News Alert:Ya Kibanda Yahamia Kahama,Yamkuta Polisi!

News Alert:Ya Kibanda Yahamia Kahama,Yamkuta Polisi!

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
4,225
Reaction score
869
HABARI za uhakika zilizonifikia hapa Ofisini kwangu zinasema watu wanaodhaniwa kuwa ni vibaka kutoka katika machimbo ya dhahabu ya Nyangarata na Mwime wilayani Kahama mkoani Shinyanga,ambayo yamekwisha uzalishaji wake,wamemuua askari wa Usalama barabarani;Salum Mtepa mwenye cheo cha Staff Sajenti,kwa kumpiga na kitu kizito kifuani.


Tukio hilo lilitokea nyumbani kwake eneo la Majengo mjini Kahama usiku wa kuamkia jana baada ya watu hao wanaokadiriwa kuwa wanne kufika nyumbani kwake na kuvunja kibanda cha biashara kwa lengo la kuiba ndipo askari huyo alipotoka nje kwenda kupambana nao.


Ilidaiwa baada ya kutoka nje vibaka hao waliokuwa na pikipiki watatu walikimbia akabaki mmoja aliyekuwa na kifaa ambacho hutumiwa na wachimbaji wa dhahabu katika machimbo madogo madogo kwa ajili ya kuvunjia miamba ya mawe ambacho hujulikana kwa jina la Moko.


Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Polisi wilaya ya Kahama;George Simba,askari huyo alipigwa na kifaa hicho kifuani wakati akijaribu kupambana na kibaka huyo,hali iliyopelekea kuvuja damu nyingi ndani ya kifua na kusababisha kifo chake.


Simba alisema hali ya vibaka katika mji wa Kahama ni mbaya kwani wameongezeka kutokana na machimbo ya Nyangarata kujaa maji na Mwime kuisha uzalishaji wake,hali iliyofanya vijana wengi kutoka kwenye maeneo hayo bila kuwa na fedha.


Alisema hivi sasa wimbi la vibaka hao limekuwa tishio huku akiahidi kupambana nao ikiwa ni pamoja na kuwasaka kwa nguvu zote vibaka waliohusika na kifo cha askari huyo wa usalama barabarani,ingawa hadi leo mchana hakuna mtu yeyote aliyekuwa amekamatwa juu ya kuhusika na tukio hilo.
 
poleni sana ndugu zangu wa Kahama! na kuweni makini kwa watu msiowafahamu.
 
Nani ana picha ya hicho kifaa kinachoitwa MOKO nikione?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
R.I.P traffic police but mind yourselves that civilians can also kill. Be justers.
 
Kwa hiyo Unataka tuamini Kibanda alitamiwa na kujeruhiwa na vibaka??
 
Sasa hii na ya Kibanda vina uhusiano gani?huyu karestishwa na vibaka,wakati kibanda kangolewa visagio incl meno,kucha,nk na maafisa usalama wa taifa kwa agizo la wakuu wa nchi!! Mi nikajua policcm kafanyiwa na uwt kumbe wapi.
 
Back
Top Bottom