NEWS Alert:CCM yapata pigo


WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Messages
4,225
Points
1,195
Age
40
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2011
4,225 1,195

Wakuu wakati baadhi ya wanaCDM wanakimbilia ndani ya CCM,wale wajanja ambao tayari wameusoma upepo wa siasa za nchi hii na hasa wanasiasa waliokamaa wanasepa na kujiunga CDM,hebu soma huyu kamanda ambaye wakati wengine wanaikimbia CHADEMA yeye amekurupuka kutoka CCM na kujiunga chadema.

MWISHONI mwawiki iliyopita chama cha Mapinduzi CCM wilayani Geita kilipata pigo baada yakada wake maarufu katika wilaya hiyo na mkoa mzima wa Geita kwa ujumla DaudSunzu Katwale Ntinonu kuhamia chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA).


Kuhama kwa Katwale kutoka CCM na kwenda CHADEMA ni pigo kubwa kwa CCM na hasa ikizingatia kwambakada huyo amehamia chama ambacho kwa sasa kinaonekan kuishika pabaya CCM katikawilaya hiyo na maeneo mengi ya Mkoa wa Geita,jambo ambalo ni wazi kuwa litakuwalimeleta mshituko ndani ya chama Tawala.

Kada huyo mwenye miaka 49 tangu kuzaliwa kwake alizaliwa katika kijiji cha Ikurwa kata yaIhanmilo Tarafa ya Geita wilayani Geita,lakini akakulia katika kijiji chaKatende wilaya ya Chato ambayo wakati huo ilikua katika Wilaya Mama yaBiharamulo katika mkoa wa Kagera.

Alianza kujihusisha na masuala ya Siasa mwaka 1988 ambapo alichagulia kuwa Katibu waVijana kata ya Katende ambapo mwaka 1993 akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa vijanawa kata na wakati akiwa na nafasi hiyo aliamua kugombea Udiwani wa kata hiyomwaka 1994 na kufanikiwa kupata nafasi hiyo.

Akiwa nacheo cha Udiwani Katwale alifanikiwa kuongoza kamati mbalimbali za kudumu zahalmashauri ya wilaya ya Biharamulio hadi alipomaliza awamu yake mwaka2000,ambapo hakugombea tena nafasi hiyo na kuamua kujiingiza akatika masuala yaBiashara na wakati huo akawa amehamishia shughuli zake za kibiashara wilayaniGeita.

Alipofika wilayani Geita mwaka huo huo akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa wafanyabiashara wawilaya hiyo pamoja na kuwa kamanda wa Vijana wa kata ya Kalangalala,nailipofika mwaka 2002 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo namjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza hadi 2007.

Mwaka2003-2008 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza kuu la Wazazi Taifa,na mwaka 2002alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka katika kata yaKalangalala cheo ambacho amedumu nacho hadi uchaguzi wa ndani ya chama hichoulipofanyika Mwezi Novemba mwaka huu.

Nasema CCM imepata pigo kubwa kwa sababuka kwa mujibu wa Wasifu wa kada huyu hapo juu niwazi kwamba alikuwa ni mwanasiasa aliyekubuhu na hasa ikizingatiwa kwambawakati wa uongozi wake ndani ya chama cha Mpinduzi katika wilaya hiyo yenyemajimbo matatu ilikuwa haina upinzani wa kutisha kama uliopo hivi sasa.

Kibaya zaidi kwa CCM ni kwamba Katwale amejiunga na Mpinzani wake Mkubwa katika msuala yaKisiasa na hasa katika wilaya ya Geita ambayo kwa sasa hakuna ubishi kwambaCHADEMA kimekuwa na nguvu kubwa na kadri siku zinavyokwenda kinazidikujiimarisha na hasa vijijini ambapo siku za nyuma ilikuwa haikubaliki kwawananchi ukiachilia mbali maeneo ya mjini.

Yawezekana CCM wakamdharau Katwale kwa sasa kwamba hana kitu lakini ukweli unabakipalepale kwamba huyu ni mtu hatari sana katika masuala ya kisiasa na hata badhiya viongozi wa CCM Taifa wanamfahamu na pia misimamo yake katika masuala yamsingi ambayo wakati mwingine yalisababisha kukosana na viongozi wakubwa wachama hicho Taifa na hivyo kumjengea chuki na kuamua kumuondoa kabisa kwenyemedani ya siasa kwa kuhakikisha hapiti katika nafasi yoyote alliyoomuakugombea.

