Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,582
NENO LANGU KWAKO … SOMA TAFADHALI ..
Jambo la kwanza kumbuka kwamba hakuna mtu anayejali mambo / maisha yako zaidi ya wewe mwenyewe! Na kila mtu ana muda sawa na mwingine, kwa siku kila mtu amepewa masaa 24 tu. Anza kwa kuzingatia mda, ugawe muda wako katika makundi kwa utashi wako ukizingatia kuwa kila utakachojipangia unakifanya ndani ya muda ulioupanga.
MUDA NI MALI, JALI MUDA WAKATI NA MAHALI
Kwa lolote unalotaka kulifanya lipangie unalifanya lini, mda gani na sehemu ipi.
Mfano!
Siku inaanza saa sita za usiku
– Anza kwa maombi! Haya inabidi yawe maombi ya mda mrefu; maombi unayopaswa kuomba hapa ni kuziweka haja zako mbele ya Bwana.
Alfajiri – Kagua makazi yako ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya mwili
Asubuhi – Tafakari mambo unayopaswa kuyafanya kwa siku hiyo na tanguliza maombi kabla ya kuyafanya.
Mchana – Maombi mafupi (Kumbuka huu ni muda wa chakula cha mchana)
Alasiri – Tafakari kazi ulizozifanya kwa siku hiyo
Jioni – Ongea na marafiki / familia n.k
Usiku – Sala fupi na kupumzika.
Yale yote unayopanga kuyafanya kamwe hayawezi kufanikiwa iwapo hautaujali muda. Na hii ndo tofauti kubwa kati ya watu matajiri na maskini. Lolote unalolifanya ndani ya muda lazima likuletee mabadiliko chanya kwenye maisha yako.
TUENDELEE KUSHAULIANA MEMA ZAIDI ILI TUFIKE SALAMA KULE TUNAKOELEKEA.
Nikutakieni mwanzo wa mwaka mpya 2017 wenye watanzania waliobadilika na kujali muda.
Yours;
Tutor B - Creative Director