Neno ndoto linavyoathiri dhamira katika maisha halisi

bestboy

Senior Member
Oct 18, 2012
130
225
Nimekaa na kutafakari kwa muda sasa jinsi neno ndoto linavyotumika katika maisha yetu katika kufikia malengo tunayojiwekea na kugundua kwamba lina athari kubwa kuelekea kwenye kutimiza tunayoyatarajia.
Kwanza kwa tafsiri ya neno lenyewe NDOTO ni mfululizo wa picha, mawazo, mihemko na hisia ukiwa usingizini, hii inaleta maana kwamba ndoto si jambo halisi bali ni hisia au mawazo ukiwa usingizini.
Nikirudi kwenye mada yangu ni kwamba, nimesikia watu wengi wakisema "Nina ndoto ya kuwa daktari, mwalimu, engineer" au kazi nyingine yoyote mhusika anayoipenda au kutamani kuifanya, kauli hii hupelekea wengi wao kushindwa kutimiza nia zao au malengo yao sababu tu ya neno ndoto waliloanza nalo.
Unapotaka kuwa mtu fulani katika maisha yako ni vyema ukatumia kauli ya kusema "Nataka kuwa daktari, mwalimu , engineer n.k. badala ya kusema nina ndoto ya kuwa daktari, mwalimu , engineer n.k" kuweka neno "ndoto" kunafanya dhamira yako ibaki kuwa ndoto bila kutimia.
Kusema nataka kuwa, kunatengeneza akili yako kupambana kutimiza dhamira hiyo katika hali yoyote ile tofauti na neno ndoto linaloifanya akili irelax kusubiri miujiza huku ikipambana kwa taratibu zaidi.

Tusiwe na ndoto, tudhamirie kuwa tunavyotaka.
 

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,603
2,000
Ulipaswa kuwa pastor wa kipentekoste.
Huko wengi huangamizwa kwa haya mambo ya ndoto.
Nice message.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom