Kwa hili, Messi na Mashabiki wako mnatudanganya sana

Nabii kibonge

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
268
500
Hivi ndivyo ilivyo inapita miaka mingi, yanatokea mabadiliko mengi lakini mpira ni ule ule, either ushindi au lose bado ni vile vile. Na muhimu zaidi ni kila zama na watu wake na katika zama hizi ni ukweli kabisa soka limetawaliwa na miamba kama kina Lionel Messi.

Ni kawaida kuwasikia mashabiki wakisifia vilivyo kipaji cha gwiji wa soka toka Argentina wengine wakidiriki kumwita G.O.A.T kwa maana kwamba Greatest of All The Time. Kimakonde tuseme mchezaji bora wa mpira wa miguu kuwahi kutokea.

Yawezekana Messi atakuwa anastahili kuitwa G.O.A.T kutokana na mitazamo mbalimbali lakini katika pita pita zangu nilijaribu kurejea baadhi ya mambo kama ifuatavyo

Binafsi mimi ni muumini wa real perfomance na impact ya mchezaji akiwa on the pitch na sio muumin mkubwa wa tuzo mbalimbali za kupima ubora wa wachezaji ikiwemo ballon d or. Japokuwa ni kweli ballon d or inatokana na perfomance ya mchezaji hivyo vinahusiana lakini ni swala lililo wazi kuhusu dought mbali mbali za ugawaji wa tuzo hizo (mfano Shevchenko 2004, Ronaldo 2013 , Messi 2010 na 2012 niishie hapo kwa leo)

1. Takwimu za messi katika campaigns za La liga 2019/2020. Messi amemaliza akiwa na magoli 25 na assist 21, kiukweli ni perfomance ya hali ya juu lakini ukichunguza kiundani utajua how stats can fool you.

Katika magoli 25 ya messi, magoli 20 amezifunga timu zilizo chini ya nafasi ya 10 (11-20) hii ni 80% ya magoli yake yote

Katika magoli yake 5 hayo aliyozifunga timu( Atletico madrid(2), sevila ,Granada ,Sociedad, kubwa ni mawili tu (2) aliyofunga open space huku hayo mengine ni kupitia set pieces (penalties 2 zikiwemo ( atletico na sociedad))

Ni ukweli usiopingika katika msimu huu messi kafunga magoli yaliyoweza kuamua mchezo( game wining goals) jumla ya 6. Wakati huo huo Neymar miguu ya glasi anatakwimu kubwa zaidi ya hiyo (7) Lewandowski 12, Ronaldo 10.

Messi amemaliza na jumla ya assist 21 huku assist 4 zimetokana na freeckicks, 5 ni back pasees ( jumla ya open space assist ni 15) huku akiwa na avarage ya key passes 2.7 per game.Ni kweli messi ni player maker mkubwa lakini kaachwa mbali na playermakers kama KDB (3.9) Luiz Alberto (3.0) Thomas Muller na wengine wengi

Achana na hilo tuhamie UEFA, katika msimu huu wa 2019/2020 huku ukiwa unaelekea mwaka wa 5 bila ya barcelona kutwaa kombe hilo pia ndani ya miaka 9 barcelona wikiwa wametwaa mara moja tofauti na ilivyokuwa miaka 10 ya nyuma kwani wametwaa taji hilo mara 3. Pia ni wazi ubingwa wa 2015 kila mmoja anaefuatilia soka anajua mchango wa neymar.

Lionel messi katiga group stage ana jumla ya magoli 68 katika mechi 72. Na katika level ya knock out hadi fainali ana jumla ya magoli 46 katika mechi 69 Ni ukweli usiopingika tumeshuhudia Messi akishindwa kuinusuru timu yake dhidi ya As Roma (2018/2019) Liverpool (2017/2018) pia Juventus (2016/2017)na Atletico Madrid

Swali langu je Lionel messi ni mchezaji wa Timu ndogo tu??( Anaonesha ubora wake akiwa anacheza na timu ndogo tu na katika mashindano madogo ikiwemo ligi na sio UEFA au World Cup)

Ni wazi kila mtu anajua jinsi Pele na Maradona walivoonesha ubora wao bila kujali timu walizokuwa nazo

Pele akiiongoza timu yake ya brazil 1958 kuchukua kombe la dunia. Timu ambayo ilishindwa kufanya vema 1950 na hata 1954 dhidi ya Hungary huku wakiwemo wachezaji mahiri kama Zitto pia Nilton Santos lakini ingizo jipya la Pele mwaka 1958 ndio lililofungua mwanga kwa brazil kwani katika nusu fainali pele akiwa na umri wa miaka 17 aliweza kupiga hattrick dhidi ya Ufaransa na katika kumchabanga sweden Goli 5-2 pele alifunga goli 2 na assist juu ( shukrani kwa mario zagallo na vava kwa magoli ya ushindi) ni wazi tumeona pele wa miaka 17 alikuwa chachu ya ushindi wa brazil(kombe la dunia) na pia si mchezaji wa timu ndogo

1986 Nani asiyejua mchango wa diego maradona. Katika Argentina ya 1986 unamjua nani zaidi ya maradoan. Buruchuga??? Ni wazi bao 2 za maradona dhidi ya waingereza ni chukizo la mda wote kwa waingereza.Achana na mafanikio ya maradona timu ya taifa.

Ni Maradona huyu huyu aliehama toka barcelona na kwenda Club ya Napoli ambayo haikuwa na taji lolote na ilikuwa kwenye hali mbaya ( usifananishe na Ronaldo kwenda Juventus) huku akichangia kiasi cha pesa yake mfukoni kukamilisha usajili huo. Maaajabu ni kwamba baada ya ujio wa maradona Club hio ilitwaa mataji yafuatayo

- UEFA CUP 1989
- SERIE A 1987, 1990
-Coppa Italia 1987
-SUPER COPA ITALIANA 1990

Napoli haikuwahi kushinda Serie A kabla, Napoli haikuwahi kushinda Uefa cup kabla na hadi sasa hawajawahi kushinda toka diego Maradona aondoke( hicho ni kipimo cha jinsi club hiyo ilivyokuwa ndogo). Pia Maradona aliondoka Club hio akishikilia rekod ya mfunganji bora wa mda wote iliyokujwa kuvunjwa juzi juzi hapa (2015-)

Je Messi anaweza kwenda club ndogo isiyofahamika na kufanya makubwa yote hayo? Anaweza kwenda Newcastle united na mambo yakawa hivyo hivyo???

Mwisho mashabiki wa messi kama kawaida yao watakimbilia kwenye ubora wa kupiga faulo wakijisahaulisha kuwa messi hata kwa Ronaldo hajamfkia Je tutamfananisha na Juninho Penambucano????? Kamuulize Oliver khan na bayern yake au Barcelona wanamjua vizuri

Kuhusu national team sina ya kuongea maana hamna kingino zaidi ya buyu(0) kwa international trophies

Je messi ni mchezaji wa mechi ndogo( anaonesha perfomance kwenye timu ndogo au mashindano madogo tu?)

Je messi anastahili kuitwa G.O.A.T????
 
Hadrianus

JF-Expert Member
Feb 19, 2020
437
1,000
1. Takwimu za messi katika campaigns za La liga 2019/2020
Messi amemaliza akiwa na magoli 25 na assist 21, kiukweli ni perfomance ya hali ya juu lakini ukichunguza kiundani utajua how stats can fool you.

Katika magoli 25 ya messi, magoli 20 amezifunga timu zilizo chini ya nafasi ya 10 (11-20) hii ni 80% ya magoli yake yote

KWAHIYO HIZO TIMU ZA CHINI ULITAKA AFUNGE NANI?
 
So case kufunga lakini tunapopima compitence ya mchezaji lazima tuconsider pia uwezo wa kufunga mechi kubwa sio ndogo peke yake
 
Nabii kibonge

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
268
500
Kwamba Messi ni mzigo? Huu uzi mzima umeuleta kumjadili mtu wa miaka 33? Haya hebu lete uchambuzi wako juu ya magoli 90 aliyofunga ule msimu.
Sio mzigo ila shida ni kwamba kuna baadhi ya mambo jamaa anakuwa overatted na hilo utakundua ukifanya analysis lakini kuhusu goli 91 ni kweli hiyo ni great perfomance
 
Kigoma Independent

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
1,825
2,000
1. Takwimu za messi katika campaigns za La liga 2019/2020
Messi amemaliza akiwa na magoli 25 na assist 21, kiukweli ni perfomance ya hali ya juu lakini ukichunguza kiundani utajua how stats can fool you.

Katika magoli 25 ya messi, magoli 20 amezifunga timu zilizo chini ya nafasi ya 10 (11-20) hii ni 80% ya magoli yake yote

KWAHIYO HIZO TIMU ZA CHINI ULITAKA AFUNGE NANI?
Ambao sio ma GOAT ndo wafunge
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
17,021
2,000
Sio mzigo ila shida ni kwamba kuna baadhi ya mambo jamaa anakuwa overatted na hilo utakundua ukifanya analysis lakini kuhusu goli 91 ni kweli hiyo ni great perfomance
To be fair msimu huu jamaa hana performance kubwa. So you can throw all that you want lakini alichofeli kwenye kuscore amecompensate katika assisst.

Pia naamini Barcelona inaishiwa kikosi kipindi hichi. Wachezaje nane wanakaribia au wamepita 30s so overall performance ni mbovu pia tofauti na wachezaji alionao Lewandowski, Haaland au Ronaldo hawa anaweza toka mtu akaingia mtu ila siyo Barcelona ya sasa.

Na kwakua hata youngsters waliopo Barca ni viazi tutarajie hii rock bottom aliyopo Messi kuendelea na next season, unless akienda Juve kama ripoti zinavyodai.
 