Ni mtu mwenye uwezo wa kujenga hoja kuiwasilishamahali panapotakiwa na kuisimamia,haijalishi atabaki peke yake katika hoja hiyolakini lengo lake ni kuhakikisha kwamba haki inapatikana,ndiye kiongozi pekeeambaye aliwahi kuwawajibisha kwa kuwafukuza ndani ya chama zaidi ya mabalozi100 waliodaiwa kukisaliti chama wakti wa uongozi wake,lakini pia aliwakemeabadhi ya viongozi walioonekana kwenda kinyume na madili ya chama.


 

Attachments:

K

Kamuzu

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Messages
996
Points
225
K

Kamuzu

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2008
996 225
Haya bana, kwa mbali nawaona waleeee, wanakuja jiandae.
 
GOOGLE

GOOGLE

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Messages
1,870
Points
2,000
GOOGLE

GOOGLE

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2012
1,870 2,000
Wala hakuwa kada mkubwa huyo bwana.
 
A

adolay

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Messages
8,565
Points
2,000
A

adolay

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2011
8,565 2,000
Wanaokimbia chadema kurudi ccm wanayao moyoni na ukisection brain yao nikama wametapeliwa maana ukweli watausoma wakiwa wamechelewa.

Wakati cdm inaelekea peponi wao wanaelekea kuzimu kwa kuikimbiia heri na kuifuata shari.
 
Apolinary

Apolinary

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2011
Messages
4,726
Points
1,225
Apolinary

Apolinary

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2011
4,726 1,225
Ni sawa lakini hatopewa nafasi ya kugombea ubunge mwaka 2015! Vingnevyo atakua ni mlaku wa madaraka tu! Haiwezekani mtu kaona cdm ina population ya watu ndo anakuja kujiunga nayo . Siku zote alikuwa wapi?
 
Father of All

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Messages
3,090
Points
1,225
Father of All

Father of All

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2012
3,090 1,225
Sioni pigo zaidi ya kuwa siasa za kawaida. Pigo ni pale CCM itakapoangukia pua.
 
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Messages
4,225
Points
1,195
Age
40
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2011
4,225 1,195
Ni sawa lakini hatopewa nafasi ya kugombea ubunge mwaka 2015! Vingnevyo atakua ni mlaku wa madaraka tu! Haiwezekani mtu kaona cdm ina population ya watu ndo anakuja kujiunga nayo . Siku zote alikuwa wapi?
Ni kweli lakini nadhani hakujiunga CDM kwa ajili ya kutafuta ubunge,isipokuwa nadhani ni vyema ikaeleweka tu kwamba wakati wengine wanakimbia wengine wanaingia,kwa hiyo hili ni jambo la kujivunia kama chama.
 
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Messages
4,225
Points
1,195
Age
40
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2011
4,225 1,195
Sioni pigo zaidi ya kuwa siasa za kawaida. Pigo ni pale CCM itakapoangukia pua.
Yawezekana unalosema likawa sahihi lakini nadhani hata mvua kubwa yenye dhamira ya dhati ya kunyesha huwa haianzi kwa Kasi,mara nyingi inaanza manyunyu kana kwamba haitanyesha!!!!!!!!!
 
N

nummy

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2011
Messages
587
Points
0
N

nummy

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2011
587 0
Huo ndio mtindo wa CCM kama hujui, wana mtuma mtu maarufu sana ili kukupumbaza kwamba amehama. Kwani vigogo wa CDM wako upande upi unavyofikiri wewe
 
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Messages
4,225
Points
1,195
Age
40
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2011
4,225 1,195
Huo ndio mtindo wa CCM kama hujui, wana mtuma mtu maarufu sana ili kukupumbaza kwamba amehama. Kwani vigogo wa CDM wako upande upi unavyofikiri wewe
Mi naamini siasa ni usanii ndiyo maana simuamini mwanasiasa yeyote,naishi naye na kumsikiliza lakini simwamini kabisa.
 
Ringo Edmund

Ringo Edmund

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2010
Messages
4,891
Points
0
Ringo Edmund

Ringo Edmund

JF-Expert Member
Joined May 10, 2010
4,891 0
ccm bana kuna viongozi wa votongoji hapa morogoro,mkundi wamenuniliwa na ccm wanadai ni vigogo wa chadema.
 
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Messages
4,225
Points
1,195
Age
40
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2011
4,225 1,195
ccm bana kuna viongozi wa votongoji hapa morogoro,mkundi wamenuniliwa na ccm wanadai ni vigogo wa chadema.
Sasa wamenunuliwaje kama ni viongozi wa CCM,hebu fafanua naona kama vile umejichanganya?
 

Forum statistics

Threads 1,283,662
Members 493,764
Posts 30,796,057
Top