mameneja wazuri wakuendesha hotel?
Nachokiona hapa ni kuwa wasauzi afrika wao wanathamini vyao hata kama wako nje ya kwao, itakumbukwa watu walishapiga kelele kuhusu bidhaa zipatikanazo shoprite ya kuwa hadi nyanya na vitunguu hata mchicha vinatoka hukohuko SA, sasa ambacho watu watajionea hapa ni kuwa mchanga, maua, mbolea, signboards, tisheti, viatu, sabuni, vitambaa, computer, curtains na vyooote vinatoka sauzi afrika, hivi ina maana hapa hatuna hivyo vitu; vingine itasemekana labda viwango na jee hata mbolea na mchanga??
Ikumbukwe walisema katika ajira wataweka mbele wazawa...hii imefia wapi??
Kali nyingine ni kuwa Raisi wetu yuleyule aliyeifunguaga Snow Crest Hotel then kesho yake ikaja kuvunjwa ukuta ndio anakuja tarehe 17Dec kuifungua hii ambayo ilikuwa mali ya watanzania then mkapa na magufuli wakaiuza na sasa watanzania hawana hata percent moja hapa, hilo moja pili ni kuwa wafanyakazi woote ni wametoka kenya ama sauzi afrika ma bara asia na pia waliopewa tenda za ku-supply vyakula ni wakenya tupu na vyote vinatoka hukuhuko kenya kuanzia kuku, maharage hadi matunda, jamani rais hana washauri wakamfungua kwenye hili na jee watanzania tutakuwa wapole hadi lini watu wanakuja kupora malighafi zetu na kukimbia??
Hotel hii hadi maua na mchanga vyote vimetoka South Africa ambapo ndipo ilipo kampuni iliyopewa jukumu la kuindesha hotel hii ijulikanayo kama Zabulan.
Acha uongo wewe hii hotel inamilikiwa kwa ubia mwenye hisa nyingi ni Sunda mfanyabiashara wa madini Arusha na anaimiliki kupitia kampuni ya blue jewel ya Arusha, acha kudanganya wana jf ukifikiri wote hatuna taarifa umetumwa nini?
Kampuni ya Blue jewel iliingia ubia na Southern Africa Development Fund, ndio wawekezeaji wenza wa Sunda ukiiendelea na uongo wako hapa nakuumbua.
Acha chuki tunataka mji wetu wa Arusha uendelee na sio kuleta chuki kama zako
Kwa hiyo Sumaye naye yumo?Heshima kwako Mchaga,
Mkuu wangu Sunda ana hisa chache sana wawekezaji ndio majority shareholder.sunda alifulia siku nyingi hakuwa na sababu ya kuvunja vunja Mt meru alitakiwa kufanya ukarabati kidogo uku biashara ikiendela alikuja gundua hawezi kuikarabati hotel mwenyewe ikabidi awaite wawekezaji wa kumsaidia kuikarabati na kuiendesha upo mkuu.Ebu fikiri kidogo muda aliotumia kuikarabati hadi leo ni miaka mingapi.Kwa taarifa yako Mt meru bila mkono wa F Sumaye waziri mkuu mstaafu Sunda asingeipata sana sana wanamtumia.
Ndio manake ,unauliza ndevu kwa OsamaKwa hiyo Sumaye naye yumo?
Nice and Beautiful again,
Looks like Kempinsk Kilimanjaro Hotel.
Arusha ni Mahoteli Full kuanzia Sanawari,Ngurelo & Philips hadi raha.
Karibuni Sana Arusha.