Never share your feeling with woman, never

Kuna Movie moja hivi ya ki China (nimesahau jina) niliwahi kuangalia zamani kidogo. Kuna mahali kijana mmoja alikua anataka kuoa kwaiyo akamuomba babu yake ampe ushauri kuhusu wanawake. Babu yake akamwambia;

"Show her you care, but never let her know how much you love her"

Leo nimeona huu uzi nikakumbuka hayo maneno ya kwenye ile Movie (Ilikua na subtitle) .

Mwanaume unatakiwa umjali mwanamke wako, mahitaji yake umtimizie lakini kamwe usije ukamuonesha unampenda kiasi gani! Yeye ndio anatakiwa akukadirie jinsi unavyompenda lakini asiwe na uhakika ni kwa kiasi gani. Namna bora ya kufanya hivi ni kujitahidi sana kuonekana neutral linapotokea jambo lolote linalogusa hisia zako kwa nguvu. Sio kisa tu umemuona dame wako amesimamishwa na mjamaa njiani, unaenda kuleta ugomvi nyumbani bila kujali walikua wanaongea nini. In fact, issue kama hizi unatakiwa kufuta tu mdomo kama haujaona vile, sijui kama unanielewa vizuri...!!

Mwanamke ataku.challenge sana kwenye vitu vingi ili tu akuone unavyo.react achukue point.. lakini wewe unatakiwa kumfanya aone kama kila kitu kwako wewe ni KAWAIDA tu. Akipatwa na tatizo, mfariji na sio kulia lia tena kama yeye. Mshirikishe mambo ambayo unaona anaweza akawa na msaada nayo tu, potezea mambo ambayo unajua hawezi kukusaidia chochote. Na hata akitishia kukuacha au akakuuliza kitu cha kukutega, usi.panick, fanya ajue tu kuwa hakuna kitu kitakachokutokea ambacho utashindwa kukabiliana nacho. Yes, that is a Sign of a Real Strength!

Ukiwa na mindset ya namna hiyo kama mwanaume, mambo mengi sana utayamudu sio tu kwenye mahusiano, lakini hata kwenye nyadhifa mbalimbali katika maisha. Hata ukitaka kuwa mfanyabiashara mzuri au kiongozi mzuri mahali popote pale, jaribu sana kukaa mbali na emotional decisions. Maamuzi ya hisia ni alama ya udhaifu!

La Mwisho, sio kila mwanaume anaweza kumudu changamoto zake zote za maisha peke yake. Na sio kila mwanamke ana tabia ya kutumia matatizo ya mwanaume kama silaha ya kumtawala. Kikubwa ni kujifahamu wewe na wanaokuzunguka. Kama umejaliwa kuwa na watu sahihi wenye msaada na nia njema kwako sio mbaya ukiwashirikisha mambo yaliyokuzidi uwezo wakusaidie hata kama ni wanawake. Just make sure unashare madhaifu yako + feelings zako na watu sahihi : )
 
Na hii siyo kwa wanaume tu hata wanawake wanatakiwa waitumie hii itawasaidia..
 
Miez 6 baada ya kuoa nikatakiwa kusepa kwa masomo kwa scholarship ya maana, si mbali kiasi cha kushindwa kurudi home kila nikipenda, ebana eeeh nlipigwa bit sio la nchi hii na mtoto kisu ninaempenda chagua nenda shule au ndoa huku mavyeti ya ndoa yakiwa yamemwagwa chini mbele ya mama mkwe! Nikasema hawa hawanijui mtoto wa mkulima mim, niache scholarship, na salary inabaki vilevile eti kisa mke, nikawaambia, hata kama mama yangu angekuwa anazikwa leo ningeondoka, ndugu wangemaliza msiba! Kwa sasa yeye ndio anafurahia maisha kuliko mim, hujisemea tu, yan wew ukishika lako mbishi sana! Never ever kuwa mnyonge kwa mwanamke, utateseka sana, na wenyew hawapendi mwanaume dhaifu na anaepelekeshwa kamwe, usishangae Shish huyoo kwa UCHEBE again

Sent from my SM-N910U using JamiiForums mobile app
 


Hapa sawa kabisa, you must have a feminine heart to know this.
Ila kuna kitu hujasema ‘weak women’ wagonjwa wa nafsi, waliojaa ombwe ndani yao hawa kwa hakika huhangaika kumcontrol mwanamme. Mwanamke mwenye afya ya akili na nafsi hujibidisha kumfanya mwanamme ‘Dume’
 
Mwanamme msimamo!!

mwanamke wa shoka humfurahia mwanamme anayesimama na ‘The right thing’
Sababu anajua siku moja mume atalazimika kusimama naye, akiwa anayumbishwayumbishwa huweza kumtelekeza kiwepesi zaidi hata huyo aliyepo pindi akipata chungu kipya.
 
Mkuu umeanza vizuri, ila umaliza vibaya,.
Shida zako na mkeo mwambie baba yako maana ndio mwanaume kama wewe.
Ni matumaini yangu ulikuwa ushindi jikoni na mama? 😎😎
Ila tulikubaliana hakuna kucatch fiilingz au jitaidi ubaki na akili zako
 
Ugumu unakuja pale mwanamke anatupotumia pesa au nguvu za kiume kama fimbo aisee utajuta sana...
 
nilivyopata tu watoto kila kitu kiliishia hapo sasa hv ni mwendo wa kuchomoa betri tu
 
Sasa wewe wapoteze wenzio😅😅😅
 
🍷🍾 Nakuja kulipa
 
nice stuffs😀😀keep on coming
 
Mwanaume lazima uwe strong, ukiwa weak kubali kulea watoto wa wenzio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…