Apo umeongea mkuu
 
Barca isipokuwa makini kwenye kujenga timu upya tutayaona na ya man u sio mda
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
17,021
2,000
Barca isipokuwa makini kwenye kujenga timu upya tutayaona na ya man u sio mda
Hili liko wazi sana. Maana katika youngster ambaye anatajwa sana ni Ansu Fati ambaye ghafla hype imekata kwakua hata kudeliver imekua tatizo. Na maajabu yake wamemleta Pjanic, mchezaji mwingine in his 30s
 
Kelevra

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
294
500
Mkuu hiyo dought ulimaanisha doubt au?
Tukiachana na hayo mimi pia huwa siamini kwenye stats inapokuja suala la football.
Messi kama Messi ameshaidhihirishia dunia kuwa yeye ni hatari kwa kufunga michezo mikubwa kama two finals against Man U ikiwemo game iliyochezwa Wembley chini ya Mabeki kama kina Ferdinand na Nemanja Matic...Ndiye mchezaji anaongoza kuifunga Madrid ambayo ni timu bora kuwahi kutokea tangu kuanzishwa kwa mpira...mbaya zaidi ameifunga Madrid even kipindi kuna beki zenye roho mbaya kama Pepe na Sergio Ramos...Kuhusu Jerome Boateng CV yake ilishushwa na Messi huyo huyo akiifunga Bayern sina shaka unaujua ubora wao...any way tuachane na hizo maana nazo ni stats ila nikukumbusha tu huyu jamaa anafunga timu kubwa kuliko mchezaji yeyote niliyewahi kumshuhudia.

Mwaka 2010 Winfrey Schneider alikuwa akiclaim tuzo ya uchezaji bora as alikua na Uefa Cup pia alikua Finalist wa Worlcup...Zlatan Ibrahimovic alimuuliza Schneider kwamba ana uhakika anajua kuliko Messi?
Swali ambalo napenda ujiulize nafsini mwako mtoa mada bila ya hizo stats una uhakika hao unaowashindanisha na Messi wanajua kuliko Messi? Messi ambaye tunajua ni floppy lakini anahusika kwenye goal 40+?

Mwisho napenda kukumbusha kwamba Napoli haiwezi kumlipa Messi zama zimebadilika alichoapply Maradoma can't be applicable in a modern football unless aende kustaafu huko Napoli.
 
wazunguwawili

JF-Expert Member
May 29, 2019
1,919
2,000
Umeufunga uzi mzee. Salute kwako. Sijajua yeye timu kubwa kaangaliaje.

Mkuu Nemanja Matic ~ Nemanja Vidic apo utakuwa umechanganya, hata hivyo ulikuwa unaona messi anacheza barcelona ya aina gani na hata magoli aliyoshinda mwenyewe umeyaona hata Goroud angeshinda compare Zidane (1998&2002) Isitoshe hata ronaldo tu

Swala la Wesley Sneidjer ( umekosea kuandika) , mkuu kwani zlatan ni nani katika soka? Kwamba akiongea ndio kaongea au? Ballon d or inatolewa kwa mchezaji aliyeperfom vizuri kwa msimu au mwaka husika na sio permenent mfano mdogo tu Michael Owen kachukua balon d or 2001 unataka kusema alikuwa bora kuliko Gaucho, De lima , Zidane, Nedved au?????? 2010 Sneidjer alikuwa na mafanikio yafuatayo

-UEFA CHAMPONS LEAGUE ( akiwa yeye ni kinara wa assist ikiwemo assist 2 za fainali alizompa diego milito)
(Kumbuka hap hao inter waĺimtoa barca kwenye knockout)
- kashinda Sarie A na Coppa Italia kiujumla na UEFA tunasema TREBLE
- Reaching world cup Final huku akiwa na magoli 5 na man o the match 4 ikiwemo mechi waliyowatoa brazil ya kina ricardo kaka

-messi msimu wa 2010 aliishia kuvaa medali ya La Liga tu hata copa del rey hakunusa af bado unataka kusema nini mkuu?

Halafu pia kama unaongelea El clasico ni wazi messi kacheza mechi nyingi za el classico so lazima tuexpect atakuwa na magoli mengi hata hivyo ukichunguza utajua mengi ni ya 2015- kurudi nyuma ikiwemo 5-0 ile madrid mbovu ya morinho hata ivyo ukisema.

Sijakuelewa mkuu, mpira umebadilika nini siku hizi mkuu hadi jambo alilofanya maradona lishindikane?? Kama ni mabeki unaowataja kina ramos hata miaka hiyo walikwepo, kumbuka maradona kacheza dhidi Maldini na Baressi na Costarcuta wakiwa upande wa ac milan huo ni ukuta ulioruhusu magoli machache kuwahi kutokea bado kacheza na west Germany yenya watu kama kina Lothar Matthaus na Karl Heinz Rumennige ( tembelea list ya ballon d or utawaona) sasa nini kimebadilika mkuu???
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom