Kuna ushahidi gani kwamba Raia Mwema au Dr. Slaa watamulikwa kwa ajili ya kuongea bila ''kigugumizi'', kwa kuongea taarifa ''za kina na uchunguzi'' Watachunguzwa na nani?
Sasa unataka watu waongee vipi? Kwa kigigumizi, bila kufanya uhcunguzi wowote? Kuhusu Dr. Slaa kwamba anaweza kuwa mgomea Urais kwa tiketi ya Chadema na uwezekano wake wa kushinda Uchaguzi, hilo sijui, sijalifikiria. Lakini hapa lazima ukumbuke what Mao Zedong used to call ''objective reality and subjective thinking.'' Kwamba lazima tuhahakikishe kwamba tunalinganisha subjective thinking yetu na objective reality.
Usiseme Dr. Slaa anafaa kuwa Rias kwa vile tu Dr. Slaa ni binamu yako, au tu kwa vile wewe ni mwanachama wa Chadema, lakini lazima utazame objective reality na uone kweli kama Dr. Slaa anao uwezo wa kushinda kura ya Urais.
Unaweza kutazama ukaona kitu mbele yako ambacho hakipo,kipo tu ndani ya mawazo yako. Unaweza kuitazama kamba ukafikiria kwamba ni nyoka. Kwa hiyo unaweza kumtazama Dr. Slaa ukadhani anaweza kuwa Rais, kumbe ni kama kufikiria kwamba kamba ni nyoka. Au unaweza kumtazama nyoka,na ukadhania kwamba ni kamba, halafu matatizo mengi yanaweza kukufika.
Kwa hiyo, wakati mwingine unatazama kitu,kumbe hakipo, vile unavyokiona wewe. Wakati mwingine unatazama kitu, kumbe kiko vile vile unavyokitazama wewe. You have to decide.
Labda Dr. Slaa anazo qualities ambazo zinaweza kumfanya awe Rais. Labda you were not wrong in thinking kwamba Dr. Slaa anafaa kuwa Rais. Lakini hizo qualities anazo kiasi gani,to what extent. Do not give too much credit, do not give him too little credit.
Hapa, I must say, siongee kuhusu qualities za Dr. Slaa,and whether or not anafaa kuwa Rais,[hayo mambo nitawaachia politcal commentators. Jambo muhimu ni kwamba unaposema kwamba Dr. Slaa anafaa kuwa Rais, kama wewe ni political comentator, uyakumbuke maneno hayo uliyoyasema kabla yauyakumbuke baada ya Uchaguzi, ama sivyo utakuwa kama Shekh Yahya, ambaye anatabiri mambo mengi kabla ya Uchaguzi, lakini baada ya Uchaguzi hakuna mtu yoyote ambaye anakwenda kumuuliza, mbona mambo aliyotabiri hayakutokea] ila naongea tu kuhusu umuhimu, ulazima, wa kulinganisha subjective thinking na objective reality.
Kama vile Polisi wanavyoweza kuwakamata washukiwa kadhaa katika tukio la uhalifu, halafu inabidi waamue kama wote wanahusika, and to what extent, au labda wote hawahusiki na inabidi waachwe huru.