Ngano na visasili

Ngano na visasili

Joined
Nov 20, 2016
Posts
23
Reaction score
14
“JUMBA LA AJABU”
************************
_______Hadithi za ngano na visasili zina umuhimu mkubwa kwa jamii, zinatoa maaso, maonyo na ujumbe. Aidha, hadithi zinakuza akili za watoto na kuwafanya wawe na tafakuri kubwa. Hapa mimi nita-andika hadithi ya Jumba la ajabu niliyohadithiwa na baba yangu nilipokua mdogo.

_______Nakumbuka ilikua ni kipindi cha mavuno ya karafuu mwaka wa 2002, tukichambua karafuu nyumbani kwetu. Nikiwepo mimi, mama, baba na mjukuu wao dada Hawaa. Baba alianza ufunguzi wa hadithi yake kwa kusema “Hadithi, hadithi” mimi na Hawaa tukaitika. “Hadithi njoo, ukweli njoo utamu kolea” Baba akaendelea.... Hapo zamani kulikua na Jumba la ajabu, jumba hilo lilikua na kuta sita, ni tofauti na nyumba nyengine abazo zinakua na kuta nne. Ndani ya jumba hilo kulikua na vituko vya ajabu ambavyo kikawaida haviko katika nyumba nyengine. Kituko kimoja ni kua, mama wa jumba hilo alikua anaolewa na kuachwa na waume tofauti. Kila mume aliemuowa mama huyo alikua ana vitimbi vyake.

_______ Kituko cha pili ni kwenye ubadilishwaji wa hao waume. Waume walikua wakigombewa. Waume wawili wenye nguvu walikua wanajitokeza kumposa mama kila mama huyo alipohitaji kubadilisha mume, huku watoto wa mama huyo wakiwa ni waamuzi, mama yao aolewe na nani.

_______ Kituko cha tatu ni kuwa, hao watoto wenye maamuzi ya kuchagua baba wa familia, kupata maonevu pindi wanapofanya hivyo. Ama kweli “fahali wapiganapo, nyasi ndio huonewa” baba alisema huku akionyesha kukunja sura alipokua akiendelea na hadithi yake.

_______ Waume walio-muowa mama wa jumba la ajabu ni pamoja na bwana Vita, bwana Ruhusa na Chamoto. Hali ya uchumi katika kila nyumba hubadilika. Hivyo jumba la ajabu lilikua hivyo pia. Mara nyengine wanafamilia walipata shibe na mara nyengine walikosa milo mitatu.

______ Kipindi mama wa watoto alipokua na bwana Vita iliwahi tokea njaa. Watoto walikosa milo mitatu. Bwana huyu alikua mkali lakini, hakusita kuenda kwa jirani yake kujiombea ugali, ijapokua jirani huyo alim-gaiya ugali kwa masharti magumu. Baadae aliona hali ni ngumu, hivyo alimua kumuacha mke wake. Hapo sasa mke huyo aliolewa na bwana Ruhusa. Na kwa bwana huyu pia, nyumba hali ikawa bado ni mbaya. Nae alienda kwa jirani yake mwenye nacho amsaidie. Nae alipewa misaada ya kjisukuma mbele. Misaada haya yalikua na masharti makubwa zaidi.

________Bwana Ruhusa alikubali hivyo hivyo. Jirani wa bwana Ruhusa alitambua kua, Jumba la ajabu linaongozwa na waume wazembe. Hivyo jirani huyo akamuambia bwana Ruhusa, "ili nikusaidie vizuri basi niruhusu nije nifanye shughli zangu nyumbani kwako" Nae akasema “Ruhsa” jirani alifurahi maana, alijua kuna mengi yatakayomnufaisha ikiwemo “kula tamu ya mama huyo”

________ Mengi yalipita na hatimae mama watoto aliolewa na Chamoto. Kwa bwana huyu ilikua pata shika nguo chanika. Aliwataka wana wafanye kazi, waache maneno ya kusema wana njaa. Na hivyo, hakunyanyua mguu wake na kuenda kuomba ugali kama walivyofanya bwana vita na bwana Ruhsa. Aliona njia pekee ni kubana matumizi kwa familia yake na kusisitiza kazi.
 
Back
Top Bottom