IAmShedeOne
JF-Expert Member
- Jul 2, 2015
- 202
- 385
NENO LA MATUMAINI.
SIKU moja kundi kubwa la vyura likiwa linahama sehemu moja kwenda nyingi, kwa bahati mbaya vyura wawili wakatumbukia kwenye shimo. Kutokana na urefu wa shimo hilo, vyura waliobaki nje waliwaambia wenzao wawili kuwa, hakuna uwezekano wa kuwaokoa.
Pamoja na maneno hayo, vyura hao wawili waliendelea kuruka huku na kule, wakijaribu kutoka shimoni. Bila kujali jitihada zao, kundi la vyura kule juu liliendelea kuwaasa wenzao watulie tu na kusubiri kifo, kwani hakuna namna ya kuwaokoa.
Mwishowe, chura mmoja katika shimo, alikata tamaa kwa maneno ya wenziye, akaanguka kwa kujipiga chini na kufa. Aliyebaki hai, aliendelea na kuendelea kuruka huku na kule ili kujiokoa. Kwa simanzi na masikitiko, vyura wenziye waliendelea kumwambia atulie tu, asijisumbue, kwani hakuna uwezekano wa kutoka humo, na kwamba ni bora asubiri kufa taratibu kuliko kujichosha na kufa kwa uchungu mkubwa.
Bila kukata tamaa, Chura yule aliendelea kuruka na kuruka zaidi, mpaka hatimaye akafanikiwa kutoka. Akiwa nje ya shimo, vyura mwenziye walimuuliza: "Hatukutegemea kama utaokoka. Ni kipi kilikufanya uamini kuwa utaokoka, mpaka ukapuuza ushauri wetu wa kijinga?"
Chura hakuwajibu. Wakamuuliza tena, hawakujibiwa. Baada ya muda ndipo wakagundua kwamba mwenzao alikuwa kiziwi, hakuwa akiwasikia kwa kila walichomuuliza. Walipojaribu kuwasiliana naye kwa vitendo, ndipo aliwaambia kwamba, akiwa shimoni hakujua kama walikuwa wakimwambia atulie, bali alijua wenziye wanampigania kwa kumtia moyo wa matumani na kumtaka aendelee kuruka. Na kweli aliendelea kuruka kwa moyo mmoja akiamini atafanikiwa, na kweli akafanikiwa.
Hiyo ndiyo nguvu ya maneno, yanaweza kuponya na yanaweza kuangamiza. Chura wa kwanza aliposikia maneno ya kukatishwa tamaa; alichoka, akakata tamaa na kufa. Lakini chura wa pili alipohisi anatiwa moyo, alizidi kupambana na hatimaye alitoka. Hivyo basi, kabla hujatoa neno kinywani mwako, tafakari mara mbili kama litaokoa ama kuangamiza.
***