Neverland Ranch (makazi ya Michael Jackson)

Basi Nenda

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
20,184
45,910
Michael anatajwa kuwa moja kati ya watumbuizaji bora zaidi kuwahi kutokea hapa duniani,lakini pia watu wengi humfahamu kama mwanamuziki aliyekuwa na visa vingi zaidi duniani.

Moja kati ya sifa zake kubwa ni kwamba mtu huyu alikuwa ni mtoto aliyekataa kukuwa kama PETER PAN ambaye ni muhusika katika stori za watoto ambaye yeye aliishi kwenye kisiwa ambacho watoto hawakuwi ,hawazeeki na hawafi,kisiwa hicho ni never land

Michael jackson aliipenda sana stori hii ya peter pan, huenda kwa sababu alikuwa na mambo na matendo ya kitoto wakati ni mtu mzima,mapenzi yake hayo kwa hadithi hiyo ilipelekea naye ajijengee never land yake mwenyewe kama ya peter pan

Basi akanunua eneo lenye ukubwa wa ekari 12,700 huko California kwa USD 19.5 million, mwaka 1987 na kulifanya makazi binafsi,vifuatavyo ni vitu alivyoweka humo ndani

1.TRAIN STATION
Michael jackson alinunua train mbili za mvuke na kujenga reli ( three railroads: one 3 ft (914 mm) narrow gauge named "Neverland Valley Railroad) kwake pamoja na train station kubwa kuliko ile ya kigoma,train hizo zilifanya kazi ya kumzungusha tu homo ndani yeye na wageni wake ambao wengi ni watoto
Na palikuwa na wahudumu kabisa waliogawa ice cream ,pipi nk kwa wageni,
Baadae aliongeza treni moja ya umeme kwa ajili ya watoto wake


2.ZOO (bustani ya wanyama)
Michael jackson alikua ni mtu mpenda wanyama sana,kwa mfano alinunua sokwe kwa usd 65,000 sokwe mmoja tu aliyeitwa bubble,alisafiri nae kote duniani alipokwenda na alipandishwa first class kwenye ndege,
Kwenye zoo yake aliweka wanyama kama tiger,simba,tembo,twiga ,swala,mbuni nk


3. AMUSEMENT PARK
Michael alipenda sana michezo ya kitoto hivyo alijenga nyumbani kwake hapo sehemu ya kuchezea na kuweka vitu kama. Ferris wheel ,
Carousel, Zipper , Octopus, Pirate Ship ,
Wave Swinger, Super Slide, roller coaster, bumper cars (gari za umeme) na
amusement arcade

4.ARTIFICIAL LAKE (ziwa bandia)
Mj hakuishia hapo alijenga ziwa bandia lenye ukubwa wa heka nne likiwa na maporomoko ya maji,

5.VIWANJA VYA MICHEZO
michael aliweka viwanja vya basketball , tennis nk

6.NYUMBA ZA MAKAZI NA WAGENI
nyumba aliyoishi ilikua na vyumba 6 vya kulala na bafu 9
-kulikuwa na nyumba ya wafanyakazi
-nyumba ya zimamoto (fire department)
-nyumba za wageni
-jumba la cinema la kutosha watu 50

Neveland iliendelea kuwa makazi ya michael mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambapo alikataa kurudi kuishi hapo kwa sababu police walipafanyia uchunguzi juu ya tuhuma zake za kubaka watoto,alidai wamepadhalilisha hivyo hawezi tena kurudi,na hakurudi kuishi hapo mpaka anakufa

NB: Kwa sasa makazi hayo yanauzwa kwa dau la USD 100 million







220px-NeverlandRidesGone.jpeg
2929119800000578-3101512-Strict_The_agents_have_stressed_that_this_is_not_fans_chance_to_-a-1...jpeg
2929115800000578-3101512-Grand_living_quarters_WSJ_reports_the_home_which_is_located_betw-a-1...jpeg
2929116C00000578-3101512-Renovated_Listed_by_Sotheby_s_and_Hilton_Hyland_most_of_the_tell-a-2...jpeg
2928999A00000578-3101512-Mini_town_While_the_amusement_park_has_now_been_removed_there_ar-a-2...jpeg
220px-Neverland_Ranch's_gates.jpeg
292899E700000578-3101512-Not_the_same_Neverland_pictured_2001_now_known_as_Sycamore_Valle-a-2...jpeg
 
Mkuu
Bill gate nyumba yake sio ya mchezo,inaweza kutambua hadi watu waliomo na anafuga nyangumi
Wanajimwambafai ila sio sana
Hawahitaji kujimwambafai saaana maana kila mtu anajua jamaa hela anazo.

Angalia hata Mengi hamna mtu alijua jamaa ana mjengo wa kufa mtu kule Machame mpaka alivyokufa ndo watu wakajua, ila angalia sasa vijana wa Bongo Fleva/Movie wakina wema/wolper wanavyopenda kujimwambafai kwenye nyumba za watu huku wamepanga,mpk hua wanafukuzwa kodi.
 
Back
Top Bottom