Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 710
- 1,610
Leo asubuhi The Chanzo wameondoa press ya Gwajima YouTube wakiweka wazi kuwa wametakiwa kuondoa story hiyo na TCRA sababu press hiyo imekosa 'Mizania', hawakulance kwenye namba ya watu waliotekwa nchini kwa kwenda kuihoji mamlaka serikali na hivyo kusababisha wananchi kuichukia serikali yake!š¤£š¤£
Wengine waliondoa kimyakimya ikiwa ni tetesi tu kuwa serikali ilishapeleka vitisho ila The Chanzo wametuweka wazi, kuwa ni serikali ndio imetaka hayo kwa kutumia hiyo hoya ya mizania.
Lakini tukiangalia hili kwa undani ni kweli ni kuhusu 'mizania (kubalance)' story au ni sababu jambo ni gumu na serikali hawana majibu hivyo ili wakimbie kusulubiwa basi wanakimbilia kuzuia maudhui hayo hasa ukizingatia sasa wananchi wanafuatilia kwa karibu mwenendo wa kisiasa kuelekea uchaguguzi mkuu Oktoba?
Kama mnakumbuka mwishoni wa 2024 Tanganyika Law Society (TLS) walitoa orodha ya watu waliotekwa, ikiwemo mazingira waliyotekwa pamoja na status yao. Mbona hatukuona mambo za kubalance? Au sababu waliofanya hawakuwa media na hawakuwa na njia ya kuweza kuwabana?
Kwanini waje kuzuia haya kwa Gwajima? Kwasababu kupitia media wananchi wengi zaidi watademand uwajibikaji? Uko wapi uhuru uliohakikishiwa na katiba kuhakikisha wananchi wanapata taarifa?
Kwanini kimewafanya serikali wasijibu toka TLS walipotoa ripoti yao? Si si sawa na hiki alichoongelea Gwajima? Ni sababu TLS hawana wafuasi wengi kwa taarifa kufika katika kila upande wa Tanzania?
Na kuhakikisha mnaziminya zaidi media mkaja na bodi ya ithibati, ambayo huko mbeleni mtataka kila maudhui yawe yanapitiwa kama upuuzi wanaofanya BASATA ili kuwe na habari za uchawa tu.
Hili linatakiwa kukemewa kwa nguvu zote, wanaoathirika sio media pekee, ni mpaka wewe mlaji wa mwisho unaotegemea media hizi kukupa taarifa zenye tija kwa maslahi ya taifa wakati wote. Fikiria taarifa zote zikiwa zinasifia tu serikali tutakuwa tunaishi kwenye jamii gani ambayo haiwezi kutofautisha kati ya mbivu na mbichi?
Wabunge hawa wanaenda kuwa mawaziri mpaka Rais tunawachagua sisi, uchawa ni sisi ndio tufanya uendelee, tukiamua ukome utakoma leo, yaani kiufupi maamuzi yako mikononi mwetu kukemea kila aina ya ushenzi unafanyika nchini. Kazi kwetu kuendelea kuechekea haya yaendelee ama lah!