Final Copa America, Brazil against Peru, mechi yao ya kwanza mashindano haya Brazil 5- Peru 0, Je Peru kapenyaje?

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
BRAZIL wametinga Finali baada ya kumfunga Argentina magoli 2 Kwa 0,
Brazili kwenye mechi waliyokutana na Peru mashindano haya haya walimcharaza Peru 5 kwa Mtungi,
Najiuliza je Peru kapenyaje kwa Chile mabingwa mara 2 mfululizo wa Kombe hilo?

Je fainali inawezekana Brazili akapoteza licha ya kumuaibisha Peru hapo mapema mabao 5 kwa mtungi?

TUJUE MAMBO MUHIMU SANA
2019 Copa Aemrica Brazil wanaonekana kuwa vizuri na kuwa katika nafasi nzur ya kuutwaa ubingwa huo, Mtanange uo utapigwa jumapili katika uwanja wa Marakana wabrazili wanauita (ELIMARAKANAZO),
Tunategemea kuona samba safi sana kuwahi kutokea katika kipindi cha hivi karibuni,
Brazili ilitinga fainali baada ya kuibamiza Argentina na Messi wao magoli mawili bila majibu, wakati huo Peru ikimfunga magoli matatu kwa mshangao bingwa mara mbili mfululizo wa mashindano hayo Chile kwa mwaka 2015 na 2016,
Hizi timu mbili zimekutana katika hatua ya makundi yaan Brazili na Peru na vikosi vile vile ambavyo vilipelekea Peru kupoteza mchezo huo mbele ya Brazil kwa Magoli 5 bila majibu



Brazil imekuwa inafanya vizuri hata bila ya kuwa na Neymar
Imewachukua muda kidogo kuwafanya mambo yao yaende sawa sawa lakin wameweza kufanikisha hili, Tumeona mpira safi sana ambao umepigwa na Brazili bila mchezaji wao tegemezi huyu, ila uwepo wa Roberto Firimino na Gabriel Jesus umesaidana na uwezo wa Coutinho na beki Daniel Alves ambaye amefanikisha ulinzi wa hali ya juu katika safu ya Ulinzi ambako mpaka sasa Brazil hajafungwa goli lolote lile tokea mashindano yameanza,

hii inaweza kuwakumbusha furaha yao ya mwaka 2007 walipowin kombe hilo,

Tukutane Jumapili 23:00

Britanicca
 
Mpira ni mchezo wa makosa, inategemea ni nani atanufaik na makosa ya nani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom