Netanyahu ataka Trump apewe tuzo ya Nobel

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amempendekeza Rais Trump kwa tuzo ya Amani ya Nobel na kwamba ameshatuma barua kwa kamati ya tuzo ya Nobel juu ya pendekezo lake hilo. Rais wa Marekani Donald Trump amesema ana matumaini kwamba Hamas wako tayari kuafikiana juu ya kuwaachilia mateka na usitishaji wa mapigano Gaza. Trump ameyasema hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya Marekani usiku wa kuamkia leo.

Viongozi hao wawili wamekutana kwa mara ya tatu mwaka huu na katika ziara hii ajenda kuu kati yao ilikuwa ni kujadili jinsi ya kuvimaliza vita vya Gaza vya zaidi ya miezi 21 kati ya Israel na Hamas.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amempendekeza Rais Trump kwa tuzo ya Amani ya Nobel na kwamba ameshatuma barua kwa kamati ya tuzo ya Nobel juu ya pendekezo lake hilo.

Trump amekuwa akijinasibu kama mpatanishi wa amani na amekuwa akitaka kutambulika kwa mchango wake wa upatanishi katika migogoro duniani ikiwemo mgogoro wa hivi karibuni kati ya India na Pakistan, pamoja na Serbia na Kosovo.
 
John Bolton gave away that secret he is obsessed why Obama got the Nobel Prize, na yeye anataka apewe.

Siku hizi kila nchi inatumia hiyo flattering tactic itampendekeza Trump apewe Nobel. Walianza Pakistan kabla ya Israel/Israel 12 days conflict. Baada ya US kuangusha mabomu Iran na Pakistan nao wakatangaza kuondoa support yao ya Nobel.

Sasa hivi kila mtu akitaka kitu kutoka US wanaanza na kumpendekeza for Nobel. Iła Trump saa zingine anakuwa kama mtoto.
 
Hiyo tuzo ya Nobel itakuwa haina thamani tena akipewa Trump wakati yeye ndio anachochea migogoro zaidi akiona anae msupport anazidiwa ndio anageuka msuluhishi
 
Hizo tuzo huwa hazina vigezo, ni mtu anasema fulani apewe na anapewa?

Asipewe amalizane na Iran kwanza.
 
Kichwa cha habari kingependeza kuwa
"Kichaa ampa tuzo kichaa mwenzake"

Trump akipewa tuzo ya Nobel basi haitakuwa na maana tena...
 
Yeye nani huyo mpaa asema Trump apewe Nobel, ikiwa vita vya Iran alikuwa hana sauti mpaa Trump ndio akasema vita visimame. Israel si mtumishi tu anatimwa kafanye hivi fanya hivi alipozidiwa mwenye amri akaingia direct.

Niliwambia humu watu Israel ni show off tu hana lolote, walivyo anzwa tandikwa Tela Aviv Trump alirusha taulo jeupe 😆 😂
 
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amempendekeza Rais Trump kwa tuzo ya Amani ya Nobel na kwamba ameshatuma barua kwa kamati ya tuzo ya Nobel juu ya pendekezo lake hilo. Rais wa Marekani Donald Trump amesema ana matumaini kwamba Hamas wako tayari kuafikiana juu ya kuwaachilia mateka na usitishaji wa mapigano Gaza. Trump ameyasema hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya Marekani usiku wa kuamkia leo.

Viongozi hao wawili wamekutana kwa mara ya tatu mwaka huu na katika ziara hii ajenda kuu kati yao ilikuwa ni kujadili jinsi ya kuvimaliza vita vya Gaza vya zaidi ya miezi 21 kati ya Israel na Hamas.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amempendekeza Rais Trump kwa tuzo ya Amani ya Nobel na kwamba ameshatuma barua kwa kamati ya tuzo ya Nobel juu ya pendekezo lake hilo.

Trump amekuwa akijinasibu kama mpatanishi wa amani na amekuwa akitaka kutambulika kwa mchango wake wa upatanishi katika migogoro duniani ikiwemo mgogoro wa hivi karibuni kati ya India na Pakistan, pamoja na Serbia na Kosovo.
Na Mimi naunga mkono Trump apewe hiyo tuuzo kwa jinsi alivyowaokoa waajemi kutoka kwenye kipigo cha wayahudi Mungu pekee ndo anajua.
 
Hiyo tuzo ya Nobel itakuwa haina thamani tena akipewa Trump wakati yeye ndio anachochea migogoro zaidi akiona anae msupport anazidiwa ndio anageuka msuluhishi
Trump alikuta vita moja ya ukrain ila sasa ameaznisha vita nyingien tatu
Iran -israel
China -usa - taarif
Halafu anataka apewe tuzo ya amani mbona kichekesho
 
Swali langu ni kwamba kwanini baada ya vita vya iran kumalizika jamaa akaemda marekani?

Nahisi kuna jambo ambalo haliko sawa kwa watu wote 2, kwa nini wakutane sasa?
 
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amempendekeza Rais Trump kwa tuzo ya Amani ya Nobel na kwamba ameshatuma barua kwa kamati ya tuzo ya Nobel juu ya pendekezo lake hilo. Rais wa Marekani Donald Trump amesema ana matumaini kwamba Hamas wako tayari kuafikiana juu ya kuwaachilia mateka na usitishaji wa mapigano Gaza. Trump ameyasema hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya Marekani usiku wa kuamkia leo.

Viongozi hao wawili wamekutana kwa mara ya tatu mwaka huu na katika ziara hii ajenda kuu kati yao ilikuwa ni kujadili jinsi ya kuvimaliza vita vya Gaza vya zaidi ya miezi 21 kati ya Israel na Hamas.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema amempendekeza Rais Trump kwa tuzo ya Amani ya Nobel na kwamba ameshatuma barua kwa kamati ya tuzo ya Nobel juu ya pendekezo lake hilo.

Trump amekuwa akijinasibu kama mpatanishi wa amani na amekuwa akitaka kutambulika kwa mchango wake wa upatanishi katika migogoro duniani ikiwemo mgogoro wa hivi karibuni kati ya India na Pakistan, pamoja na Serbia na Kosovo.
Yeye Mwenyewe anatafutwa na ICC lini kajua samani ya Aman ¿¿

kweli IRAN iliwasha MOTO bado kuna wajinga wanawaza Israel kuja kuichokoza Iran tena. !!! Mpaka kesho Netanyahu anamshukulu Trump kwa kuzuiya viuma vya Iran visiendelee kutua Telaviv..
 
Back
Top Bottom