Neno lako ni Upanga — Kiwango halisi cha Christo Frequency

Neno lako ni Upanga — Kiwango halisi cha Christo Frequency

Boloski

Member
Joined
Apr 7, 2025
Posts
16
Reaction score
28

Katika viwango vya siri vya mafundisho ya zamani, tulifundishwa kuwa:​


"In the Beginning was the Word, and the Word was God." (Yohana 1:1)

Lakini si kila mtu ataelewa ufunguo wa ndani wa mstari huu.
Neno halikuwa tu sauti — Neno lilikuwa Frequency ya Uumbaji katika ulimwengu huu.
Christo Frequency
ni sauti inayotengeneza Ulimwengu mpya ndani yako na ulimwengu huo ndio utakao jidhihirisha kwa nje.

Wakati unazungumza, hupeleki tu mawazo fikra zako ila — unatuma frequency ambayo ama:
  • Inajenga (Creative Current)
  • Inaharibu (Destructive Current)
Christo Consciousness ni hali ambapo maneno yako hayabebi tu maana — yanabeba Muundo wa Mungu ndani yake. Maneno yako yanakuwa kama laser beam — yanakata giza na kutengeneza mwanga.

Kanuni ya Siri:
Unapozungumza kutoka kwenye moyo safi, uliojaa imani, maneno yako huvaa Mwili wa Nuru (Light Body) na hupeleka miujiza kwa kasi isiyo ya kawaida.



🔱 Somo la Leo:
Usiongee kwa hasira au kwa hofu. Kila neno lako litumike kama chombo cha kuunda.
Maneno ya woga yanatengeneza minyororo ya mahangaiko.
Maneno ya Imani na upendo yanatengeneza Milango ya faida na baraka.

Maneno yako ni daraja la kuvuka kutoka dunia ya mateso hadi dunia ya miujiza.
Leo chagua kuzungumza kwa kiwango cha Christo — kiwango cha Miujiza.

Anza kwa kusema "Sauti yangu ni mwali wa Nuru. Neno langu ni Ulimwengu unaozaliwa."
 
Back
Top Bottom