Netanyahu Kutembelea Uganda - Entebbe!!

Kokola

Senior Member
Sep 5, 2015
135
78
Mwaka 1976 July 4 Makomando wa Jeshi la Israel (IDF) walivamia uwanja wa ndege wa Entebbe, Uganda na kuwaokoa raia wa KiIsrael waliokuwa wametekwa na kundi la magaida wa Kipalestina kwenye ndege ya Ufaransa. Katika kutimiza adhma hiyo askari wa Kiganda 20 waliokuwa wakilinda uwanja wa ndege usiku huo waliuwawa katika majibishano ya risasi na askari wa KiIsrael. Kamanda wa oparesheni ile aliyewaongoza makomando hao wa Israel alikuwa anaitwa Jonathan Netanyahu aka Joni, ambaye ni kaka wa waziri wa sasa wa Israel Bwana Benjamin Netanyahu, alipigwa risasi na askari wa Kiganda na kufia pale Entebbe.

Akiwa Waziri Mkuu wa Israel Ben Netanyahu anatembelea Uganda na kutakuwa na shughuli za kuadhimisha miaka 40 toka tukio hilo lifanyike na kwa upande wa Ben Netanyahu kwake binafsi atakuwa kaja kuona alipoangukia kakake. Kwa WaIsrael hii iko sawa, je kwa WaGanda hii imekaaje.
 
Back
Top Bottom