Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,910
- 2,789
Wakuu nimekaa nikatafakari kiasi kuhusu mwenendo wa dunia yetu hii. Tunaishi kwa matukio. Dunia bila matukio, yawe mazuri au mabaya haijakamilika. Sasa wapo ambao wanatengeneza hayo matukio na wapo ambao wanaishi kulingana na hayo matukio. Wengi wetu tunaishi kulingana na matukio hayo. Wachache wao ndio hutengeneza matukio hayo. Mojawapo ni trend ya sasa ya uhuru wa kujiamulia hasa linapokuja suala la mwili wako.
Kwa uchache niliyoyasikiabtoka hiyo new order ni kuwa taasisi ya familia inavunjwa vunjwa. Pia kuundwa kwa jinsia ya tatu. Imani itahama toka kumwabudu Mungu hadi kumuabudu binadamu, n.k.
Kwa trend iliyopo ni kuwa tunaishi katika dunia ambayo kwa asilimia kubwa tunaona au kusikia yanayotendeka. Tunaweza kuweka kumbukumbu kwa namna mbalimbali. Hata baada ya miaka 2000 kuanzia leo, vizazi vijavyo vitakuwa na access ya taarifa nyingi sana kama vile wanaangalia filamu. Hayo sisi hatukubahatika kuyaishi, ndio maana hadi leo bado suala la imani kwa mfano lina utata mwingi. Picha ya Yesu tu inatutoa jasho kama kweli tunazoona zinakaribiana na ufanano wa Yesu mwenyewe.
Hoja yangu ni kwamba, ukristu uliingia duniani miaka 2000 iliyopita. Kabla ya hapo hapakuwa na ukristu. Yapo mengi sana yalifanyika katika kuueneza ukristu. Ndipo tunasikia vita ya msalaba, yaani Crusade. Walioishi nyakati hizo wangekuwa na teknolojia hii tungeshangazwa na yaliyopita. Hatimaye ukristu upo.
Miaka 500 baadaye uislam ukaingia. Ukaenezwa kwa kila mbinu na mabavu na tukasikia kuhusu jihad. Watu wakafa, watu wakasaliti imani zao. Hatimaye uislam upo.
Ukapita muda mrefu zikaanza pilika za New world order na matao yake. Ndio leo tunasikia kuhusu LGBTQIA na shifa zake. Hii ajenda kwa sasa inapitishwa kulingana na wakati tuliopo. Muda ukifika ni wazi kuwa new world order nayo itashika hatamu. Haya yatatokea kwa kuwa hii ni dunia.
Tuliosoma historia tuliwashangaa sana kina Chief Mangungu kwa kurubuniwa kwa shanga na vioo. Miaka 500 mbele vizazi vijavyo vitashangaa ilikuwaje babu zao wakarubuniwa kwa kukopeshwa. Hatuyaoni haya kwa kuwa tuko ndani ya box. Tukishatiwa katika kapu la historia ndio itakuwa njia bora zaidi ya kujua ni nini kilitokea kipindi cha karne ya 21. Ni hayo tu