new HIV

njoro

Senior Member
Dec 21, 2010
178
8
Mara baada ya kuambukizwa HIV, dalili za mwanzo ni zipi? na inachukua muda gani hizo dalili kuanza kujitokeza? Naombeni kujuzwa jamani
 
Ukienda kupima na kukuta umeathirika watakupa ushauri wa nini cha kufanya. Kama umepima mwenyewe na hivi test tube wanazouza mitaani nenda kajisalimishe kwa wataalamu watakupa ushauri nasaha!!:hat::hat:
 
nenda zahati iliyokaribu watakufahamisha vizuri na kukutoa wasiwasi
 
pombe mbaya mkuu..inatokea ila ukipima kama hauna usirudie tena..jifunze kujizuia mkuu inasaidia..majuto ni mjukuu...halafu ngoma si kama malaria...ngoma hauponi mkuu ndo ntolee so kua makini next time
 
Umenikumbusha wasiwasi niliokuwa nao kipindi fulani. Ila baada ya kupima kama mara tu hiv na kukuta niko fiti, sa hiv mna mchumba wangu mmoja na nategemea kumuweka ndani soon. Vicheche mwiko kwani hamna faida zaida ya kukuharibia ndoto zako tu.
 
Umenikumbusha wasiwasi niliokuwa nao kipindi fulani. Ila baada ya kupima kama mara tatu hiv na kukuta niko fiti, sa hiv mna mchumba wangu mmoja na nategemea kumuweka ndani soon. Vicheche mwiko kwani hamna faida zaida ya kukuharibia ndoto zako tu.
 
Ni ngumu sana ndugu yangu kujua kama umeambukizwa ukimwi bila ya kupima kwa siku za mwanzo. Maana kuna wengine huwa hawaonyeshi dalili zozote zile hata kwa miaka kumi.Kwa mujibu wa uanishaji uliofanywa na wataalamu wa shirika la Afya Duniani yaani WHO, kuna hatua (stages) kuu nne za ugonjwa wa VVU/UKIMWI ambazo ni:

1. Hatua ya kwanza [Primary HIV Infection]
Hatua hii huwa kwa muda wa wiki nne. Ni asilimia 20 tu ya watu wenye maambukizi ya VVU walio kwenye hatua hii ambao hupata dalili na viashiria vikali vya ugonjwa huu lakini mara nyingi madaktari hushindwa kutambua kama mgonjwa amepata maambukizi ya VVU kutokana na dalili na viashiria vyake hapa kufanana sana na dalili za magonjwa mengine. Mgonjwa aliye katika hatua hii ya kwanza ya maambukizi ya VVU huweza kuonesha dalili na viashiria kama vile kuvimba tezi (swollen lymph glands), kupatwa na homa kali, kuumwa koo (sore throat), kujihisi mchovu, kujihisi maumivu sehemu mbalimbali mwilini (body aches), kutokwa na vipele mwilini (skin rash), na pia kutapika, kuharisha au kuumwa tumbo

Mgonjwa anayepata dalili na viashiria hivi tunasema kwamba amepata “Acute HIV infection/Acute HIV retroviral infection au seroconversion illness.” Dalili hizi hutokana na mwili wa mtu mwenye maambukizi ya VVU kuanza kutengeneza kinga dhidhi ya VVU.
Hatua ya Pili (Clinically Asymptomatic Stage)

Katika hatua hii ambayo inaweza kudumu kwa muda wa miaka kumi, mgonjwa anakuwa haonyeshi dalili/viashiria vyovyote vile isipokuwa anaweza kuwa na tezi zilizovimba [swollen lymph nodes]. Kiwango cha VVU kwenye damu hupungua sana lakini mgonjwa anaweza kuambukiza mtu mwingine yoyote na vipimo vya VVU vina uwezo wa kutambua uwepo wa maambukizi y VVU katika damu.

Tafiti mablimbali zimeonesha kwamba VVU katika mwili huwa bado zinazaliana [active] na hukimbilia/hujificha kwenye tezi [lymph nodes]. Kutokana na kujificha kwake katika hatua hii, kipimo cha kupima wingi wa virusi vya ukimwi (Viral load test) katika mwili hutumiwa sana ili kuweza kutambua uwepo wa VVU. Kipimo hiki pia husaidia katika kumpangia mgonjwa tiba yake.

Hatua ya Tatu [Symptomatic HIV infection]
Kutokana na kuongezeka kwa wingi wa VVU katika mwili, kinga ya mwili huzidi kudhoofika na hii husababishwa na;
• Tezi na tishu zilizoathiriwa na VVU huharibika kutokana na maambukizi ya muda mrefu
• VVU hubadilika badilika na kuwa na uwezo zaidi wa kuathiri tishu na sehemu mbalimbali za mwili na hata kuziua/kuziharibu seli zinazokinga mwili kutokana na maambukizi zinazojulikana kama T helper cell
• Mwili hushindwa kumudu uharibifu wa T helper cell na kushindwa kuzalisha seli nyingine mpya.


Kama mgonjwa wa VVU hatumii dawa za kuvubaisha VVU au anatumia ARV's ambazo hazimsaidii au hazifanyi kazi vizuri mwilini mwake, basi mgonjwa ataendelea kuingia kwenye hatua ya nne ya Ukosefu wa Kinga Mwilini (Ukimwi) au AIDS.


Hatua ya Nne [UKIMWI]
Hatua hii hujulikana kama Ukosefu wa Kinga Mwilini [UKIMWI] au AIDS, ambapo mgonjwa hupata maambukizi ya magonjwa nyemelezi pamoja na saratani za aina mbalimbali kutokana na kupungua kwa kinga mwilini.

Hivyo ni vyema ukapime tu ndugu yangu ili uondokane na hofu.. ukishapima utajiona kama umetua mzigo.
 
Muarubaini nami iliwahi kunitokea kama wewe, yani ilichukua kama mwaka mzima kujishahuri kwenda kupima. Nakumbuka Bf wangu aliniambia tukapime nilimzungusha sana, mwisho nikafunga safari peke yangu kwenda kupima...nilipopata majibu siku hiyo hiyo nikampigia simu tukapime, nilipomu hadithia alicheka sana. Toka hapo nimetulia kwa mpenzi wangu na nimejijengea tabia ya kupima mara kwa mara.
 
Umenikumbusha wasiwasi niliokuwa nao kipindi fulani. Ila baada ya kupima kama mara tu hiv na kukuta niko fiti, sa hiv mna mchumba wangu mmoja na nategemea kumuweka ndani soon. Vicheche mwiko kwani hamna faida zaida ya kukuharibia ndoto zako tu.

Kipi hapo kinagarantii huyo mchumba wako kutokwenda kuutafuta unakopatikana na kukuambukiza?

Mpk hapa hamna aliyejibu swali lililoulizwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom