu na vitu
vitokanavyo na soya, njegere.

Wanga – ni vyakula vya kutia nguvu mwili. Wanga upo kweye nafaka, mchele,
ngano, mtama, ulezi, uwele, viazi na muhogo.

Vyakula vya kutia joto na nguvu mwilini - husaidia mwili kuweka akiba ya
chakula cha kuupa mwili nguvu. Kuna nguvu mara mbili zaidi kama ilivyo kwenye
protini na vyakula vya kuupa mwili nguvu. Hii ina maana, ulaji wa mafuta husababisha
ongezeko la uzito kwa watu. Ladha nzuri, shida au tatizo la mafuta husabibisha

ugonjwa wa moyo kwa watu na ongezeko la uzito. Kwa watu walio athirika na

VVU hili siyo tatizo lao kwa kawaida kwa sababu, wao wanajitahidi waongezeke
uzito. Vyakula vyenye mafuta ya mgando na ya maji maji ni– siagi, karanga ufuta,
soya, nazi, (embe mafuta) parachichi, krimu, maziwa, nyama nyekundu kama ya
ngombe, nguruwe na kondoo.

Vyakula vya kulinda mwili – ni muhimu sana, mwili huhitaji kiasi kidogo kwa
afya ya mtu, hupatikana kwenye vyakula vya aina nyingi tofauti, ndio maana
vyakula tofauti katika mlo ni muhimu kwa afya ya binadamu, hutoa aina tofauti
(mbali mbali) ya vitamini na madini.

VVU, kupungua uzito na utapiamlo
Watu wengi huishi katika jumuia ambazo zina upungufu wa chakula na tatizo

la utapia mlo. Watu hawahitaji chakula cha kutosha tu, bali pia wanahitaji
aina mbalimbali ya vyakula, mfano, anayetumia muhogo kama chakula na
habadilishi, atadhoofika. Kama mtu anaweza kuwa mgonjwa kwa kutokula

chakula cha kutosha na sahihi, ana ugonjwa wa utapiamlo. Utapiamlo
unaweza kusababisha magonjwa na kupungua uzito. Njia mojawapo ya kudumisha
afya mzuri ni kula chakula bora. Huu ni ukweli hasa kwa wenye VVU

na UKIMWI. Wana uwezekanao wa kuwa na utapiamlo kutokana na kuugua
mfulululizo, kuharisha kunakosababisha mwili usipate lishe iliyopo kwenye

chakula, kupoteza hamu ya kula na vidonda mdomoni husababisha kula kwa
shida. Kupungua uzito ni kawaida kwa wenye VVU, kiasi kwamba baadhi ya
sehemu ya Bara la Afrika ugonjwa wa UKIMWI huitwa "slim".

Kama mtu yeyote ana shida wakati wa kula

Walioathirika na VVU wanaweza kuwa
na kichefu chefu na kutapika. Chai

au dawa yaweza kusaidia. Mwenye
vidonda mdomoni vyakula baridi na
visivyo na viungo hufanya maumivu
kupungua wakati wa kula. Watu wenye

kumeza kwa shida, kusogeza kichwa
mbele, na kula vyakula laini, husaidia
kumeza kwa urahisi. Uangalifu uzingatiwe

wakati wa kunywa ili kuepuka
kupaliwa. Utumiaji mrija wakati wa
kunywa kunaweza kukasaidia wakati
mwingine. Shida ya kula au kunywa

huenda ikawa ni kwa sababu ya ugonjwa ambao waweza kutibika, mfano ukungu
mdomoni; katika hali hii waeleze watu wakamuone mhudumu wa afya.

Kula vyakula bora vya aina mbali mbali; husaidia wenye VVU kuwa na
nguvu na afya. Chakula bora ni mlo mmoja wenye mchanganyiko wa vyakula
vyenye lishe mbali mbali muhimu. Lishe muhimu ni protini, wanga, mafuta
yaliyoganda na ya maji, vitamini na madini.

Wanawake na watoto wanahitaji lishe bora. Kwa sababu wanawake
hupoteza lishe nyingi wakiwa kwenye hedhi, ujauzito na wakati wa kunyonyesha.

Watoto huhitaji chakula cha ziada kwa sababu wanakua haraka. Watoto
wenye VVU huhitaji chakula zaidi ili wawe na afya nzuri, VVU huongeza
mahitaji ya chakula mwilini mwao.
 
Unapocheki miez 10 au 12 hivi baada ya kutembea labda na + na hujakutwa na HiV Kuna uwezekano tena hapo ikiwa hujapata emergency nyengine inayopelekea hii kitu?
 
Back
Top Bottom