Neymar/Brazil 3 - Messi/Argentina 0

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Usiku wa leo umechezwa mchezo wa kuwania kufuzu kwa kombe la dunia kati ya wababe wawili wa Amerika Ya Kusini(South America derby),Brazil vs Argentina

Brazil wakiwa nyumbani wamefanikiwa kuwatandika bila huruma timu ya Argentina iliyokuwa imesheheni wakali wake wote kama vile Messi,Di Maria,Aguero,Higuan,Otamendi,Marcherano,Bilgia...nk Jumla ya magoli Matatu kwa Sifuri

Brazil wakipiga Soka la Kitabuni lenye Ufundi mkubwa aka Samba walianza kufunga magoli yao kupitia kwa Coutihno,Neymar na Paulihno akifunga la mwisho.

Chini ya kocha wao mzawa Tite Ukuta wa Brazil ukiongozwa na Miranda,Marquinos,Alves na Marcello uliwadhibiti washambuliaji wa Argentina na kuhakikisha Nyavu zao hazigushwi huku golini akisimama Allison.

Ulikua mchezo mzuri sana mpira ulianza saa nane na dk 45 saa za Tanzania,Naiona ile Brazil ya Akina Cafu,Lucio,Robert Carlos,Dida/Claudio Tafareli,De lima ikirudi kwa Kasi.

Hongereni Samba Boys/Brazil kwa ushindi wenu mnono.
 
Brazili wamerudi Mahala pao, kwa sasa hawajafungwa mechi hata moja tangu Timu ichukuliwe na kocha mpya, Jamaa wanaanza kurudi waliko kuwaga.
 
contihooooo katika ubora wake huyu jamaa ndani ya sita hafungi goli lakini nje ya kumi na nane ni hatari hapana chezea
 
contihooooo katika ubora wake huyu jamaa ndani ya sita hafungi goli lakini nje ya kumi na nane ni hatari hapana chezea
Jamaa ana nguvu za miguu sana goli la jana pia ni nje ya penati box
 
Brazili wamerudi Mahala pao, kwa sasa hawajafungwa mechi hata moja tangu Timu ichukuliwe na kocha mpya, Jamaa wanaanza kurudi waliko kuwaga.
Tatizo ilikua selection ya Timu na upangaji wa Timu

Uyo Miranda anakaba mpaka kivuli
 
Back
Top Bottom